Sakho, Mayele mwendo wa pesa tu! Banda, Makambo nao ndani
Muktasari:
HAKUNA siri, madini ni moja ya rasilimali zinazoliingiza taifa mapato makubwa kutokana na thamani yao. Lakini kama hujui hata kwenye soka kwa sasa kuna ‘madini’ mengine ambayo yamekuwa yakiliingiza soka mkwanja wa maana. Ni nyota wa kigeni wanaosajiliwa na klabu mbalimbali nchini kila msimu.
HAKUNA siri, madini ni moja ya rasilimali zinazoliingiza taifa mapato makubwa kutokana na thamani yao. Lakini kama hujui hata kwenye soka kwa sasa kuna ‘madini’ mengine ambayo yamekuwa yakiliingiza soka mkwanja wa maana. Ni nyota wa kigeni wanaosajiliwa na klabu mbalimbali nchini kila msimu. Klabu zimekuwa zikisajili nyota wa kigeni kutoka nje ya nchi ambao wamekuwa wakilitunisha mfuko wa soka kwa namna fedha zinazotozwa kwa kuwepo kwao haopa nchini, kiasi hata zile kelele za wadau kwamba ongezeko la wageni katika Ligi Kuu Bara ni msala, hakuna anayezisikiliza.
Wingi wa maproo hao umekuwa na faida nyuma yake hata nje ya soka.
Kwa taarifa ambazo Mwanaspoti limezinyaka kwa msimu huu kuna wachezaji wa kigeni 77 na kila mmoja hulipa Sh 4 milioni TFF kwa mwaka ambapo ni sawa na Sh 333,333 kwa mwezi na kwa jumla yao inaonyesha TFF huvuna kiasi cha Sh 308 milioni kwa mwaka.
Upande wa Uhamiaji mchezaji hulipa dola 2050 sawa na wastani wa Sh 4.7 milioni ili kupata kibali cha kuishi hii haijalishi mkataba wake na timu ni wa muda gani kwani hulipa mara moja kulingana na mkataba wake wa kazi. Hivyo serikali huingiza Sh 360 milioni kwa mwaka.
Kwa upande wa Wizara ya Kazi, kila mchezaji hulipa dola 1000 wastani wa Sh 2.3 milioni hivyo kwa wachezaji 77 huingiza kiasi cha zaidi ya Sh 154 milioni.
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) wenyewe huchukuwa dola 500 wastani wa Sh 1 milioni kwa kila mchezo hivyo kwa mwaka kwa wachezaji 77 huingiza Sh 77 milioni.
Dirisha la usajili la wachezaji lilifungwa usiku wa Agosti 31 na jumla ya mataifa 16 yapo kwenye Ligi Kuu pamoja na Championship League (zamani Ligi Daraja la Kwanza).
Kwa upande wa soka la wanaume Taifa la Congo DRC ndio linaongoza kuwa na wachezaji wengi (16) huku Yanga pekee ikiwa na Wakongo saba, Uganda wachezaji (9), Burundi (8), Ghana na Kenya (7).
Zambia na Zimbabwe (5) Cameroon (4), Malawi (3), Nigeri, Bukina Faso, Rwanda na Mali (2), Senegal, Ivory Coast, Msumbiji wakiwa na mchezaji mmoja na kufanya jumla ya wageni 77.
Wachezaji hao wanatoka kwenye timu tisa za Ligi Kuu na timu nne za FDL huku Yanga na Simba zikionekana kuwa na wachezaji wengi zaidi (12) na Azam akiwa na wageni 10 na kule FDL, DTB ikisajili wageni saba.
Kwa upande wa Ligi Kuu ya Wanawake ina jumla ya wachezaji 33 na Kenya inaongoza kuwa na idadi kubwa ya wachezaji hapa Tanzania wakiwa na wachezaji 19.
Nayo TSC Queens ikiwa na wachezaji saba wote raia wa Kenya huku The Tiger Queens ikiwa na wachezaji wengi zaidi kuliko timu yoyote (8), hivyo kufanya jumla ya wachezaji wa kigeni 110.
Kwa maana hiyo TFF inaingiza kwa mwaka mmoja Sh 308,000,000 milioni kwa upande wa Ligi Kuu Bara na FDL kwa upande wa Ligi Kuu ya Wanawake wapo 33 ina maana TFF inaingiza Sh 132,000,000 milioni kwa mwaka na kufanya kwa mwaka kukusanya Sh 440,000,000 milioni.
Mwanaspoti linakuletea kila timu na idadi ya wachezaji wageni waliokuwa kwenye timu hizo.
