Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Sare ya Liverpool, mashabiki wamshambulia Arne Slot

Muktasari:

  • Kikosi hicho kilichoanza mchezo huo juzi bila kuwa na baadhi ya mastaa kama Ibrahima Konate katika beki ya kati, Federerico Chiesa, Hugo Ekitike na Mohamed Salah kilionyesha mchezo wa kawaida, huku kikiwapa nafasi wapinzani wake nafasi ya kupambana walau kurejesha imani ya mashabiki baada ya matokeo yasiyoridhisha siku za karibuni.

LIVERPOOL, ENGLAND: UAMUZI wa kushangaza wa kimkakati wa kocha Arne Slot huku Liverpool wakijikuta wakiteleza kwa sare dhidi ya Tottenham Hotspurs kwenye Ligi Kuu England, umepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa timu hiyo ambao wameshutumu wakidai ameinyima ushindi.

Kikosi hicho kilichoanza mchezo huo juzi bila kuwa na baadhi ya mastaa kama Ibrahima Konate katika beki ya kati, Federerico Chiesa, Hugo Ekitike na Mohamed Salah kilionyesha mchezo wa kawaida, huku kikiwapa nafasi wapinzani wake nafasi ya kupambana walau kurejesha imani ya mashabiki baada ya matokeo yasiyoridhisha siku za karibuni.

Hata hivyo, lawama zaidi zilikuwa katika fomesheni ambayo Slot aliingia nayo uwanjani, ambao ilionekana kana kwamba mastaa wa kikosi hicho wakicheza bila umakini na kuishia sare dhidi ya timu inayopambana kutoshuka daraja.

Kwa kawaida, Liverpool na Spurs huzalisha mabao mengi, na kutokana na kiwango cha hivi karibuni cha Tottenham, baadhi ya mashabiki walitabiri matokeo ya mabao mengi. Hata hivyo, ilikuwa ni hadithi ileile ya Liverpool msimu huu; walionekana kukosa mpangilio dhidi ya timu ambayo inaonekana kama imekata tamaa.

Dominik Szoboszlai aliitanguliza Liverpool kwa bao la ustadi, lakini mambo yalibadilika mwishoni pale Richarlison - mchezaji wa zamani wa Everton alipofunga bao la kusawazisha kwa kusukuma mpira wavuni mbele ya kipa Alisson Barker katika dakika za mwisho za mchezo.

Bao hilo liliibua mtazamo kwamba Liverpool inaonekana kama timu isiyo na mtindo maalumu wa uchezaji, kwani kuna wakati inakosa mbinu za kuwamudu wapinzani wake, jambo lililomfanya Slot kumpa nafasi chipukizi Rio Ngumoha nafasi ya kuanza kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu England akiwaacha benchi wakongwe.

Ngumoha alionekana kuwa bora akitoa ubunifu katika timu ambayo imekuwa ikitafuta sana mchezaji wa kuleta mabadiliko na kulinganishwa na Max Dowman, ambaye aliisaidia Arsenal kupata mafanikio Jumamosi dhidi ya Everton ambapo iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Ngumoha alicheza kwa ujasiri bila woga na hakuonekana kutikiswa alipokuwa akiikabili Spurs ambayo ni moja ya timu kubwa England na ni wazi kwamba alikuwa miongoni mwa wachezaji bora wa Liverpool kabla ya kutolewa kipindi cha pili.

Liverpool wanapigania nafasi ya kufuzu mashindano ya Ulaya, na ilipaswa kuifunga timu dhaifu ya Spurs kwa urahisi,

lakini mbinu za baadaye ziliruhusu Spurs kurudi mchezoni, ambapo mchezo ulikuwa wa kushambuliana kwa zamu, hali ambayo haikupaswa kutokea.

Akizungumzia mwenendo wa Liverpool, staa wa zamani wa Manchester City na mmoja wa wachambuzi wa soka wa England kwa sasa, Shaun Wright-Phillips alisema iwapo Liverpool ina nia ya kweli ya kufuzu michuano ya Ulaya msimu ujao mechi kama hizo zinapaswa kumalizwa mapema na siyo kugeuzwa kuwa za presha kubwa mwishoni.

Matokeo hayo kwa Slot ni vigumu kuyatetea, lakini kwa kocha wa Spurs, Igor Tudor ni ya thamani kubwa, kwani amekalia kuti kavu kutokana na namna kikosi chake kinavyocheza na kupata matokeo uwanjani.

Alisema, Liverpool walikuwa na nafasi ya kuingia katika nne bora wakiipita Aston Villa ambayo ilipoteza dhidi ya wapinzani wa muda mrefu, Manchester United. Na sasa Liverpool wako hatarini kumaliza msimu bila kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya, miezi 12 tu baada ya kutawazwa mabingwa wa England.