Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SPOTI DOKTA: Simba, Liverpool na tatizo la hasira

Muktasari:

  • Mara baada ya mchezo huo mashabiki wa Simba walijawa na hasira kali wakitoa maoni na kuukosoa uongozi pamoja na wachezaji kadhaa wa timu hiyo.

KATIKA mechi za soka Jumamosi iliyopita gumzo vijiweni ilikuwa ni kipigo cha mabao 2-0 ilichopokea Simba kutoka kwa Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Mara baada ya mchezo huo mashabiki wa Simba walijawa na hasira kali wakitoa maoni na kuukosoa uongozi pamoja na wachezaji kadhaa wa timu hiyo.

Hali ya hasira kwa mashabiki haikuishia hapo, bali iliendelea pia katika mitandao ya kijamii. Ukiacha Simba, kule England katika Ligi Kuu kwenye timu ya Liverpool kumeibuka maneno makali baada ya mshambuliaji Mohamed Salah kutoa maoni baada ya mchezo dhidi ya Leeds United.

Salah alinukuliwa alisema anahisi “ametupwa chini ya basi” baada ya kuachwa kwenye benchi kwa kutocheza michezo mitatu iliyopita ya Liverpool, jambo lililomfanya aachwe nje ya kikosi pia kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumanne dhidi ya Inter Milan juzi.

Maoni hayo yaliwaibua wachambuzi wa soka ambao ni wachezaji wastaafu wa klabu ya Liverpool ikiwamo Jamie Carragher ambaye alimkosoa vikali Mo Salah, akimtaka kutotoa maoni kama hayo kipindi hiki.

Malumbano haya yenye hasira kwa klabu ya Simba na Liverpool ni ishara kuwa klabu hizo, hasa mashabiki wake wamejawa na mzigo wa maudhi. Hali inayoashiria kushindwa kuvumilia kutokana na timu hizo kufanya vibaya mfululizo.

Salah anatarajiwa kuondoka kujiunga na timu yake ya Taifa ya Misri itakayoshiriki Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) Jumatatu ijayo, lakini mustakabali wake Anfield una shaka kubwa.

Hata katika mchezo wa UEFA wa juzi Jumanne hakupangwa katika mchezo huo walioshinda bao 1-0 dhidi ya Inter Milan. Hali ambayo inaashiria kuwa hakuna uhusiano mzuri na kocha wake.

Katika hali ya kibinadamu huwa ni kawaida kwa wachezaji au mashabiki kulipukwa na hasira aidha kutokana na timu kufanya vibaya kwa mfululuzo.


HASIRA IKO HIVI

Hasira ni moja ya matokeo yanayoashiria kuwapo kwa hisia za kawaida. Lakini pale inapozidi mwilini ni jambo la hatari kiafya pamoja na kiuhusiano na kijamii.

Hasira ya mwanadamu yaweza kuwa ya kawaida, ya kati na ile kali iliyokithiri. Hasira isipodhibitiwa inaweza kusababisha ugonjwa wa akili.

Chanzo cha hasira huweza kuwa ni matukio yanayomtokea katika maisha ya kila siku, yapo mambo ndani ya mwili kama vile kuwaza mawazo hasi na nje ya mwili kama vile kuudhiwa au kutishiwa.

Uwepo wa hasira ni mwitiko wa kimwili wa kuonyesha hisia hasi za kimwili huku kuwa na furaha huwa ni hisia chanya kimwili.

Hisia zetu za kimwili huwapo katika eneo la maalum katika ubongo, mwanadamu huweza kutumia hasira katika kujitunza na kujihami.

Hasira huendelea kuwapo na kumtawala endapo atakuwa anaendelea kutumia hasira hiyo kama kielelezo cha maudhi aliyoyapata.

Hasira humuathiri mtu uhusiano wake wa kijamii, hisia za kiakili na kimwili. Ndio maana kwa mchezaji kama Salah kuwekwa benchini ni jambo la kuudhi kwa upande wake.

