Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

VICHWA VIKALI: Wako wapi wakali 10 wa Ballon d’Or iliyowatosa Ronaldo na Messi

New Content Item (1)
New Content Item (1)

Muktasari:

  • Masupastaa hao wawili, Messi na Ronaldo ushindani wao kwenye soka uliwafanya kutawala kwenye tuzo hiyo kwa zaidi ya miongo miwili, ambapo mmoja ameshinda mara nane na mwingine tano.

PARIS, UFARANSA: MARA ya kwanza tangu 2003, si Lionel Messi wala Cristiano Ronaldo ambaye ametajwa kwenye kuwania tuzo ya Ballon d’Or 2024.

Masupastaa hao wawili, Messi na Ronaldo ushindani wao kwenye soka uliwafanya kutawala kwenye tuzo hiyo kwa zaidi ya miongo miwili, ambapo mmoja ameshinda mara nane na mwingine tano.

Wakali hao ni kama walikuwa wameiteka tuzo hiyo kwa maana ya kuwapo kwenye mchuano karibu katika kila mwaka tangu 2003.

Kwenye Ballon d’Or 2003 si Messi wala Ronaldo alikuwamo kwenye kinyang’anyiro, ambapo ndo ilikuwa mara ya mwisho kwa tuzo hizo za ubora wa mchezaji binafsi duniani kutohusisha jina la mmoja wa masupastaa hao.

Na sasa mwaka huu, kwenye tuzo za Ballon d’Or zitakazotolewa Oktoba, mastaa hao hawapo. Mastaa waliotajwa kuwania tuzo hiyo ya Ballon d’Or 2024 ni Jude Bellingham, Hakan Calhanoglu, Dani Olmo, Dani Carvajal, Cole Palmer, Ruben Dias, Declan Rice, Artem Dovbyk, Rodri, Phil Foden, Antonio Rudiger, Alejandro Grimaldo, Bukayo Saka, Erling Haaland, William Saliba na Mats Hummels.

Wengine ni Federico Valverde, Harry Kane, Vinicius Jr, Toni Kroos, Vitinha, Ademola Lookman, Nico Williams, Emiliano Martinez, Florian Wirtz, Lautaro Martinez, Granit Xhaka, Kylian Mbappe, Lamine Yamal na Martin Odegaard.

Lakini, ushajiuliza wako wapi mastaa hao 10 wa mwisho ambao walichuana kwenye tuzo za Ballon d’Or, ambazo Ronaldo na Messi majina yao hayakuwapo wote kwa pamoja?

New Content Item (1)
New Content Item (1)

10. David Beckham

Aliingia kwenye tuzo hiyo miezi 10 baada ya kujiunga na Real Madrid akitokea Manchester United.

David Beckham hakuweza kushinda mwaka 1999 wakati alipozidiwa na Rivaldo.

Mwaka 2007, Beckham alishtua wengi alipoamua kuachana na Madrid na kwenda LA Galaxy, alikoenda kumalizia maisha yake ya soka kama mchezaji.

Staa huyo alicheza pia kwenye vikosi vya AC Milan na Paris Saint-Germain kabla ya sasa kumiliki timu huko Marekani, Inter Miami, ambayo anaichezea supastaa Lionel Messi.

WK6
WK6

9. Gianluigi Buffon

Buffon aliweka viwango vyake na kuwa mmoja wa makipa mahiri kabisa duniani katika miaka ya 2000. Ubora wa Mtaliano huyo ulikuwa unaongezeka kwa kadri anavyokwa mkubwa, ambapo aliisaidia Italia kunyakua ubingwa wa Kombe la Dunia 2006.

Mafanikio hayo yalimfanya kuwa namba mbili kwenye Ballon d’Or 2006, ambapo mshindi alikuwa Mtaliano mwenzake, Fabio Cannavaro.

