Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sauti zisizoisha ladha Krismasi

Muktasari:

  • Achana na ishu za kula, kunywa na kutembeleana, lakini kipindi hiki cha Krismasi kinabebwa na burudani ya muziki unaochukua nafasi muhimu katika tamaduni za watu duniani kote kutoka kwa ngoma za jadi hadi pop, rock na sauti za kisasa.

KRISMASI ni kipindi kinachochangamsha mioyo kwa furaha, upendo na matumaini kwa waumini wa dini ya Kikristo nchini na duniani kwa ujumla.

Achana na ishu za kula, kunywa na kutembeleana, lakini kipindi hiki cha Krismasi kinabebwa na burudani ya muziki unaochukua nafasi muhimu katika tamaduni za watu duniani kote kutoka kwa ngoma za jadi hadi pop, rock na sauti za kisasa.

Baadhi ya waimbaji na makundi wamekuwa maarufu kila Krismasi inapowadia kutokana na nyimbo zao zilizopendwa na kutangazwa kila ufikapo msimu huu.

Katika makala hii, tunaangazia kazi na mafanikio ya wasanii ambao nyimbo zao hutamba sana katika msimu kama huu kila mwaka kama Baba Gaston, Jim Reeves, Mariah Carey, ABBA, na Boney M na jinsi sauti zao zinavyoendelea kudunda majumbani mwa wengi na mitaani kipindi hiki.


1. BABA GASTON

(Kakolele Mama...Viva Krismasi...)

Utasema nini kuhusu wimbo huo maarufu kutoka kwa mwanamuziki Mkongomani aliyekuwa amelowea hapa Tanzania kabla ya kuhamia Kenya miaka ya 1970, Ilunga Omer 'Baba Gaston'.

Mwanamuziki huyo aliyebadilisha jina baada ya agizo la Rais Mobutu Seseko miaka ya 1970 na kujiita Ilunga Chenji Kamanda wa Kamanda, alitamba na bendi mbalimbali ikiwamo Orchestre Baba Nationale, ambayo ndio iliyozalisha kibao hicho cha Viva Krismasi...kisichochuja kwa miaka yote tangu kilipoachiwa mara ya kwanza miaka ya 1970 jijini Nairobi hadi alipofariki dunia mwaka 1997.

Baba Gaston aliyezaliwa mwaka 1936 huko Lubumbashi, DR Congo (Zaire ya zamani) kipindi hiki anafahamika zaidi kupitia wimbo huo wa Kakolele Viva Krismasi na nyingine.


2. JIM REVEES

Jim Reeves alikuwa msanii maarufu wa muziki wa country wa Marekani na sasa anajulikana kwa sauti ya baridi, lakini yenye hisia kali. Alizaliwa mwaka 1923 na kuacha alama isiyofutika katika muziki, ikiwa ni pamoja na nyimbo za Krismasi ambazo zimeendelea kusikika kwa vizazi vingi.

Ingawa Reeves hakuwa ameandaa albamu nyingi za Krismasi wakati wa maisha yake, sauti yake ya kipekee imeifanya “Silent Night”, “Oh Come, All Ye Faithful” na nyimbo nyingine za Krismasi kuwa za kukumbukwa zaidi. Sauti yake ya laini na yenye upole huwafanya wasikilizaji kuhisi amani na faraja, sifa zinazohusiana kwa undani na msimu wa Krismasi.


3. MARIAH CAREY

Hakuna mtu anayezungumziwa zaidi linapokuja muziki wa Krismasi kisasa kuliko Mariah Carey. Alizaliwa Marekani, Mariah ni mmoja wa wasanii waliopata mafanikio makubwa zaidi katika muziki wa pop duniani. Lakini tangu 1994, wimbo wake wa Krismasi “All I Want for Christmas Is You” umekuwa maarufu kimataifa.

Wimbo huu umeshika rekodi kwa mara nyingi kutamba katika chati mbalimbali kila msimu wa Krismasi, na kusababisha Mariah apewe maua yake kama “Malkia wa Krismasi.” Bila shaka, sauti yake ya juu na mtiririko wa midundo unaovutia umemfanya Mariah Carey kuwa mtunzi na muimbaji anayeheshimiwa sana. Pia ametunga na kuachia matoleo mengine ya Krismasi kwenye albamu zake, lakini hakuna iliyokamata kama All I Want for Christmas Is You — wimbo ambao umekuwa msingi wa utamaduni wa sikukuu kote duniani.


4. ABBA

ABBA ni kundi la pop kutoka Uswidi lililojulikana kwa sauti za kipekee na nyimbo zenye melodi tamu. Ingawa ABBA haikuwa maarufu kwa albamu za Krismasi kama wengine, baadhi ya nyimbo zao zimekuwa sauti za kuvutia katika kipindi cha sikukuu kutokana na hisia za furaha na kumbukumbu.

Katika baadhi ya nchi, nyimbo kama Happy New Year mara nyingi huchezwa wakati wa msimu wa mwisho wa mwaka na Krismasi, zikitumia muundo wa muziki wa ABBA kuleta furaha na matumaini kwa wasikilizaji. Muziki wa ABBA umevuma duniani kote, na kila Krismasi katika mikutano ya familia mara nyingi hujumuisha nyimbo zao zinazoburudisha na kuamsha hisia nzuri.


5. BONEY M

Boney M ni kundi la disco-latin kutoka miaka ya 1970, lililojulikana kwa mitindo ya kipekee na midundo ya kuvutia. Lilipata umaarufu mkubwa kwa nyimbo kama Rivers of Babylon na Daddy Cool, lakini moja ya michango yake ya kudumu kwa msimu wa Krismasi ni wimbo “Mary’s Boy Child – Oh My Lord.”

Wimbo huu, uliochanganywa kwa ustadi wa sauti za vichwa vya ngoma za disco na ujumbe wa Krismasi kuhusu kuzaliwa kwa Yesu Kristo, umekuwa kipenzi cha sikukuu. Kutokana na midundo yenye nguvu na sauti za kuimba pamoja, wimbo huu umekuwa sehemu ya utamaduni wa Krismasi maeneo mengi, hasa Ulaya na Marekani.


KENNY RODGERS

Kenny Rogers alikuwa mwimbaji mashuhuri wa Marekani mwenye sauti nzito na ya hisia, aliyependwa duniani kote. Mbali na nyimbo zake za kawaida kama The Gambler na Lucille, Kenny Rogers aliacha alama kubwa katika muziki wa Krismasi.

Albamu na nyimbo maarufu za Krismasi ni pamoja na Christmas (1981) – albamu yake maarufu zaidi ya Krismasi, Silent Night, Little Drummer Boy, Away in a Manger na White Christmas

Kenny Rogers pia alirekodi wimbo wa Krismasi “Once Upon a Christmas” (1984) pamoja na Dolly Parton, wimbo ambao umeendelea kupendwa kwa miongo mingi kutokana na ujumbe wake wa amani na matumaini.