Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Si mchezo… Huku lazima ujipange vyema

MTIBWA Pict

Muktasari:

  • Mtibwa iliyoshuka daraja msimu wa 2023-2024 na kurejea msimu huu, imekumbana na kichapo hicho Septemba 21, 2025, ambacho kinaifanya inakuwa ni timu ya nne kupoteza pambano la kwanza la Ligi Kuu Bara baada ya kupanda tangu msimu wa 2021-2022.

BAADA ya kusota kwa siku 481 katika Ligi ya Championship, Mtibwa Sugar imeanza vibaya Ligi Kuu Bara msimu huu kufuatia kuchapwa bao 1-0 na Mashujaa katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Mtibwa iliyoshuka daraja msimu wa 2023-2024 na kurejea msimu huu, imekumbana na kichapo hicho Septemba 21, 2025, ambacho kinaifanya inakuwa ni timu ya nne kupoteza pambano la kwanza la Ligi Kuu Bara baada ya kupanda tangu msimu wa 2021-2022.

Rekodi zinaonyesha, tangu msimu wa 2021-2022 hadi sasa, ni timu tisa zilizopanda daraja kutoka Championship, ambapo kati ya hizo zilizoshinda ni nne sawa na zilizopoteza pia, huku moja tu ikitoka suluhu, kama Mwanaspoti linavyozielezea.

MTI 01

MSIMU WA 2021-2022

Msimu huo ulishuhudiwa Ihefu ambayo kwa sasa ni Singida Black Stars ikipanda Ligi Kuu Bara baada ya kuongoza kwa pointi 66, ambazo ni sawa na DTB iliyokuja kubadilishwa jina baadaye na kuitwa Singida Big Stars, zikitofautiana kwa mabao tu.

Ikiwa katika Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2022-2023, Ihefu ilianza kwa kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa maafande wa Ruvu Shooting, lililofungwa na aliyekuwa nyota wa kikosi hicho, Ally Bilaly dk19, katika pambano lililopigwa, Agosti 15, 2022.

Kwa upande wa DTB iliyotambulika baadaye kwa jina la Singida Big Stars, ilianza vizuri kwa ushindi wa bao 1-0 la nyota wa zamani wa kikosi hicho raia wa Brazil, Peterson Da Cruz 'Peu' dk36, katika mechi iliyopigwa, Agosti 16, 2022.

MTI 02

MSIMU WA 2022-2023

Huu ndio msimu uliopandisha timu tatu kwenda Ligi Kuu Bara zikitoka Championship, ambapo mbili zilizomaliza ya kwanza na ya pili zilipanda moja kwa moja kwa mujibu wa kanuni, huku nyingine ilipanda kupitia mechi za mtoan0 yaani playoffs.

Mabingwa msimu huo, walikuwa ni maafande wa JKT Tanzania waliomaliza na pointi 63, wakiungana na Kitayosce kupanda daraja ambayo baadaye ilibadilishwa jina na kuitwa Tabora United na sasa TRA United, iliyokuwa ya pili kwa kukusanya pointi 60.

Mbali na JKT na Kitayosce ambayo kwa sasa ni TRA United zilizopanda moja kwa moja, timu nyingine ni maafande wa Mashujaa ambao walipanda kwa kuishusha Mbeya City kwa jumla ya mabao 4-1, ambayo hata hivyo, imerejea tena msimu huu wa 2025-2026.

Baada ya kupanda Ligi Kuu, JKT ilianza vizuri na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya Namungo lililofungwa na Martin Kigi dk43, mechi iliyopigwa, Agosti 15, 2023, huku kwa upande wa Tabora United ikianza kwa kuchapwa mabao 4-0.

Tabora ambayo ni TRA United kwa sasa, ilichapwa mabao hayo na Azam, yaliyofungwa na Feisal Salum 'Fei Toto' aliyefunga matatu (hat-trick) ya dakika ya 3, 9 na 13, huku jingine moja likifungwa na Prince Dube anayeichezea Yanga katika dk5.

