Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

SI MCHEZO; Selena, Mondi na CR7 wanavyonufaika na ustaa

Muktasari:

  • Sio ajabu kuona msanii akipewa dili la fedha nyingi kwa lengo la kutangaza biashara, bidhaa, huduma au kuhamasisha kampezi fulani kupitia mitandao ya kijamii, ushawishi wa chapa ya msanii husika hasa mtandaoni ndio unaleta fursa hiyo.

UMAARUFU wa kazi zao unawafanya wasanii kutengeneza chapa zenye ushawishi mkubwa na hivyo kujikusanyia mamilioni ya wafuasi katika mitandao ya kijamii kitu ambacho ni fursa nyingine kwao kuingiza fedha nje ya sanaa yao.

Sio ajabu kuona msanii akipewa dili la fedha nyingi kwa lengo la kutangaza biashara, bidhaa, huduma au kuhamasisha kampezi fulani kupitia mitandao ya kijamii, ushawishi wa chapa ya msanii husika hasa mtandaoni ndio unaleta fursa hiyo.

Kwa mujibu wa Influencer Marketing Hub, Selena Gomez ndiye msanii duniani anayelipwa fedha nyingi kutangaza katika mtandao wa Instagram, Selena mwenye wafuasi zaidi milioni 424 anakadiriwa kulipwa Dola2.5 milioni,kwa tangazo moja.

Selena ambaye anafanya muziki na filamu amekuwa akitangaza bidhaa za urembo na mitindo, na kwa ujumla ni watatu katika ya watu wenye ushawishi (influncer) duniani wanaolipwa vizuri akiwa ametanguliwa na Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Hata hivyo, ukweli ni kwamba sio kila msanii maarufu mwenye idadi kuwa ya wafuasi kwenye mitandao ya kijamii ana nguvu ya ushawishi ya kumuwezesha kupata dili hizo kama wengi wanavyodhani.

Mkurugenzi wa Serengeti Bytes ambaye ni mtaalam wa masoko mtandaoni (digital marketing), Kennedy Mmari anasema msanii ni lazima aonyesha ushawishi kwa kile anachotangaza, njee umaarufu wake mtandaoni.

"Hapa kuwa na 'followers' ni kitu kimoja, lakini kuwa na ushawishi katika sekta fulani ndio kitu cha muhimu zaidi, sasa ili kupewa kazi lazima uwe na uwezo wa kushawishi lile soko ambalo linahitajika," alisema na kuongeza.

"Kama umepewa kazi ya ubalozi wa kampuni ya pombe lazima uonyeshe unaweza kuwashawishi wanywaji, kama hujajionyesha hivyo maana yake inakuwa ni ngumu" alisema Kennedy katika mahojiano na gazeti hili.

Lakini baadhi ya wasanii wamekuwa wakilalamika kuwa chapa kubwa zimekuwa zikitoa dili hizo kwa upandeleo, jambo hilo linapigwa vikali na Reuben Ndege (Ncha Kalih), mbobezi upande wa matangazo aliyewahi kufanya kazi na kampuni ya Scanad Tanzania. 

Amesema chapa fulani ikitaka kuzungumza (kuwauzia bidhaa au huduma) na watu wa aina fulani, itamtafuta mtu au msanii ambaye ana kitu fulani ambacho wale watu wanakitambua au wanakikubali.

"Kwa hiyo sasa hivi kama nina chapa ya mafuta ya kupikia, nitamchukua Shilole, na kweli ukimuweka kwenye tangazo mtu anakubali kwa sababu huyu dada anamuona kwenye mambo ya chakula," alisema Reuben akiongea na Times FM na kuongeza;

"Sisemi kwa ubaya, labda nimchukue Nandy nimuweke kwenye mafuta ya kula, ndio ni msanii mkubwa na maarufu lakini hatoshi kwenye hiyo chapa. Kwa hiyo mara nyingi wanaopata hizo dili wanaendana na hizo chapa, na wamejiweka katika hali inayowawezesha kufanya hiyo biashara," alisema.

Aliongeza kuwa chapa inapotoa fedha vilevile inatemea mrejesho mzuri wa kibiashara, "Unajua zamani hayo mambo yalikuwa yanatolewa kishkaji tu, lakini sasa hivi kuna uwajibikaji".

"Kama ni kampuni inayouza vinywaji, kinarudi nini?, aidha tunakaza chapa au tunapata fedha kwa bidhaa tunazouza, kwa hiyo kama nimekupa Sh400 milioni unatakiwa kuuza zaidi ya Sh400 milioni au kukuza chapa yangu kwa thamani ya fedha," alisema.

Wasanii wa Bongofleva, Rosa Ree na G Nako wamekuwa na maoni yanayoshabiana kuhusu hilo wakati wakiongea na gazeti hili, wote wamekiri ni fursa kwao ya kuingiza kipato nje ya muziki wao.