Unapokuwa una hasira si wakati sahihi kutoa maoni, kwani kipindi hicho mwili unakuwa hauko sawa kiuamuzi, kwani umakini unakua upo chini. Vilevile hasira inaweza kukufanya kutoa uamuzi mbovu.


HASIRA INAVYOTOKEA

Mwilini mwetu ubongo ndio wenye kazi ya kuratibu shughuli zote za mwilini, kipo kituo maalumu ambacho kinahusika na hisia za kimwili.

Lakini sehemu katika ubongo hiyo iitwayo Amygdala ambayo imo ndani ya mfumo uitwao limbic ndio inahusika na hisia za mwili. Sehemu hii hutambua uwepo wa hatari nje ya mwili hivyo kuustua na kuupa mwili tahadhari kuwa kuna tishio.

Sehemu hii ndio ya kwanza kugutuka kabla ya sehemu ya pili itwayo cortex ambayo hutafakari na kuhukumu mambo kama ni kujibu mapigo au kutulia wakati wa hatari.

Sehemu hii ina sehemu ya upande wa kushoto yenye kazi ya kuzima sehemu inayohusika na hisia za mwili hivyo hasira hudhibitiwa, hii ni baada ya kutafakari na kunyumbulisha matukio yaliyojitokeza. Hasira kutokea hupita hatua mbalimbali ndani ya mwili na akilini kiujumla.

Hasira huwa inaambata na utiririshwaji wa kemikali za kimwili pamoja na vichochezi katika ubongo ambavyo husambaa sehemu mbalimbali mwilini. Vitu hivi kwa pamoja vinapotitirishwa huweza kuufanya mwili kuwa na nguvu kuliko ilivyo kawaida ili kujihami kwa lolote lile. Mtu anaweza kupambana, kukimbia au kupoteza fahamu wakati tukio hili linapotokea. Hii ni mbinu ya mwili kukabiliana na hali ngumu.

Na linaweza kuchukua dakika kadhaa kuwepo, baadae kama hasira itaendelea kuwepo basi mwili unaweza kutiririsha kiasi cha ziada cha kemikali na homoni za mfumo wa fahamu, na mwili kuweza kuanza kupambana.

Hatua hii huwa ni ya mwisho katika kuamsha hasira kali zaidi, hivyo hapa mtu anakuwa katika hatua za kupambana vikali.

Kemikali hizo na homoni zinapotiririka huambatana na mabadiliko ya kimwili na kiakili.

Mabadiliko huwa ni pamoja na mapigo ya moyo huanza kushika kasi ili kulisha misuli damu ya kutosha, mtu hupumua haraka haraka ili kuleta oksjeni nyingi zaidi, mboni za macho na lenzi hutanuka kuweza kuona zaidi, misuli huanza kujiweka imara na kuwa na nguvu sana.

Akili ya mtu mwenye hasira huwa makini zaidi kuliko kawaida na humlenga yule au kitu kilichomtisha na kumletea hasira. Ndio maana unaweza ukawa katika hatari kubwa ukaweza kujiokoa pasipo kutarajia na hapo baadaye ukajaribu kurudia kufanya hivyopasipo uwepo wa hatari ukashindwa.


MADHARA YA HASIRA

Uwepo wa hasira zisizodhibitiwa huwa na madhara kiafya kimwili na kiakili. Ndio maana klabu zina wataalam wa saikolojia ili kuwapa ushauri tiba wachezaji.

Madhara kama kuumwa kichwa, kukosa usingizi, kutokwa vipele, kukosa hamu ya kula, kuwa mwoga kupitiliza na kuumwa mwili.

Madhara mabaya zaidi ni kama vile kupata magonjwa ya moyo ikiwamo shambulizi la moyo, sonona na shinikizo la kiakili.

Habari nzuri ni kuwa tatizo la hasira linaweza kudhibitiwa kwa muathirika kufanyiwa ushauri nasaha na kupewa mbinu za kudhibiti na kupeperusha hasira iliyoganda mwilini hatimaye kumfanya awe huru kiafya.