Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Timu kiboko kwa kuchelewesha muda England

ENGLAND Pict

Muktasari:

  • Bila shaka inakukera. Ni kitu kinachokera wengi na ndio maana hata makipa kwa sasa wameanza kuhesabiwa sekunde pindi wanapodaka mipira ili kuhakikisha muda wote mpira unakuwa mchezoni.

LONDON, ENGLAND: UNAKUWA kwenye hali gani, timu yako inahitaji bao na mpinzani unayekabiliana naye, wachezaji wake wanapoteza tu muda uwanjani, kwa kujiangusha au kuchelewa kurusha mpira au kupiga golikiki.

Bila shaka inakukera. Ni kitu kinachokera wengi na ndio maana hata makipa kwa sasa wameanza kuhesabiwa sekunde pindi wanapodaka mipira ili kuhakikisha muda wote mpira unakuwa mchezoni.

Ni kawaida kwa timu ndogo inapocheza dhidi ya timu kubwa, inapoteza muda kwa sababu maalumu na hivyo pia imekuwa ikitumika pindi timu kubwa zinapokutana na moja imepata matokeo inayotaka, hivyo kupoteza muda ni kawaida.

Kwa mujibu wa Opta, kwenye Ligi Kuu England kuna timu ni mahiri kwa kupoteza muda ndani ya uwanja kuliko nyingine.

Kuanzia kwa vinara Liverpool na Manchester City hadi kwa timu zote zikiwamo zilizopo katikati ya msimamo wa Ligi Kuu England, Fulham na Brighton huu hapa ni muda uliopotezwa kwa kila timu kwa maana ya kuangalia mapigo ya frii-kiki na kurusha mipira.

ENG 05

Namba 20-17

Licha ya kutokuwa na wachezaji matata kabisa uwanjani kama Matheus Cunha, Wolves ni timu ambayo ilihakikisha mpira unakuwa mchezoni wakati wote na kupoteza muda kidogo sana, ambapo timu hiyo ina wastani wa kupoteza muda wa mchezo kwa sekunde 24.1. Manchester City, inayopambana kurejesha hadhi yake ya kuwa bingwa wa England, yenyewe ina wastani wa kupoteza muda sekunde 25.6.

Inafuatia Nottingham Forest, inayomilikiwa na Ange Postecoglou na Liverpool ya kocha Arne Slot. Forest ina wastani wa sekunde 26.4 ya muda iliyopoteza ndani ya mchezo kwenye Ligi Kuu England, wakati Liverpool inayosaka taji lake la tatu la Ligi Kuu England msimu huu, yenyewe ina wastani wa kupoteza muda, sekunde 26.8.

20. Wolves – sekunde 24.1

19. Man City – sekunde 25.6

18. Nottingham Forest – sekunde 26.4

17. Liverpool – sekunde 26.8


ENG 04

Namba 16-13

Kocha David Moyes ameifanya Everton kuwa moja ya timu tishio kwenye Ligi Kuu England na kuchuana kuwania nafasi za kucheza michuano ya Ulaya. Usajili wa kiungo mshambuliaji, Jack Grealish na Kiernan Dewsbury-Hall umeifanya timu hiyo kucheza soka la kibabe na ndio maana haitaki sana kupoteza muda wa mchezo, ikiwa na wastani wa sekunde 27.1. Fulham naye imekuwa na rekodi sawa kama za Everton, kutokana na miamba hiyo ya Craven Cottage kuhitaji mpira uchezwe muda wote, ambapo katika mechi saba ilizocheza kwenye ligi, imeweka wastani wa kupoteza muda kwa sekunde 27.4, ikiwa ni sekunde 0.5 tu zaidi ya wastani wa muda ambao Bournemouth ilipoteza ndani ya uwanja.

