Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Waliotolewa Kombe La Dunia huenda walipata mchoko

DOKTA Pict

Muktasari:

  • Mchezo huo ambao uliwakutanisha miamba ya soka ulichezwa katika uwanja wa Dallas Arlington, ilishuhudiwa mabingwa hao mara mbili wa Kombe la Dunia wakitupwa nje kirahisi.

USIKU wa Jumanne ya Julai 14, 2026 ulikuwa mbaya kwa nchi ya Ufaransa mara baada ya kufungwa mabao 2-0 na timu ya Taifa ya Hispania katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Dunia la FIFA 2026.

Mchezo huo ambao uliwakutanisha miamba ya soka ulichezwa katika uwanja wa Dallas Arlington, ilishuhudiwa mabingwa hao mara mbili wa Kombe la Dunia wakitupwa nje kirahisi.

Katika hatua hii ya nusu fainali huwa ni kawaida kwa timu nzuri hapo mwanzoni kuboronga kutokana tatizo la mchoko wa mwili na akili.

Hapo jana siku ya Jumatano, mahasimu wa kihistoria, England na Argentina walipambana katika hatua ya nusu fainali nyingine.

Mechi zote za hatua hii huwa ni kawaida kuwaona wachezaji baadhi wakicheza chini ya kiwango kutokana na kung’ang’aniwa na hali ya mchoko wa kucheza mfululizo.

DOKT 01

Chanzo cha kutolewa kwa timu hizo na kushindwa kufika fainali huenda kilikuwa ni mchoko kutokana na kucheza mfululizo.

Kadiri mchezaji anavyotumika mfululizo ndivyo pia hatari ya kupata mchoko huwa kubwa. Kitabibu mchoko hujulikana kama fatigue, huweza kuwa kikwazo kwa mchezaji kucheza kwa kiwango.

Mchezaji kutumika mfululizo huwafanya kutumia nguvu nyingi sana, lakini mwili nao huwa na kiwango chake cha ustahimilivu. Hali ya misuli kufanya kazi kupita kiasi huweza kuleta uchovu.

Ukitazama kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa siku ya Jumanne hawakuwa katika kiwango chao kilichoonekana katika mechi za awali.

DOKT 02

UCHOVU WANAUDHIBITI KAMA HIVI

Timu ambayo imeweza kutinga hatua ya fainali ina maana kuwa wachezaji wake wana bechi bora la ufundi ikiwamo wataalamu wa tiba na wa mazoezi ya viungo.

Uchovu unaotokana na mwili kufanya kazi sana, huwa ni tatizo la muda tu ambalo linaweza kuisha na mchezaji kurudi na nguvu mpya.

Wachezaji wanaweza kupata uchovu zaidi kwa kucheza mechi ngumu, kutokunywa maji mengi kabla na baada ya mechi, kucheza katika joto kali, kutopasha na kunyoosha viungo, lishe duni, kutopumzika, kusafiri umbali mrefu na kufanya mazoezi magumu kabla ya mechi.

Mara tu baada ya kumaliza mechi wachezaji huendelea na utaratibu wa kunywa maji mengi kwani mtakumbuka mashindano haya yanafanyika kipindi hiki cha joto kali, hivyo wachezaji wanapoteza maji mengi kirahisi.

Moja ya vitu vinavyochangia wachezaji kupata uchovu mkali ni upungufu wa maji mwili.

DOKT 03

Hunywa maji mengi ikikadiriwa lita 2-3 pamoja na matunda au juisi za matunda au vinywaji maalum vijulikanavyo kama sports drinks.

Huendelea kufanya mazoezi mepesi ya kunyoosha misuli ya mwili asubuhi na jioni.

Hufanya usingaji wa mwili yaani massage kwani ni mbinu mojawapo ya kuondokana na uchovu.

Usingaji huwezesha mishipa ya damu kutanuka hivyo damu kwenda kwa wingi katika misuli hivyo kuondoa uchovu kirahisi.

Hujichanganya katika vituo maalum ambavyo huwa na huduma hizi pamoja na huduma ya mvuke na moto mkavu.

Kwenye vituo hivyo huweza pia kuoga maji ya vuguvugu au katika mabafu yakisasa maalum yenye kutoa mvuke wa joto au barafu, hii husaidia kuondokana maumivu na uchovu wa mwili.

Wengi huenda kujipumzisha katika maeneo yenye hewa safi ya wazi au ufukweni na kuishi katika hoteli au makazi yasiyo na  msongamo wala uchafuzi wa kelele ikiwamo ufukweni au maeneo ya wazi. Ikumbukwe kuwa mazingira ya hewa chafu yanachangia kuongeza uchovu wa mwili kwani misuli inahitaji kutumia hewa safi yenye oksijeni ili kuondoa uchovu.

DOKT 04

Hula mlo kamili ikiwamo vyakula vyenye protini, mboga za majani na matunda na wanga kwani inasaidia kukurudishia nguvu iliyotumika na pia kurudishia akiba ya nishati katika misuli.

Protini ndio mlo unaowezesha misuli kujijenga na kufanya kazi yake kwa ufanisi na pia inatumika katika misuli wakati wa kukunjuka na kujikunja.

Lishe bora husaidia mwili wa mchezaji majeruhi aliye mapumzikoni kupona haraka kwasababu huwa na viini lishe vinavyosaidia misuli kuondokana na mchoko wa mwili.

Huwa na umakini sana katika lishe kwani ulaji holela huweza kumfanya mchezaji kuwa mvivu, kunenepa au kuongezeka uzito.

Hula mlo wa jioni au usiku masaa 2-3 kabla ya kulala kwani kula tu na kulala kunasababisha kuamka na uchovu hii ni kwasababu mwili unatumia muda mwingi kusaga chakula badala ya kujikarabati.

Kulala ni moja ya tiba nzuri ya uchovu wa mwili, mchezaji huitajika kulala masaa 6-8 mfululizo kwa usiku mmoja pasipo usumbufu wowote.

Hujiepusha na mambo yoyote yanayoweza kumpa msongo wa mawazo, sonona na shinikizo la kiakili kwani mambo haya ni hisia hasi ambazo zinaongeza uchovu wa mwili.

Huepuka na matumizi ya unywaji pombe kupita kiasi, matumizi ya tumbaku ikiwamo uvutaji sigara kwani vyote hivi vinachangia kuongeza uchovu wa mwili.

Kila baada ya mechi wachezaji kupata burudisho la akili ili kuupa mwili utulivu hatimaye  mwili huweza kukabiliana na mchoko kwa ufanisi wa hali juu.