Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

WAMECHOMOA… Watoto wa mastaa waliokimbia soka

Muktasari:

  • Mara kadhaa imekuwa kutokea watoto wa wachezaji wa mpira wa miguu kuja kuonyesha kiwango bora kukifikia kile cha wazazi au hata kukivuka.

KUNA msemo usemao kwamba “mtoto wa nyoka ni nyoka” au ule wa “maji hufuata mkondo”. Watu wamekuwa wakitumia misemo hiyo mara nyingi wanapoona mtoto anafuata nyayo za wazazi katika jambo fulani wanalofanya au walilowahi kulifanya wazazi wake.

Mara kadhaa imekuwa kutokea watoto wa wachezaji wa mpira wa miguu kuja kuonyesha kiwango bora kukifikia kile cha wazazi au hata kukivuka.

Hata hivyo, jambo hilo huwa halitokei mara zote. Kuna nyakati watoto wa wachezaji huamua kuchagua njia tofauti ama baada ya kucheza mpira kidogo au hata kabla ya kucheza.

Leo tunakusogezea baadhi ya watoto wa wachezaji ambao walipita njia tofauti na zile za wazazi waliozoacha rekodi na heshima kubwa katika soka.


BROOKLYN BECKHAM

Mguu wa kulia wa David Beckham una historia ya aina yake katika soka. Beckham aliacha heshima kubwa katika kikosi cha Manchester United, PSG, Real Madrid pamoja na timu ya taifa ya England ambako aliwahi kuhudumu kama nahodha.

Becks alikuwa zaidi ya mchezaji, bali nyota wa taifa lake na klabu.

Wakati anaelekea ukingoni, macho na masikio ya mashabiki wengi wa soka yaliangukia kwa mwanawe mkubwa, Brooklyn Beckham wakiamini kwamba  anaweza kurithi kipaji cha baba yake.

Brooklyn alianza kuonyesha uhai kwenye hilo ambapo alianza maisha yake ya soka kwa kujiunga na akademi ya Arsenal, lakini akiwa na umri wa miaka 16 aliachwa kwa kile kilichoelezwa kwamba hakuonekana kuwa na kipaji.

Kulikuwa na shinikizo kubwa la watu waliotaka kuona akivaa viatu vya baba yake, lakini kiuhalisia Brooklyn  mpira haikuwa sehemu ya ndoto zake.

Baada ya kuachwa na Arsenal aliamua kwenda kufanya kitu anapenda ambacho ni kuwa mpiga picha za wanamitindo na fasheni.


CRISTIAN TOTTI

Francesco Totti hakuwa tu mchezaji, bali alipewa ‘mfalme’ na nahodha wa kihistoria wa timu ya AS Roma yenye maskani yake Italia kutokana na heshima aliyoipata baada ya kuichezea katika maisha yake yote ya soka hadi alipostaafu.

Totti ambaye ni mshindi wa Kombe la Dunia akiwa na timu ya taifa ya Italia, wakati anaenda kustaafu mashabiki wengi wa Roma waliamini kuwa mtoto wake Cristian Totti ambaye wakati huo alikuwa katika akademi ya timu hiyo angeweza kuvaa viatu vyake siku moja.

Lakini, soka huwa lina mambo ya kikatili. Cristian hakufanikiwa hata kupanda kufikia timu ya wakubwa ya Roma na baada ya kucheza kwa muda katika timu za vijana alitolewa kwa mkopo, kisha baadaye akaachwa na sasa akiwa na umri wa miaka 20, amestaafu soka huku klabu yake ya mwisho kuichezea ikiwa Olbia inayoshiriki Ligi Daraja la Nne. Kwa sasa kijana ameamua kuwekeza muda wake zaidi katika masomo ya biashara.


BENJAMIN AGUERO

Dogo ni mtoto  Sergio Aguero ambaye jina lake kamili ni Benjamin Aguero Maradona. Wakati baba na babu yake wote ni wachezaji, dogo ameweka wazi kwamba anapenda kuja kuwa mwanamuziki.

Aguero ameoa mtoto wa Maradona, hivyo Benjamin babu yake ni mwanasoka huyo aliyefariki miaka ya karibuni  mwenye heshima kubwa katika soka. Pia baba yake mkubwa ni Lionel Messi.

Wakati watu wengi walitarajia afuate nyayo za malejendi hao, yeye aliamua kupita njia tofauti.

Awali Aguero alijaribu kumpeleka kucheza soka katika akademi ya  Tigre na Independiente, lakini mtoto ameonekana kutopenda mchezo huo na amesisitiza kwamba anachotaka kwa sasa ni kuimba tu.


WILL SHEARER

Will ni mtoto wa lejendi wa Newcastle, Allan Shearer. Baba yake ana rekodi kibao ambazo zimeendelea kuishi na hazijavunjwa katika Ligi Kuu England hadi sasa.

Miongoni mwa rekodi zinazoishi ni ile ya kuwa mchezaji pekee kufunga mabao zaidi ya 100 akiwa na klabu mbili tofauti akifanya hivyo akiwa na Blackburn pamoja na Newcastle. Pia anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi ndani ya boksi katika historia ya ligi hiyo akifanya hivyo mara 227.

Mambo yamekuwa tofauti kwa mtoto wake, Will Shearer ambaye hakuwa akipenda masuala ya mpira wa miguu na badala yake anacheza gofu.


GEORGIE TERRY

Kila shabiki wa Chelsea anafahamu vizuri kazi kubwa ambayo beki wa zamani wa kimataifa wa England, John Twery aliiweka wakati akiwa mchezaji kabla ya kurejea kwa sasa ambapo anafanya kazi kama mkufunzi wa akademi.

Terry ana watoto ambao ni pacha wa kiume Georgie John Terry na wa kike Summer Rose Terry.

Kama ilivyo kwa malejendari wengi, watoto hao wote wamekataa kufuata nyayo za baba. George alihitimu masomo ya uchumi 2024 na sasa anafanya kazi kwenye moja ya taasisi huko England, huku dada yake akiendelea na masomo.