16. Everton – sekunde 27.1

15. Fulham – sekunde 27.1

14. West Ham – sekunde 27.4

13. Bournemouth – sekunde 27.6


ENG 03

Namba 12-9

Mabingwa watetezi wa Europa League, Tottenham Hotspur wanaamini watakuwa na msimu mzuri kwenye michuano ya ligi ya ndani tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita, hasa baada ya sasa kuwa chini ya kocha mpya, Thomas Frank. Kwenye Ligi Kuu England, Spurs imekuwa na mbinu pia za kupoteza muda mchezoni, ikiwa na wastani wa sekunde 27.7. Brighton nayo, imekuwa ikiripotiwa kuwa na ujuzi wa kutumia mbinu hiyo ya kupoteza muda, ambapo ina wastani sekunde 28.6 huku Leeds United, yenyewe ina wastani wa sekunde 29.3 kwenye kupoteza muda. Kikosi cha kocha Unai Emery, Aston Villa pia kimekuwa kwenye utaratibu wa kupoteza muda mchezoni, kikiwa na wastani wa kupoteza muda kwa sekunde 29.4 katika mechi ya Ligi Kuu England hadi sasa.

12. Tottenham – Hotspur sekunde 27.7

11. Brighton – sekunde 28.6

10. Leeds United – sekunde 29.3

9. Aston Villa – sekunde 29.4


ENG 02

Namba 8-5

Chelsea na Newcastle United, zinazonolewa na makocha Enzo Maresca na Eddie Howe, mtawalia ni timu zilizopambana vikali kuwania nafasi nne za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England msimu uliopita, bila shaka zitachuana tena msimu huu. Chelsea ilianza mzimu vizuri kuliko Newcastle, lakini kuna vitu vichache sana vinavyozitofautisha timu hizo mbili kwa msimu huu wa 2025/26. Chelsea imekuwa na wastani wa sekunde 29.5 wa muda iliyopoteza mchezoni kwenye mechi zake za Ligi Kuu England, ikiwa ni sekunde 0.2 pungufu ya muda ambao, Newcastle imepoteza kwenye mechi zake. Crystal Palace, mabingwa watetezi wa Kombe la FA, wamekuwa na wakati mzuri chini ya kocha Oliver Glasner. Miamba hiyo ya Selhurst Park ina wastani wa kupoteza muda kwa sekunde 30.6 ndani ya uwanja msimu huu, huku Manchester United, yenyewe inayopambana kuboresha mambo na kuwa tofauti kwenye Ligi Kuu England msimu huu, ina wastani wa sekunde 31 wa muda iliyopoteza ndani ya uwanja kwa kusimamisha mchezo usiendelee ama kwa kupiga golikiki au kurusha mipira iliyotoka nje.

8. Chelsea – sekunde 29.5

7. Newcastle United – sekunde 29.7

6. Crystal Palace – sekunde 30.6

5. Man United – sekunde 31


ENG 01

Namba 4-1

Kwenye orodha ya timu zilizopoteza muda mwingi mchezoni kwenye Ligi Kuu England msimu huu, ipo miamba ya Emirates, inayonolewa na Mhispaniola, Mikel Arteta, Arsenal. Timu hiyo iliyoishia kushika nafasi ya pili kwenye ligi kwa misimu mitatu mfululizo ni kati ya timu zinazofukuzia ubingwa kwenye ligi hiyo, lakini yenyewe ina wastani wa kupoteza muda mchezoni kwa sekunde 31.

Vijana waliopanda daraja msimu huu, Sunderland yenyewe pia imekuwa hodari kwa kupoteza muda kwenye Ligi Kuu England msimu huu, ikiwa na wastani wa sekunde 32.3. Kwenye muda kama huo, wapo vijana wa Scott Parker, Burnley, ambao wana wastani wa sekunde 32.7 kwa muda ambao imepoteza kwenye Ligi Kuu England msimu huu kwa kufanya mchezo usimame.

Kwa timu zote za Ligi Kuu England msimu huu, Brentford ndiyo vinara wa kupoteza muda mwingi mchezoni, ambapo timu hiyo ina wastani wa kupoteza sekunde 33.5, ambazo zilifanya mchezo kusimama na kuwakosesha mashabiki uhondo kwa maana ya kuchelewesha kupiga golikiki au kurusha mpira.

4. Arsenal – sekunde 31

3. Sunderland – sekunde 32.3

2. Burnley – sekunde 32.7

1. Brentford – sekunde 33.5