Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SPOTI DOKTA: Diego Simeone kocha mtata kitabia

Muktasari:

  • Kocha huyu ni maarufu katika La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya, si tu kwa ubora wake wa kujenga timu imara kwa gharama ndogo bali pia kwa tabia zake tata ikiwamo hasira na kukwaruzana na waamuzi.

KATIKA Ligi Kuu ya Hispania, La Liga huwa ni vigumu kupita mechi kadhaa kwa kocha wa Atletico Madrid, Diego Simeone raia wa nchi ya Argentina bila kukosekana kwa kadi za njano au nyekundu au mikwazano ya hapa na pale na waamuzi.

Kocha huyu ni maarufu katika La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya, si tu kwa ubora wake wa kujenga timu imara kwa gharama ndogo bali pia kwa tabia zake tata ikiwamo hasira na kukwaruzana na waamuzi.

Kocha huyu aliyedumu kwa miaka 14 katika klabu hiyo. hukutana na mashinikizo mengi katika kazi yake, lakini licha ya utata wake. amekuwa mahiri kuijenga Atletico Madrid hivyo kumfanya apendwe klabuni hapo hata anapopata matokeo mabaya.

Moja ya vipengele muhimu vinavyopendwa kuwekwa na wasimamiaji mchakato wa kufanya usaili ili kuajiriwa ni kile kipengele kinachosema “Uwezo wa kufanya kazi chini ya shinikizo”.

Moja ya kazi ambayo kila siku ina shinikizo kubwa ni kufanya kazi ya ukocha hasa za klabu za kulipwa ambao wenzetu wanaita mameneja wa klabu.

Tazama tu makocha wa klabu za hapa nchini, Simba na Yanga ambapo ni kati ya klabu ambazo huwa ni kawaida makocha kuandamwa na mashinikizo ya mashabiki na viongozi.

Jaribu kuvaa viatu vya makocha uone jinsi wanavyopita katika nyakati ngumu. Jaribu kupata hali ya tishio la kufukuzwa kazi au kujadiliwa kuondoshwa katika nafasi yako.

Makocha wanakutana na tishio la kutumuliwa jambo ambalo kwa hali ya kibanadamu husababisha hisia hasi, hii ni hali inayoweza kumletea mtu tatizo la afya ya akili ikiwamo msongo wa mawazo.

Leo jicho la kitabibu linamtupia kocha mtata wa klabu ya Atletico Madrid ambaye ndani ya siku 5  klabu yake ilikutana na mchezo migumu miwili ambayo yote walipoteza huku wakiwa katika ubora wa hali ya juu.


Ndani ya siku 5 vipigo viwili vya maumivu

Katika Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya mahasimu wao Real Madrid wiki iliyopita siku ya Jumatano klabu hiyo ilipoteza mchezo wake kwa mikwaju ya penalti na kuondoshwa katika mashindano hayo.

Wakiwa bado wana machungu ya kutolewa UEFA wakarudi nyumbani katika ligi ya La Liga ambako siku ya Jumapili walikutana na klabu ya Barcelona ambayo ndio inaongoza ligi.

Walianza vizuri katika mchezo huo wakiongoza 2-0, lakini hapo baadaye mambo yalibadilika katika dakika za mwisho. Hii ilitokana na kufungwa mabao mawili dakika za mwisho hatimaye kupoteza 4-2.

Hili lilikuwa pigo la pili, ikizingatiwa kama wangelishinda wangeliweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa huo kwani kwa sasa hivi wako nafasi ya 3 nyuma ya Real Madrid.

Ukita-zama vyema michezo yote miwili unapata picha jinsi kazi ya ukocha inavyowaweka makocha katika shinikizo kubwa kimwili na kiakili.

Atletico Madrid katika mechi hizo zote walionekana kuwa bora na imara katika kila idara, ila bahati haikuwa yao walifungwa. Kila mpenda mpira aliona kuwa kuna kitu kizuri kimejengwa katika klabu hiyo kwa upande wa saikolojia.