Baada ya kutamba kwenye timu kibao, ikiwamo Juventus na PSG, kipa huyo alistaafu 2023 akiwa na Parma, huku akicheza zaidi ya mechi 1100.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

8. Roberto Carlos

Mchezaji aliyekuwa bora kabisa kwenye nafasi yake na kuwaacha mbali sana mabeki wa kushoto. Carlos alishika namba mbili kwenye tuzo hizo mwaka 2002, lakini alishindwa kuwamo kwenye tano bora mwaka uliofuatia wakati alipoiwezesha Real Madrid kushinda ubingwa wa La Liga msimu wa 2002-03.

Baadaye alikwenda zake Uturuki, akarudi kwao Brazil na kucheza pia Russia alikojiunga na Anzhi Makhachkala, kabla ya kustaafu soka mwaka 2016 baada ya kuichezea Dehli Dynamos.

Zaidi ya hapo, Carlos amekuwa tu akishiriki kwenye mechi za hisani kwa ajili ya kuchangia matukio mbalimbali ya kujitolea.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

7. Raul

Kabla ya CR7, kulikuwa na Raul huko Real Madrid. Mhispaniola huyo hakuhitaji jina la utani kujipatia umaarufu, alitamba kwa jina lake halisi alilopewa na wazazi wake. Hakika alikuwa anafunga mabao kama alivyokuwa anapenda.

Alishika namba mbili kwenye tuzo za Ballon d’Or 2001 na licha ya kwamba hakukaribia nafasi za juu kwenye tuzo za mwaka uliofuatia, lakini kipenzi hicho cha mashabiki wa Los Blancos alichaguliwa nahodha wa kikosi hicho cha Barnebeu.

Raul alimaliza soka lake baada ya kucheza kwenye sehemu kadhaa ikiwamo Ujerumani, Qatar na New York kabla ya kustaafu mwaka 2015. Kwa sasa amerejea Real Madrid, kuwa kocha wa timu ya vijana, Castilla.

WK8
WK8

6. Ruud van Nistelrooy

Straika wa mabao, Van Nistelrooy mabao yake 25 katika mechi 34 kwenye Ligi Kuu England zilimfanya ashinde Kiatu cha Dhahabu katika msimu wa 2002-03 na alichaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Msimu alipoisaidia Manchester United kunyakua ubingwa wa ligi hiyo.

Alifunga mabao 12 pia katika mechi nane za Ligi ya Mabingwa Ulaya ndani ya msimu huu, hivyo kumaliza namba sita kwenye Ballon d’Or 2003 ilikuwa pigo kubwa kwake, alistahili nafasi za juu zaidi ya hiyo.

Mdachi huyo kwa sasa amerudi tena Man United, kwenda kuwa kocha msaidizi wa Erik ten Hag kwenye benchi la ufundi la miamba hiyo.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

5. Zinedine Zidane

Baada ya kufanya kweli mwaka 2002 na kufunga bao matata sana kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, msimu wa Zinedine Zidane kwa mwaka 2003 ulikuwa safu, wakati alipokuwa akitamba kwenye safu ya kiungo ya Real Madrid sambamba na Mreno Luis Figo.

Zidane alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Fifa mwaka huo, licha ya kwamba kwenye Ballon d’Or alishinda namba tano.

Aliendelea kutamba kwa miaka mitano mingine kabla ya kutibua mambo kwenye fainali za Kombe la Dunia 2006, si tu kwa kukosa ubingwa, bali kwa kumpiga kichwa cha kifuani beki wa zamani wa Italia, Marco Materazzi.

Baadaye alirudi Real Madrid na kupata mafanikio makubwa zaidi kama kocha alipobeba Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa misimu mitatu mfululizo. Kwa sasa hana kazi tangu alipoachana na Los Blancos mwaka 2021.

WK7
WK7

4. Andriy Shevchenko

Shevchenko aliwasha moto na kuwa kwenye kiwango bora kabisa cha soka katikati ya miaka ya 2000, ambapo alishinda Scudetti na Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na kikosi cha AC Milan wakati alipojitengenezea hadhi ya kuwa gwiji wa kikosi hicho kwa kushika namba mbili ya wafungaji bora wa muda wote.

