Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Azam ni kweli wako siriazi na Ibenge?

NONDO Pict

SOKA letu limepiga hatua. Kuna mambo mengi yanayobadilika kwa kasi ambayo yanaashiria moja kwa moja tumeanza kuingia kwenye anga nyingine.


Ni mambo hayo ambayo yanatutofautisha kabisa na majirani zetu. Sasa hivi kwa Tanzania kuingiza timu nne kwenye mashindano ya kimataifa imekuwa ni kitu cha kawaida. Hata ukimuuliza shabiki wa mtaani kabisa ambaye hajui mpira anaona ni kitu cha kawaida, lakini siyo jambo jepesi, kuna kitu kimefanyika mahali kwa muda mrefu.


Achana na sifa ya ligi yetu kuwa kwenye nafasi za juu, hata klabu zetu na zenyewe sasa zimeanza kushindana na wakubwa kwenye renki za ubora wa Afrika. Hayo ni mafanikio ya kujivunia.

Makocha wakubwa, wachezaji wakubwa wanaiangalia ligi yetu. Leo hii  gharama za timu kuwa bingwa zimeongezeka kuanzia aina ya kikosi ulichonacho mpaka benchi la ufundi.

Ndiyo maana utaona kwa sasa hata wachezaji wanaokuja kutoka nje ni wale ambao bado wanaf-ikiria miaka mingi mbele juu ya vipaji vyao. Tanzania imegeuka daraja la wao kwenda mbele kusaka utajiri na siyo sehemu ya kustaafia. Walimu wakubwa wenye sifa wanaitamani Tanzania sasa. Tunapozu-ngumza hapa, Mkong-omani Florent Ibenge tayari yupo Tanzania.

IBE 01

Anafu-ndisha mpira Mbagala. Fungu la Azam timu yenye utajiri mkubwa zaidi wa rasilimali nchini imempa kazi ya kuhakikisha anawavusha kutimiza malengo yao hasa katika Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

Ni kocha ambae wasifu wake unatosha kushawishi watu wengine kutaka kuijua ligi yetu. Hakuna kitu ambacho hajafanya kimataifa. Tena akiwa na timu kubwa.

Ligi yetu imetawaliwa na timu mbili za Kariakoo kwa maana ya Simba na Yanga, lakini ujio wa Azam unaon-ekana kuwapa matu-maini wengi kama timu itakayo-utoa mpira wetu kwenye makucha ya miamba hiyo miwili.

Siyo kazi rahisi ya kutamka tu mdomoni lakini lazima ianze sehemu kutokana na mizizi iliyowekwa na miamba hiyo ya Kariakoo. Azam hawako mbali sana kwani kwa miaka kadhaa wameweza kukaa katikati yao na kilichobaki ni kukaa juu yao kwa kuwatumia watu wenye maono mak-ubwa kama Ibenge.

IBE 02

Nikiia-ngalia Azam nawaona Mamelodi wa Afrika Kusini ambao wao wameweza kukaa juu ya timu pendwa nchini humo Orlando Pirates na Kaizer Chiefs. Pale Misri kuna Pyramid ambao nao bado wako kwenye mchakato ambao Azam wanapitia ila kuna somo wametoa kwa Azam. Wamebeba ubingwa wa Afrika msimu uliopita.

Ujio wa Ibenge naona ni athari za yale wanayofanya Pyramid na Mamelodi kufikia hapa walipo. Kwangu mimi ujio wa Ibenge ambaye alikuwa akitamaniwa na Simba na Yanga kwa miaka mingi, nautazama kama hatua moja kwa Azam kujijengea heshima AfriKa na ndani pia kwani itawasaidia kujitangaza. Kujitangaza kivipi? Ibenge hajawahi kufeli.

IBE 03

Ni Kocha ambaye mpaka akubali kuingia sehemu lazima pawe na mradi unaoe-leweka. Anapenda mataji. Anapenda kushinda. Anapenda furaha. Lakini hata uwepo wake tu Tanzania tena Azam utawafanya wengi kutaka kujua na kumfuatilia zaidi sambamba na klabu yake mpya ambayo haina shida ya matumini kununua wachezaji wakubwa.

Uwepo wake na heshima aliyonayo na uzoefu inaweza kuinufaisha Azam kupewa huduma za VIP wanapokuwa uwanjani, namaanisha watachezeshwa kama timu ya daraja A kitu ambacho ni sehemu ya vikwazo vinavyowakabili kuanzia ligi ya ndani hadi michuano ya kimataifa. Tahadhari itakuwa kubwa maradufu ya misimu iliyopita.

Faida nyingine ni ushawishi kwa wachezaji ambao watavutiwa kuja kujiunga na Azam sababu yake kutokana na mahusiano yake na hao wachezaji na hata waliopo ni rahisi kwake kuwasimamia sababu wanamjua na wanamheshimu na watakuwa tayari kupokea maelekezo kwani wanajua mwalimu ameshafanikiwa kupitia hicho anachowaeleza. Ana kumbukumbu nyingi za kuwahamasisha kupitia wachezaji aliowahi kuwafundisha ambao sio wageni hapa kwetu natarajia kuiona Azam ya tofauti kiushindani ndani na nje ya uwanja.

IBE 04

Ibenge ni mtu anayependa mapambano makali ndani ya dakika 90. Kumbuka timu kubwa ulizowahi kumuona nazo hapa nchini alipokuja kwenye majukumu ya kimataifa. Si mtu wa kufeli kirahisi.

Anashusha watu wa kazi kwelikweli. Na hanaga mechi ndogo. Kuna kitu kimoja bado nina wasiwasi nacho. Je, Azam kweli wako siriazi? Wanamaanisha kweli? Kuna wakati imekuwa ikielezwa kuna Ukariakoo wa mbali kwa baadhi ya Watendaji wake, jambo ambalo limekuwa likikwamisha maono ya uongozi. Ndiyo maana nauliza ni kweli Azam wako siriazi sasa?

Kama wale wote wanaohusika na Azam wataweka masilahi ya timu mbele kuliko yao binafsi kuanzia kwenye usajili na namna timu inayaendea malengo yake makubwa bila kutoboa mtumbwi kwa masilahi yao na furaha za Ukariakoo basi huenda Ibenge akatushangaza. Tukutane msimu wa 2025/2026. Kuna kitu tutajifunza.