Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UCHAMBUZI: Liverpool mwanadamu mmoja mwenye maradhi mengi

JINSI maisha yanavyokwenda kasi. Liverpool hii mpya ilitamba kabla ya Corona, ikachukua ubingwa wake wa kwanza wa England baada ya miaka 30 wakati wa Corona, huku uwanja wao wa Anfield ukiwa mtupu na kikosi kimesambaratika hata kabla ya Corona haijatoweka.

Nilikuwa nikiitazama sura ya mtu anayeitwa Jurgen Klopp akimtazama ‘Mwanadamu’ wake jinsi alivyokuwa na magonjwa mengi. Liverpool. Ana magonjwa mengi ambayo mengine yanatibika na mengine hayatibiki.

Hauwezi kuamini lakini Liverpool ya sasa haina hata uhakika wa kutinga Top Four. wanashika nafasi ya nne na mgongoni kwao kuna West Ham yenye pointi 38 huku Liverpool wakiwa na pointi. Everton na Chelsea hawapo mbali pia. Wana pointi 36.

City wapo mbele yao wakiwa na fomu nzuri huku pengo likiwa ni pointi saba na wana mechi mkononi. Wanafanya wanachokifanya huku Kelvin de Bruyne akiwa ameuamia, Kun Aguero akiwa nje kwa muda mrefu pia.

Liverpool wanaumwa nini? Wana magonjwa mengi kwa wakati mmoja. Tuanze na ugonjwa huu hapa unaoitwa Second Season syndrome. Wazungu wanauitwa huu ugonjwa hivi. Sisi waswahili huwa tunasema ni ugonjwa wa uchovu katika msimu wa pili.

Mwanadamu anakuwa ametumia nguvu nyingi kupata akitakacho katika msimu wa kwanza lakini akipata anajikuta hoi na anachoka sana. Liverpool haikuwa na msimu mmoja wa kukimbiza. Imekimbiza kwa misimu minne mfululizo.

Staili yao ya mchezo inashangaza wengi. Sio tu kwamba ni wazuri wakiwa na mpira, lakini pia wasipokuwa na mpira. Wanakupa mbinyo wa kukulazimisha uwaachie mpira wao. Muda wote mpira wanakuwa nao wao tu. Walipokosa ubingwa kwa tofauti ya pointi moja kwa City misimu miwili iliyopita, Liverpool walirudi tena kwa kasi ile ile kwa ajili ya kumaliza kazi. Corona haikuwazuia kurudi vema na kumaliza kazi yao. Ubingwa wa kwanza wa Ligi ya England baada ya miaka 30!.

Sasa wanaonekana wamechoka. Uchovu unaonekana umewapata. Najua unataka niongelee majeraha ya wachezaji lakini subiri kwanza. Sadio Mane sio yule. Mohamed Salah sio yule. Roberto Firmino anachekesha tu.

Nilikuwa nikimtazama mchezaji wa Brighton anayeitwa Yves Bissouma Jumatano usiku. Baadaye nikawa namtazama Solly March. Wote na walikuwa wakiupata mpira waliweza kutembea kwa hatua nne hadi tano bila ya kukabwa. Wangefanya maamuzi sahihi. Liverpool ya miezi 12 iliyopita haikuwa vile.

Hili suala la matumizi makubwa ya nguvu ya kitu fulani kisha msimu unaofuata unachoka pia unawapata hata wale ambao wanakaribia kushuka daraja. Watazame Sheffield United.

Msimu uliopita walikaza sana kuhakikisha hawashuki. Wakatumia nguvu nyingi. Msimu huu wamekuja wakiwa wamechoka.

Baada ya hapo Liverpool wana ugonjwa mwingine unaojulikana zaidi. majeraha. Walinzi wake wa kati wameumia. Ameumia mlinzi bora zaidi wa kati duniani kwa sasa, Virgil van Dijk. Hili ni pengo kubwa. Pia wameumia Joel Matip na Joe Gomez.

Manchester United isingeweza kwenda sawa kama angeumia Nemanja Vidic nyakati zile. Real Madrid haiwezi kwenda sawa akiumia Sergio Ramos. Hauwezi kukosa kuiweka hii kubwa sababu kubwa ingawa ukweli unabakia pale pale kule mbele nako washambuliaji sio tishio sana siku hizi.

Hapo hapo Liverpool wana ugonjwa mwingine. Kocha wao hakukichangamsha sana kikosi katika dirisha kubwa lililopita la majira ya majira ya joto. Alimnunua mchezaji mmoja tum kali, Diogo Jotta. Huyu ndiye aliyeanza msimu akiwa kinara wa mabao mwanzoni mwa msimu.

Watu tulikuwa tunajiuliza namna ambavyo Firmino angekuwa na maisha magumu baada ya ujio wa Jota. Lakini ghafla na Jota naye akaumia. Mpaka leo yupo nje. Yaani mchezaji yule yule aliyekuwa kinara wao mpya wa msimu naye akaumia.

Jota alikuja kujaribu kuvuruga utatu mtakatifu wa Mane, Salah na Firmino lakini ameumia na kiubinadamu wachezaji hawa watatu wamerudi katika uhakika wao ule ule wa kupata nafasi zao. waingereza wanasema Comfort Zone. Ukichanganya na uchovu wao basi Liverpool haiendi vyema kule mbele.

Sasa tumebakia tunatazama mbio za Liverpool msimu huu zitafikia wapi. siwaoni wakichukua ubingwa. Bahati nzuri ambayo wanayo mpaka sasa ni ukweli hata City wenyewe wameibuka hapa karibuni tu.

Kama City angekuwa na fomu tunayoifahamu tangu mwanzo wa msimu kuna uwezekano pengo kati ya City na Liverpool lingekuwa pointi 25 msimu huu.

Liver-pool ya msimu uliopita alianza kwa kushinda mechi saba za kwanza mfululizo. Ghafla akajikuta ana pointi 21. Watu walikuwa wanazungumzia Liverpool kwenda msimu mzima bila ya kufungwa na kuiga mwendo wa Arsenal ya Arsene Wenger ya mwaka 2004.

Lakini leo Liverpool wameingia Februari wakiwa wametosa sare saba na wamefungwa michezo minne.

Hii ina maana mpaka kufikia sasa Liverpool wamepoteza pointi 26 kwa urahisi tu. Hali yao sio nzuri.

Ule uwanja wao ambao ulikuwa mgumu kufungika umekuwa rahisi. Wamefungwa na timu ndogo tu. Burnley na Brighton.

Kesho wanacheza na Manchester City pale Anfield. Wanaweza kushinda au kufungwa lakini jambo hilo halitaamua msimu wao.

Wakifungwa wataipeleka City mbali sana lakini hata wakifungwa haimaanishi watakuwa wana nafasi kubwa ya kutetea msimu wao.

Hasa kwa kuzingatia kwa sasa wameanza kupoteza dhidi ya timu za kawaida. Hautaweza kutabiri watafanya nini katika mechi zijazo dhidi ya timu za kawaida.

Kitu kinachonisikitisha kwa Liverpool hii ni ukweli kwamba fomu yao ya miaka ya karibuni imedhulumiwa kwa kutwaa ubingwa mmoja tu. Liverpool walipaswa kutwaa mataji haya kwa misimu miwili mfululizo iliyopita. Hili la msimu uliopita lilipaswa kuwa la utetezi tu. Lile ambalo waliachwa pointi moja na City lilipaswa kuwa lao.

Imeandikwa na EDO KUMWEMBE