Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Tahadhali ukimbiaji pembezoni mwa barabara

DOKTA Pict

Muktasari:

  • Ukimbiaji huo ni mdogo mdogo hujulikana kama jogging, huainishwa kitabibu kama aerobic exercise kwa mwenye uhitaji wa kuboresha afya ya mwili.

UFANYAJI mazoezi mepesi ya kukimbia katika barabara za huduma au pembezoni ni maeneo ambayo watu hupenda kuyatumia kufanya mazoezi  ya ukimbiaji mwepesi.

Ukimbiaji huo ni mdogo mdogo hujulikana kama jogging, huainishwa kitabibu kama aerobic exercise kwa mwenye uhitaji wa kuboresha afya ya mwili.

Ukimbiaji huo umekuwa zaidi ukifanywa na watu ambao pengine wanabanwa na majukumu ya kazi au wanaishi maeneo ya mbali huku wakiwa kazini.

Vilevile wakimbiaji  wanapotoka jioni kazini au asubuhi jirani na maeneo  ya kazi hukumbia ili baadaye waingie kazini.

Ukimbiaji wa pembezoni mwa barabara hupendwa zaidi na watu wa aina hiyo wenye umri mkubwa. Mara nyingine hufanya hivyo kwa vikundi vidogo ili kupata hamasa na ari ya ukimbiaji.

Kutokana na upigaji hatua za maendeleo katika nchi yetu vivyo hivyo kuendana na kuongeza kwa visa vya magonjwa yasiyoambukiza (NCD) inashauriwa kufanya mazoezi.

DOKT 01

Magonjwa yanatokana na mienendo na mitindo mibaya ya maisha ikiwamo kutoushughulisha mwili kwa mazoezi na ulaji holela wa vyakula hatimaye jamii hukumbwa na unene.

Mwamko wa ukimbiaji unatokana na ukweli kuwa jamii imeanza kutambua zoezi la kukimbia kidogo kidogo ni nyenzo muhimu ya kukabiliana na unene.

Tafiti zinathibitisha zoezi linalochangia watu kuwa na utimamu bora wa afya ya mwili na kuishia muda mrefu ni la kukimbia kidogo kidogo kwani linawezesha mwili kuepukana na unene.

Unene huweza kuwa mkubwa na kuwa unene uliokithiri hivyo humweka mtu katika hatari zaidi ya kupata magonjwa yasiyoambukiza ikiwamo kisukari, shinikizo la juu la damu, magonjwa ya mishipa ya damu, kiharusi, ugonjwa sugu wa figo na saratani.

Kukimbia kidogo kidogo ni zoezi rahisi kufanywa na mtu mzima au kijana mwenye unene.  Lakini, kuna faida na hasara za kukimbia pembezoni mwa barabara hasa kutokana na baadhi ya miji katika nchi za uchumi wa kati na wa chini kutoweka maeneo rafiki ya kufanyia mazoezi hayo.

Baadhi ya wakimbiaji hujikuta wakikimbia pembezoni mwa barabara huku wakipishana na vyombo vya moto. Hali hiyo inasababisha baadhi kugonjwa na kufa au kupata majeraha.

Lakini, pia ipo baadhi ya miji ambayo ina uchafuzi mkubwa wa hali ya hewa ikiwamo kutoa moshi mwingi kutoka katika vyombo vya moto au vumbi kutokana na magari.

Ingawa Tanzania hatujifikia viwango vya juu vya uchafuzi wa hali ya hewa kupitia moshi wa magari au viwanda, hivyo bado haijawa tishio kwa wakimbiaji wa pembezoni mwa barabara za huduma.

DOKT 02

Kukimbia kwenye barabara ya huduma hubeba hatari kadhaa zinazohusiana na vyombo vya moto na ubora wa hewa anayovuta mkimbiaji. Yafuatayo yanaainisha matatizo yanayoweza kujitokeza.


1. HEWA CHAFU, VUMBI

Magari yanayopita kwenye barabara za huduma yanaweza kusababisha hatari ikiwamo vumbi na kutoa takasumu zilizopo katika moshi unaoweza kuathiri afya ya upumuaji.


