Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mke mlishe hivi mumeo

Muktasari:

  • Kipindi cha mapumziko si ruhusa ya kula kila kitu kinachoonekana mbele ya macho. Kama unaishi na mwanamichezo, huu ndio muda ambao unaweza kumsaidia kulinda afya yake kuliko hata kipindi cha mashindano.

Mke, mlishe hivi mumeo kipindi hiki cha mapumziko kama ni mwanamichezo anayetaka kurudi uwanjani akiwa fiti.

Kipindi cha mapumziko si ruhusa ya kula kila kitu kinachoonekana mbele ya macho. Kama unaishi na mwanamichezo, huu ndio muda ambao unaweza kumsaidia kulinda afya yake kuliko hata kipindi cha mashindano.

Sahani anayokula leo inaweza kuamua kama atarudi mazoezini akiwa mwepesi na mwenye nguvu au akiwa ameongeza uzito na kupoteza ubora wake.

Wanamichezo wengi huingia katika mapumziko wakiamini wanaweza kula bila mipaka kwa sababu hawana mechi za kila wiki.

Hata hivyo, wataalamu wa lishe wanaeleza kuwa mwili bado unahitaji virutubisho bora ili kuendelea kujijenga, kurekebisha misuli na kujiandaa kwa msimu unaofuata.


SIO KILA SIKU VYAKULA VYA MAFUTA

Mapumziko si tiketi ya kula chipsi, kuku wa kukaanga, maandazi, keki na vyakula vingine vyenye mafuta mengi kila siku. Vyakula hivyo vinaweza kuongeza kiwango cha uzito kwa kasi, jambo linaloweza kufanya mwanamichezo aanze maandalizi ya msimu mpya akiwa hayupo tayari kimwili.

Badala yake, mlo uwe na mafuta yenye afya kutoka kwenye parachichi, karanga au mbegu kwa kiasi kinachofaa.


USISAHAU PROTINI

Misuli haihitaji protini wakati wa mazoezi pekee. Hata kipindi cha mapumziko mwili unaendelea kujirekebisha.

Vyakula kama samaki, kuku asiye na ngozi, mayai, maharage, dengu na nyama isiyo na mafuta mengi vinaweza kusaidia mwili kuendelea kujenga na kutunza misuli.

Lengo si kula protini nyingi kupita kiasi, bali kuhakikisha zinapatikana kwenye milo ya kila siku kwa uwiano unaofaa.


WANGA KIDOGO

Watu wengi huamini mwanamichezo anatakiwa kuacha kabisa wanga akiwa mapumzikoni. Hilo si kweli kabisa .

Kinachobadilika ni kiasi cha wanga kulingana na kiwango cha shughuli anazofanya. Chagua wanga wenye nyuzinyuzi kama wali, viazi vitamu, ndizi za kupika, mihogo, magimbi na nafaka zisizokobolewa.


MATUNDA NA MBOGA MBOGA

Rangi nyingi kwenye sahani mara nyingi huashiria aina nyingi za virutubisho.

Mboga za majani, karoti, nyanya, pilipili hoho na matunda mbalimbali hutoa vitamini na madini chuma (dagaa) vinavyosaidia mwili kujikinga na magonjwa na kuchangia afya ya misuli na ngozi.

Ni vizuri sehemu ya kila mlo iwe na mboga au matunda.


MAJI MENGI KULIKO SODA

Wapo wanaodhani kwa kuwa hakuna mazoezi makali basi kunywa maji si jambo la kuzingatia.

Ukweli ni kwamba mwili bado unahitaji maji ya kutosha kwa kazi zake zote. Maji husaidia mmeng’enyo wa chakula, usafirishaji wa vyakula na utendaji wa misuli.

Badala ya kutumia soda au juisi zenye sukari nyingi kila siku, maji yanapaswa kuwa kinywaji kikuu isipokuwa pale ambapo kuna sababu maalum.


ACHANA NA HIVI

Pipi, chokoleti, biskuti, keki na vinywaji vyenye sukari nyingi vinaweza kuongeza ulaji wa kalori bila kuongeza virutubisho muhimu.

Hii haimaanishi havipaswi kuliwa kabisa, bali ni vyema vitumike kwa kiasi badala ya kuwa sehemu ya kila siku ya mlo.


ASUBUHI MUHIMU

Baadhi ya wanamichezo hubadilisha ratiba zao kipindi cha mapumziko na kuamka kuchelewa kiasi cha kuruka kifungua kinywa.

Mlo wa asubuhi unaweza kusaidia kupata virutubisho muhimu kwa siku nzima. Chakula kizuri kinachofaa kwa wakati huo kinaweza kujumuisha mayai, uji wa nafaka zisizokobolewa, mtindi usio na sukari nyingi, matunda au mkate wa nafaka kamili.


USIACHE HIVI

Badala ya kula chipsi au vitafunwa vilivyosindikwa kila mara, fikiria matunda, karanga kwa kiasi, mtindi usio na sukari nyingi au mahindi yaliyochemshwa. Hivi vinaweza kusaidia kushiba na kuongeza virutubisho muhimu.


KULALA KWA WAKATI NI LISHE

Hakuna mlo bora unaoweza kufidia usingizi mbovu. Kipindi cha mapumziko ni nafasi ya mwili kujirekebisha, hivyo kulala kwa muda wa kutosha pamoja na kula lishe bora kunaweza kusaidia mwanamichezo kujiandaa vizuri kwa msimu unaofuata.


USHAURI WA ANTI

Kwa kifupi, mapumziko hayamaanishi kuacha kujali Afya yako na kila chochote tu. Badala yake, ni muda wa kuupa mwili nafasi ya kupona huku ukiendelea kupata virutubisho vinavyohitajika.

Sahani ya mchezaji inatakiwa isikosekane protini, wanga, mboga, matunda, mafuta yenye afya na maji ya kutosha inaweza kuwa msingi mzuri wa kumsaidia mwanamichezo kurejea mazoezini akiwa katika hali nzuri.