Hata hivyo, Tabora ilikuwa na wachezaji wanane uwanjani baada ya wengine kutokamilisha usajili, ambapo mechi ilichezwa kwa dakika 18 badala ya 90, kutokana na nyota wao wawili kuumia na kubakia sita ambao kikanuni hairuhusu pambano hilo kuendelea.

Kwa upande wa maafande wa Mashujaa ambao walipanda kupitia 'playoffs', walianza vizuri Ligi Kuu mechi ya kwanza, baada ya kuifunga Kagera Sugar mabao 2-0, Agosti 16, 2023, yaliyofungwa na Adam Adam dakika ya 15 na Othman Dunia katika dakika ya 73.

  

MTI 05

MSIMU WA 2023-2024

Msimu huu ilipanda KenGold iliyokuwa bingwa wa Championship ikimaliza na ointi 70, ikiungana na Pamba Jiji iliyomaliza ya pili kwa pointi 67, ambayo ilirejea Ligi Kuu Bara baada ya miaka 23, tangu iliposhuka daraja mwaka 2001.

Katika Ligi Kuu Bara, Pamba Jiji ikiwa nyumbani ilianza kwa suluhu (0-0), dhidi ya maafande wa Tanzania Prisons, katika pambano lililoshuhudia ushindani wa hali ya juu, lililopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Agosti 16, 2024.

Kwa upande wa KenGold ambayo imeshuka daraja ikitoka Championship baada ya kuburuza mkiani kwa pointi 16, ilianza vibaya kwa kuchapwa mabao 3-1, dhidi ya Singida Black Stars katika pambano lililopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mechi hiyo iliyopigwa, Agosti 18, 2024, ilishuhudiwa mabao ya Singida yakifungwa na Emmanuel Keyekeh dakika ya 41, Elvis Rupia dakika ya 61 na Mohamed Damaro dakika ya 81, huku bao la upande wa KenGold lilifungwa na Joshua Ibrahim dakika ya 68.

MTI 03

MSIMU WA 2024-2025

Msimu huo ulishuhudiwa Mtibwa Sugar iliyoshuka daraja msimu wa 2023-2024, kwa kuburuza mkiani na pointi zake 21, ikirejea tena Ligi Kuu Bara, baada ya kumaliza mabingwa wa Ligi ya Championship, kufuatia kukusanya jumla ya pointi 71.

Mtibwa iliungana na Mbeya City kupanda, baada ya timu hiyo ya Mbeya kumaliza nafasi ya pili na pointi 68, ikirejea tena Ligi Kuu, kufuatia kushuka msimu wa 2022-2023, ilipotolewa na Mashujaa kwa jumla ya mabao 4-1, katika mechi ya mtoano.

Mbeya City ndio pekee iliyoanza vizuri Ligi Kuu msimu huu wa 2025-2026, kwa kuifunga Fountain Gate bao 1-0, lililofungwa kwa penalti na Habib Kyombo katika dakika ya 56, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati, Septemba 18, 2025.

Kwa upande wa Mtibwa Sugar, imeanza Ligi Kuu msimu huu kwa kuchapwa bao 1-0 na maafande wa Mashujaa, lililofungwa na Idrisa Stambuli katika dk32, mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani Kigoma, Septemba 21, 2025.

Mara ya mwisho kwa Mashujaa na Mtibwa kukutana katika Ligi Kuu kabla ya pambano la Septemba 21, 2025, ilikuwa pia kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, ambapo kikosi cha maafande kiliibuka na ushindi wa mabao 3-2, Mei 25, 2024.

Mabao ya Mashujaa yalifungwa na aliyekuwa nyota wa kikosi hicho, Reliants Lusajo aliyefunga mawili na jingine la Mundhir Vuai, wakati ya Mtibwa yalifungwa na Seif Karihe, huku jingine ni la kujifunga mwenyewe la Samson Madeleke.