DTB FC -7
Amissi Tambwe - Burundi
Danny Phiri - Zimbabwe
Emmanuel Ngama - Burundi
Hemedy Murutabose - Burundi
Nicholas Gyan- Ghana
Owen Chaima - Malawi
Tafadzwa Kutinyu - Zimbabwe
GWAMBINA FC -4
Kone Moustapha - DR Congo
Ndongo Michel - Cameroon
Olivier Kabangu - DR Congo
Wandaman Kabongo -Congo
KITAYOSA FC -2
Katende Elie - DR Congo
Tshama Nsumbu- DR Congo
AFRICAN LYON -2
Apheal Femi Aloba - Nigeria
Solomon Mutapili -Zimbabwe
SIMBA -12
Baka Inonga-DR Congo
Banda Peter- Malawi
Bernard Morrison-Ghana
Bwalya Rally- Zambia
Duncan Nyoni- Malawi
Kagere Medie-Rwanda
Kanoute Sadio- Mali
Chriss Mugalu- DR Congo
Onyango Joash - Kenya
Pape Sakho - Senegal
Pascal Wawa - Ivory Coast
Taddeo Lwanga - Uganda
YANGA -12
Bangala Yannick - DR Congo
Djigui Diarra - Mali
Djuma Shabani - DR Congo
Fiston Mayele - DR Congo
Heritier Makambo -DR Congo
Jimmy Ukonde - Msumbiji
Khalid Aucho - Uganda
Moloko Jesus - DR Congo
Mukoko Tomombe - DR Congo
Saidi Ntibazonkiza - Burundi
Yacouba Songne- Burkina Faso
AZAM FC -10
Bruce Kangwa - Zimbabwe
Charles Zulu - Zambia
Daniel Amoah -Ghana
Kenneth Muguna - Kenya
Mathias Kigonya-Uganda
Nico Wadada - Uganda
Paul Katema -Zambia
Prince Dube -Zimbabwe
Rodgers Kola
- Zambia
Yvan Mballa - Cameroon
BIASHARA UNITED -7
Ambrose Awio - Uganda
Baron Oketch - Kenya
Christian Zigah - Ghana
James Ssetuba - Uganda
Metthew Odongo-Uganda
Opare Collins - Ghana
Shaphan Siwa- Kenya
NAMUNGO FC -6
Bigirimana Blaise - Burundi
David Molinga- Dr Congo
Eric Kwizera - Burundi
Jonathan Nahimana - Burundi
Obrey Chirwa - Zambia
Stephen Sey - Ghana
COASTAL UNION -5
Joseph Zziwa - Uganda
Ngamchiya Amza - Cameroon
Pasco Kitenge - DR Congo
Sosthenes Idah - Kenya
Victor Akpan - Nigeria
KAGERA SUGAR -5
Nouridine Balora -Burkina Faso
Ppolinaire Tientcheu- Cameroon
Ackson Harodi-Uganda
Stephen Duah- Ghana
Timothy Omwenga- Kenya
KMC FC -3
Emmanuel Mvuyekure- Burundi
Faruk Shikhalo- Kenya
Jean Mugiraneza -Rwanda
MTIBWA SUGAR -2
Boban Zirintusa -Uganda
Nzigamasabo Styve- Burundi
LIGI KUU YA WANAWAKE
ALLIANCE GIRLS-3
Anita Agunda-Kenya
Eliver Mungo-Kenya
Florida Omusanga-Kenya
BAOBAB QEENS-1
Jeanne Pauline-Rwanda
FOUNTAIN GATE PRINCESS FC-4
Carolyne Rufa-Kenya
Faith Machora-Kenya
Niyonkuru Sandrine-Burundi
Pauline Kathuruh-Kenya
RUVUMA QUEENS-3
Fanis Kwamboka-Kenya
Nakasumba Fatumah-Uganda
Rachele Gakima-Burundi
SIMBA QEENS-4
Asha Djafari-Burundi
Danai Bhobho-Zimbabwe
Joelle Bukuru-Burundi
Musolo Mawete-DR Congo
TIGER QUEENS-8
Alice Kalimba-Rwanda
Diana Koske-Kenya
Drailer Sati-Kenya
Elizabeth Katungwa-Kenya
Linda Kihara-Kenya
Natasha Witika-Zambia
Samantha Okeya-Kenya
Zakia Umubyeyi-Rwanda
TSC QUEEN -7
Cynthia Matekwa-Kenya
Fridhaus Mwakaga-Kenya
Meali Bakari-Kenya
Micky Emma-Kenya
Nanzugu Chilo-Kenya
Vereneta Mkoa-Kenya
Zaithuni Ali-Kenya
YANGA PRINCESS -3
Aniella Uwimana-Burundi
Daniela Kanyanya-DR Congo
Olga Kalamba-DR Congo