Vipigo hivi viwili vimeumiza hisia za mashabiki na klabu hiyo kwa ujumla, lakini katu hutasikia kamdomo kama ilivyo kwa klabu nyingine kutaka kocha aachie ngazi.

Tofauti na ilivyokuwa kwa klabu ya Arsenal chini ya mzee Arsene Wenger akiboronga mashabiki walishinikiza afutwe kazi. Lakini kwa Atletico unaanzaje kumtaka Diego Simon aondoke katika klabu hiyo ambayo uimara wake na ubora wake unawakosha mashabiki.

Diego Simeone utata wake kitabia na faida zake iko hivi:

Kocha wao huwa anajulikana kuwa ni mtata ndani ya Ligi Kuu ya La Liga pamoja na UEFA huwa ni kawaida kulimwa kadi kutokana na tabia zake za kukwaruza na marefa wanaoboronga kiuamuzi.

Akivurugwa kocha huyu huwa harudi nyuma, lazima atalipuka kwa hasira na huku akifoka. Habari nzuri ni kuwa pamoja na hasira hizo huwa hapigi au kukunjana na mtu.

Vile vile timu ikipata ushindi hulipukwa kwa furaha kubwa kiasi kwamba saa nyingine hukimbia kuzunguka uwanja na kusereka kwa magoti.

Katika mchezo wa Jumatano UEFA aliwafokea wachezaji wake akiwataka kutosikitika na kutolewa kwao. Badala yake akawataka kushikamana wote kuwashukuru mashabiki.

Hii ilikuwa na jambo zuri kitabibu kwani inaboresha utulivu wa kiakili wa wachezaji ambao walikuwa wana jukumu jingine siku ya Jumapili.

Kocha huyu ambaye sasa amedumu klabuni hapo kwa miaka 14, amekuwa kinara sana wa kujenga timu hiyo na huku pia akiwa kama meneja huwaunganisha mashabiki na wachezaji.

Tabia yake ya kuwaamsha mashabiki na kuwaonyesha ishara kuwa shangilieni kwa nguvu inawapa sana hamasa na ari ya ushindi wachezaji wake.

Mashabiki ni moja ya msingi muhimu katika kuwajengea wachezaji saikolojia nzuri hatimaye kujisikia vizuri na kucheza kwa kujiamini, kuwa na uamuzi mzuri na kujisahihisha haraka wanapokesea.

Kocha huyu mtata huwa na tabia za wazi wazi pale unapomkorofisha huwa ni kawaida kulipuka kwa hasira bila kuogopa wala kujali kitakachotokea.

Katika mahojiano yake mara baada ya mchezo wao dhidi ya Madrid alisema usiku huo wao walikuwa bora, hakuwalaumu wachezaji wake ikiwamo waliokosa penalti.

Mtata Diego aliwananga wachezaji wa Madrid akiwataja kwa majina ikiwamo Kylian Mbappe, Vinicius Jr na Jude Bellingham hukuakionyesha ishara kuwa hawakuwa bora kuliko wachezaji wake.

Mtata huyu huwa hakai hata kidogo katika benchi, yeye huwa ni mwanzo mwisho anapambana kutoa maelekezo. Akitoka kwa wachezaji anahamia kwa mashabiki na kuwapa ishara washangilie.

Katika machapisho kadhaa ya sayansi ya tiba ya wanamichezo inaeleza kuwa meneja mzuri wa timu si tu pekee ana uwezo mkubwa kufundisha bali pia kujenga saikolojia nzuri ya upambanaji kwa timu.

Utulivu wa kisaikolojia kwa mashabiki na wachezaji kunaifanya timu kuwa na ustahimilivu mkubwa, ndio maana hata pale wanapopoteza mchezo huendelea kushikamana.

Atletico katika michezo yao migumu walionekana kutokukata tamaa, walikuwa wanajiamini kama vile wameshinda na huku pia wakionyesha juhudi kubwa hata pale walipoonekana kuchoka.

Tabia za kocha huyu zinaonekana kuwa na faida katika timu, siku zote anapambana kuhakikisha wachezaji wake wote wanakuwa sawa kisaikolojia hata pale wanapokuwa wamekosea.