2. MAJERAHA

Nyuso ngumu na mashimo ya barabara za pembezoni zinaweza kuongeza hatari ya majeraha ya pamoja katika misuli na mifupa kwenye nyayo, visigino na vifundo vya magoti


3. HATARI BARABARANI

Kuongezeka kwa hatari ya ajali. Barabara za huduma, hasa zile zilizo na uwezo mdogo wa kuona mbali au sehemu nyingi za kufikia zinaweza kuwa hatari kwa wakimbiaji kutokana na uwezekano wa kugongana na vyombo vya moto.

Madereva wasio waungwana na madereva kwenye barabara za huduma wanaweza kutatizwa kwa kuingia au kutoka njia kuu na kupita ile ya watembea kwa mguu na wakimbiaji pasipo kujua.

DOKT 03

Ukosefu wa miundombinu ya watembea kwa miguu, barabara za huduma mara nyingi hukosa njia ndogo au  maeneo maalumu ya watembea kwa miguu na hivyo kulazimisha wakimbiaji kushiriki katika njia zilizo karibu na vyombo vya moto, na hivyo kuongeza hatari ya ajali. 


4. UBORA WA HEWA

Vyombo vya moto huchoma mafuta na kuzalisha hewa chafu ya hydrocarbon. Kukimbia karibu na barabara huhatarisha wanaokimbia kuvuta hewa chafu - uchafuzi wa hewa ikiwamo naitrojenidioksidi, benzini na vichafuzi vingine vinavyoweza kukera mfumo wa upumuaji na kuchangia matatizo ya moyo na mishipa. 


5. HATARI MUDA WA kUKIMBIA

Wakimbiaji hupenda nyakati za jioni au asubuhi. Mida hii kwa miji mikubwa kama Dar huwa na msongamano mkubwa wa vyombo vya moto. Hii inawaweka kuwa katika hatari ya ajali au kuvuta hewa chafu.


6. MAMBO MENGINE

Maeneo mengine ya pembezoni mwa barabara huwa na miundombinu isiyo rafiki, hivyo inaweza kuongeza athari kwenye viungo ambayo inaweza kusababisha majeraha.

Nafasi ndogo barabara za huduma inaweza kutoa eneo ndogo la kukimbia, na hivyo kufanya iwe vigumu kuzunguka vizuizi au kukwepa watembea kwa miguu wengine.

Muonekano wa pembezoni wakati wa kukimbia katika hali ya mwanga wa chini mapema asubuhi au jioni kwenye barabara ya huduma inaweza kuwa hatari katika macho.

DOKT 04

Pia mwanga mkali au hafifu unaweza kumsababishia mkimbiaji kutoona vizuri na hatimaye kuweza kupata ajali.


Fanya yafuatayo kuboresha ukimbiaji wa pembezoni mwa barabara


1. Njia mbadala salama zaidi

Wakati wowote inapowezekana chagua kukimbia kwenye bustani, njia zilizotengwa kwa ajili ya watembea wa mguu au kwenye vinjia vya kando eneo la mbali na msongamano wa vyombo vya moto.


2. Kimbia kupishana na vyombo vya moto

Kama ni lazima ukimbie barabarani, kimbia dhidi ya msongamano wa magari ili uweze kuona magari yanayokuja mbele yako. 


3. Mavazi yanayoakisi

Vaa nguo zinazong’ara na uzingatie kutumia vifaa vya kuangazia wenye vyombo vya moto, hasa wakati wa hali ya mwanga wa chini kama vile asubuhi au jioni jioni. 


4. umakini na spika za sikio, miwani

Epuka kukimbia huku umeweka spika za masikioni kusikiliza muziki kwa sauti kubwa na vaa miwani yenye kuwezesha kuona. Vifaa hivyo vinaweza kuathiri ukimbiaji wako na mazingira uliyopo katika kuona na kusikia.


5. Chagua nyakati rafiki

Epuka kukimbia wakati wa kilele cha saa za msongamano wa vyombo vya moto au wakati mwonekano wa mazingira ni mbaya. Izingatiwe kwa wabunifu wa barabara wanapaswa kubuni barabara za huduma za pembezoni ambazo zitamlinda mkimbiaji.

Ni muhimu sheria za barabarani zikasimamiwa ipasavyo hasa kwa waendesha bodaboda na magari kutozitumia vibaya njia za pembezoni na kuwaathiri wakimbiaji. Ujenzi wa miji mipya uzingatie barabara zenye nafasi kubwa kulingana na miongozo ya kimataifa ya ujenzi mijini.