Rosa Ree ambaye amekuwa akitangaza bidhaa za pombe na nywele, amesema ni biashara nzuri ambayo inategemea zaidi msanii husika ameijenga vipi chapa yake mbele ya jamii na wanaohitaji kumtumia.

"Ni kitu kikubwa kwa sababu sanaa ni ajira, pale ambapo kampuni zinakufuata zinataka kufanya kazi na wewe ina maana sanaa yako ina ushawishi katika jamii. Kwa hiyo ni kitu kikubwa ambacho kimewapa mafanikio makubwa wasanii wengi na nina furahi na mimi ni miongoni mwa hao, nimepata dili nyingi," amesema.

"Kwa kifupi hiki kitu ni kikubwa kwa wasanii kwani imeweza kutengeneza mlango mwingine wa kuingiza kipato upande wetu. Shukrani kwa mashabiki wameniweka sehemu ambayo imenifungulia milango mingi," amesema Rosa Ree.

Rosa anasema kampuni yoyote inapomtazama msanii na kuona ana ushawishi na anaweza kuwaongezea kitu, ndipo wanamuita mezani na kumpa dili, hakuna msanii anayepewa dili kwa bahati mbaya, lazima uwe na kitu ambacho unakiweka mezani na yeye.

"Hivyo wasanii wote unaona wanafanya kazi na kampuni mbalimbali, ni kwamba wanaweza kushawishi jamii kuhusu bidhaa na huduma za kampuni husika, na pia wanaweza kuwaongezea kiasi kikubwa cha mauzo ndio maana wanatoa hizo dili," amesema.

Kwa upande wake G Nako kutoka kundi la Weusi ambaye anatangaza mavazi, huduma za mitandao ya simu, pombe n.k, amesema wasanii kupata dili hizo kwa wingi sasa ni ishara kuwa tasnia inazidi kukua.

"Ni kitu kingine ambacho inaonyesha tasnia inatanuka, kampuni nyingi zinawatumia wasanii kama 'influencer' na hiyo inaonyesha kwamba wasanii ni watu ambao wanaaminika na kuweza kuzishika hizo chapa na kwenda nazo sokoni," amesema.

Je, kampuni hizo zinapokuwa zinamfuata G Nako huhitaji nini hasa kutoka kwake na kwa kuzingatia nini?. Rapa huyo anasema cha muhimu na taswira (image) ambayo tayari msanii anakuwa ameitengeneza ambayo inaendana na bidhaa anayoenda kuitangaza.

"Ni namna msanii anavyokuwa ameijenga chapa yake, na chapa nyingine zinakuwa zinakuona, na kila chapa inakuwa anamuhitaji msanii kwa namna ambavyo anakuwa amejiweka mbele ya jamii," amesema na kuongeza. 

"Kwa mfano mimi nimewejiweka kama mtu ambaye napenda mavazi, kwa hiyo ni rahisi kumshawishi mtu ambaye anatengeneza chapa zake na mavazi kuniona. Au ni mtu ambaye anapenda kusafiri, ni rahisi kwa mtu ambaye anahusika na vitu vya safari kama Hoteli kuniona na kunipa dili," amesema G Nako.

Naye Mtaalamu wa Chapa na Mawasiliano, Docta Ukimwengu ambaye anasimamia chapa za wasanii kama Hamisa Mobetto, Idris Sultan, Jux n.k, amesema linapokuja suala la biashara kinachoangaliwa kwa msanii ni ushawishi kuendana na chapa ya mteja tu.

"Chapa inapotafuta balozi inaangalia mtu mwenye ushawishi kuendana na chapa yake na sio mtu anayefanya vizuri kwenye tasnia yake. Naweza kupenda muziki wako lakini sipendi unavyovaa, kwa hiyo hata ukitangaza bidhaa ya nguo sitoinunua kwa sababu sikuamini kwenye mavazi," amesema Docta Ulimwengu.

Ikumbukwe Diamond Platnumz aliwahi kudai kwa mwezi mmoja anapokea Sh200 milioni kwa kutangaza bidhaa na huduma mbalimbali, dili ambazo anazipata kutokana na ushawishi wake.

“Endorsement zangu kwa mwezi si chini ya Sh200 milioni, na tunasaini mikataba kila siku. Ninaingiza kwa wiki Sh55 milioni kwa siku, Sh7 milioni kwa saa moja, Sh300,000 na kwa sekunde Sh6,000,” alisema Diamond.

Ikumbukwe mcheza soka wa Ureno na klabu ya Al Nassr FC nchini Saudia Arabia, Cristiano Ronaldo ndiye mtu wenye ushawishi (influncer) zaidi duniani na anayelipwa fedha nyingi kwa kutangaza Instagram.

Ronaldo ambaye ni namba moja duniani kwa wafuasi Instagram akiwa nao zaidi ya milioni 6356, hulipwa Dola3.2 milioni, kwa tangazo moja katika mtandao huo ulioanzishwa Oktoba 2010 na hadi sasa ukiwa na watumiaji zaidi bilioni 2.4.