Baadaye alikwenda zake Chelsea, ambako hakuwa na wakati mzuri sana aliponaswa kwa Pauni 30 milioni kabla ya kurudi Rossoneri kwa mkopo mwaka 2008.

Alistaafu soka 2012 na kuingia kwenye siasa kwa muda mfupi kabla ya kuamua kuwa kocha. Shevchenko siku za hivi karibuni alikuwa Genoa, lakini alifutwa kazi 2022 na tangu wakati huo hana kazi.

New Content Item (1)
New Content Item (1)

3. Paolo Maldini

Aliyeingia kwenye tatu bora ya Ballon d’Or 2003 alikuwa mchezaji mwenzake Shevchenko na nahodha wa AC Milan, Paolo Maldini, ambaye alicheza bila ya kuruhusu bao akiwa na pacha wake Alessandro Nesta wakati Milan iliponyakua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuichapa Juventus kwenye mchezo wa fainali kwa mikwaju ya penalti.

Mtaliano huyo alitumikia AC Milan kwa muda wote wa maisha yake ya soka hadi hapo alipostaafu 2009 baada ya misimu 25 ya kuwa mchezaji.

Kwa sasa ni mmiliki mwenza wa klabu ya Miami FC, lakini pia ni mkurugenzi wa ufundi wa AC Milan, ambapo alihusika sana kwenye usajili wa mastaa wa maana waliofanya timu hiyo ishinde ubingwa wa Serie A kwenye msimu wa 2021-22.

WK9
WK9

2. Thierry Henry

Henry alimaliza nafasi ya pili kwenye tuzo za Ballon d’Or 2003, licha ya kwamba Arsenal ilishindwa kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huo.

Fowadi huyo Mfaransa alifunga mabao 32 katika michuano yote msimu huo na kuchaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mechi kwa kiwango bora kabisa alichoonyesha kwenye mechi ya fainali ya Kombe la FA, ambapo Arsenal ilinyakua ubingwa.

Msimu uliofuatia, Henry aliendeleza moto na kuwa kwenye kikosi cha Arsenal kilichocheza kwa msimu mzima bila ya kupoteza mechi kwenye Ligi Kuu England, lakini mambo yake hayakuwa mazuri kwenye Ballon d’Or. Mwaka 2007, Henry aliachana na Arsenal na kutimia zake Barcelona, kabla ya kwenda Marekani na baadaye, kurudi kwa mkopo Arsenal kabla ya kustaafu.

Kwa siku za karibuni amekuwa akijaribu kazi ya ukocha, aliongoza timu ya Ufaransa kushinda medali ya fedha kwenye Olimpiki ya Paris.

WK10
WK10

1. Pavel Nedved

Licha ya kwamba alipoteza mchezo wa fainali wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya ACMilan, Juventus ilishinda ubingwa wa Serie A katika msimu wa 2002-03 na kiungo Pavel Nedved alikuwa mtu muhimu kwenye kikosi hicho cha Juventus kwenye michuano yote hiyo, wakati alipokuwa na kazi ya kuziba pengo la Zidane.

Baadaye, majeraha yalimtibulia Nedved kabla ya kutokea kwa ishu ya kupanga matokeo ya Calciopoli, iliyofanya Juventus kushushwa daraja, lakini Nedved alibaki na timu hiyo hadi iliporejea kwenye Serie A na alifunga mabao 11 katika msimu ambao ilirejea kwenye Serie A.

Alistaafu soka 2009, lakini aliibuka tena kutoka kwenye kustaafu mwaka 2018 na kucheza mechi moja sambamba na mwanaye FK Skalna.

Nedved alikuwa kwenye bodi ya wakurugenzi ya Juventus hadi mwaka 2022 wakati yeye na wakurugenzi wengine kwenye bodi walipokutwa na kashfa nyingine na hivyo kufungiwa kujihusisha na soka huko Italia kwa miezi minane.