Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

UBISHI WA MZEE WA KALIUA: Ni kweli Yanga mbovu, lakini sio kwa Simba hii

NAOMBA ukae kwa kutulia! Yanga Baba Lao, GSM Baba Leo, kuna anayebisha huko? Kama yupo, nitumie jina lake kwenye namba yangu ya simu hapo juu.

Kariakoo Derby ndiyo mechi pekee duniani ambayo watabiri wameshindwa kuitabiri, ndiyo mechi pekee ambayo wachambuzi, wameshindwa kuichambua, haina fomula, haina historia, haina majina makubwa, ni mechi fulani hivi ya kiimani.

Ni mechi fulani ya kubakiza akiba ya manneo, kifupi, haina mwenyewe, baada ya vuta nikuvute ya muda mrefu, hatimaye mchezo wa watani wa Jadi nchini ulipigwa wiki iliyopita pale Uwanja wa Mkapa.

Haukuwa mchezo mzuri sana lakini Simba alifungwa kwa mara nyingine na GSM Boys (Yanga). Haukuwa mchezo wa kuvutia sana lakini, Mnyama alipoteza alama tatu, hakuna anayejua nini kiliwakumba Simba ndani ya dakika 90, lakini wote tunajua kwamba walifungwa.

Hakuna anayejua nani aliwafanya Yanga kuwa imara, lakini wote tunajua kama walifanikiwa kuwakoroga Simba hasa dakika 45 za kipindi cha kwanza. Simba wamekuwa Bora sana Kwa Mkapa dhidi ya vigogo wa Afrika lakini wamekuwa wakitolewa jasho sana na SGM Boys.

Al Ahly alifungwa kwa Mkapa, Kaizer Chiefs walifungwa Kwa Mkapa, hawa wote wamekwenda hatua ya Fainali michuano ya Afrika lakini, Yanga anatamba. Yanga amekuwa mbabe sana kwa Simba pale Mkapa Stadium.

Tangu GSM ameichukuwa Yanga, Simba amekuwa kibonde, Simba amekuwa mchekea, Simba amekuwa hana meno tena. Yanga anajipigia tu kila siku, anajipigia tu kila dakika, kuna mchambuzi yoyote huko anajua sababu? Tafadhali naomba uniandikie ujumbe mfupi kupitia namba yangu ya simu hapo juu.

Wiki iliyopita ulichezwa mchezo wa sita wa Watani wa Jadi huku Yanga ikiwa chini ya tajiri, Ghalib Said Mohammed. Yanga amefungwa mchezo mmoja tu, mechi ya nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam mabao 4-1.

Simba hajawahi kushinda mchezo wowote wa Ligi Kuu, ushindi kwake umebaki kuwa sare tu, Yanga ameshinda mechi tatu dhidi ya Simba, sare mbili na kupoteza mechi moja kwenye mechi zote sita walizocheza timu ikiwa chini ya GSM.

Ghalib Said Mohammed Baba Lao. GSM kiboko yao. Nini kinawasumbua Simba wanapokutana na Yanga ya GSM? Sina majibu, naomba msaada wako, naomba maoni yako. Tafadhali kama ndugu yangu unajua chochote kinachoitesa Simba inapokutana na GSM Boys, nijuze kupitia namba yangu ya simu hapo juu kwa ujumbe mfupi.

Nimetazama wachezaji wa Simba waliocheza mechi ya watani, wengi walikuwa ni wachezaji wa kigeni, nimetazama wachezaji wa Yanga waliocheza dhidi ya Simba, asilimia kubwa walikuwa ni wazawa, unadhani hii inaweza kuwa imechangia matoa haya ya hivi karibuni? Sina uhakika.

Wapo wanaoamini kuwa wachezaji wazawa wanajua zaidi utamaduni wa derby kuliko wageni, wapo wanaoamini kuwa uzalendo wa wachezaji wa kigeni ni mkubwa kwenye derby kuliko wageni. Hili nalo sina uhakika. Kitu kimoja tu ambacho nakijua, Simba amefungwa tena. Simba kapasuka kwa mara nyingine dhidi ya GSM Boys.

Derby ya Kariakoo kiboko! Kuna utofauti mkubwa sana wa ubora kati ya Simba na timu nyingine yoyote ya Tanzania lakini, Simba anapigika kilaini sana mbele ya Yanga ya GSM. Kuna watu wanaamini mabadiliko ya Kocha, Didier Da Rosa kumtoa Clatus Chama alichemka, wapo wanaoamini kuwa Chama bado alistahili kubaki dimbani. Unadhani hii ndiyo ilikuwa sababu ya Simba kufungwa? Sidhani, sina uhakika. Kitu pekee ambacho nina uhakika nacho ni kuwa Simba imefungwa, imeteseka sana huko nyuma na Yanga ya GSM, naona imeteseka tena wiki iliyopita.

Yanga wazuri mara nyingi wamekuwa wakifungwa na Simba ya kawaida, Simba wazuri mara nyingi wamekuwa wakifungwa na Yanga ya kawaida. Bado huwa sijui sababu ni nini, kama unajua muendelezo wa matokeo haya, tafadhali naomba uniandikie ujumbe mfupi wa maandishi kupitia namba yangu ya simu hapo juu. Kuna watu wanaamini Simba walitakiwa kupewa mkwaju wa penati na Mwamuzi wa mchezo lakini haikuwa hivyo, unadhani hiyo inaweza kuwa sababu ya msingi ya Simba kufungwa na Yanga? Sina uhakika, sidhani. Kitu pekee nilichokiona wikendi iliyopita ni Simba kufungwa.

Mbabe wa Al Ahly kwa Mkapa, mbabe wa Kaizer Chiefs Kwa Mkapa, ni kibonde wa Yanga kwa Mkapa, ni kibonde wa GSM Boys. Huu ni muda wa kuiheshimu sana Kariakoo Derby, ni Derby isiyotabirika, ni derby isiyochambulika, inajiendesha yenyewe.

Nafahamu Yanga iko nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, nafahamu Yanga iko kwenye hatua ya Fainali kwenye michuano ya ASFC lakini, haiondoi ukweli kuwa bado hawajawa na timu ya uhakika. Bado Yanga inasuasua, inahitaji kama wachezaji watano wapya wa kikosi cha kwanza, inahitaji wanaume wengine wapya wakuongeza nguvu, lakini, ni timu hii hii ya GSM ambayo Mnyama amekuwa hafurukuti.

Kuna watu wanaamini kuwa John Bocco alistahili kadi nyekundu kwenye mechi ile, unadhani Mnyama ndiyo angepotea mazima? Sina uhakika, siamini. Kitu pekee ambacho nakifahamu ni kuwa Simba alifungwa Kwa Mkapa, pamoja na kuwa Yanga imekuwa kama homa za vipindi msimu wanne sasa lakini, sio wanyonge sana linapokuja suala la Kariakoo Derby, wako imara sana dhidi ya Mnyama. Hongereni sana viongozi wa Yanga walau kwa kupata chakuwapozea mashabiki wenu, nendeni sasa msimu ujao mkatengeneze timu ili msimu ujao, mpunguze lawama kwa Waamuzi na Shirikisho la Soka nchini (TFF), mambo ya kubahatisha hayadumu sana. Mambo ya kutegemea muujiza kila siku sio ya kuamini sana, kama kuna mtu anajua sababu ya Simba kufungwa wikiendi iliyopita, tafadhali nijulishe kwa ujumbe mfupi kupitia namba yangu ya simu hapo juu.


IMEANDIKWA NA OSCAR OSCAR