Nyota Tembo Warriors wapasua anga

UNAWEZA kusema ni neema imewatembelea vijana wanne wa timu ya soka ya walemavu nchini maarufu kama Tembo Warriors baada ya kupata ofa ya kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Uturuki baada ya kuonyesha kiwango kizuri katika mashindano ya Afrika mwaka jana.
Vijana wao ni Frank Ngailo ambaye teyari kashatua Uturuki mwezi Januari huku wenzake watatu wakifuata mwenzi huu ambao ni Ramadhani Chomelo, Alfan Kiyanga pamoja na Sherdrack Hebron
FRANK NGAILO
Ngairo alipata nafasi ya kwenda kufanya majaribio nchini Uturuku katika moja ya klabu kubwa inayoshiriki Ligi Kuu ya soka kwa watu wenye ulemavu nchini humo, Izmir BBSK siku chache tu baada ya kutangazwa kuwa ni mchezaji wa bora wa mashindano ya Bara la Afrika ya soka kwa watu wenye ulemavu (CANAF) yaliofanyika hapa nchini na huku akiwa na mchangomkubwa wa kuipeleka Tanzania Kombe la Dunia ambapo aliifungia timu yake mabao matano.
Kiungo huyo maarufu kama ‘Mbappe’ aliiambia Nje ya Bongo kuwa hakutarajia na wala hakua na mategemeo yakwenda kucheza soka la kulipwa nje kwa wakati huu.
“Alinitafuta nahodha wa timu ya taifa ya Misri, Mahmud Tawfik mara baada tu ya mashindano kufungwa kisha akaniaomba namba zangu za simu na akaniambia kuwa kocha wa klabu yake (Izmir) anahitaji kuzungumza na mimi”
“Siku iliyofuata kocha huyo alinitafuta na kuniuliza kama naweza kujiunga na klabu hiyo nami nikamjibu kuwa naweza pia nikwambia awataarifu uongozi wangu kuhusiana na suala hilo” anasema Ngailo
Ngailo anasema changamoto iliyomkabili wakati anawasili kwa mara ya kwanza nchini humo ni ya nje ya uwanja akiitaja kuwa ni hali ya hewa ya mji wa Izimir ingawa aliamini kuwa ni jambo la muda tu kwani ataizoea.
“Hali ya hewa ya Huku ni tofauti na ya nyumbani muda mwingi ni baridi tu ingawa hata kule kwetu Ludewa kuna baridi lakini sio Kama nililolikuta Izimir” anaendelea na kusema;
“Namshukuru Mungu nimeanza kuonyesha makali yangu lakini pia siku ya Kwanza ilikua siku nzuri kwangu kwani niliweza kupata nafasi ya kuwatambua wachezaji wenzangu” anasema Ngailo akiwa nchini Uturuki.
Mwanaspoti lilifanikiwa kumpata kocha wa klabu hiyo ya nchini Uturuki, Uvren Uyanik ambapo alilithibitisha yota huyo na kusema alifika salama na tayari ameshaanza kuonyesha moto wake kwa kufunga mabao matano kwenye michezo mitatu kiasi cha kupewa mkataba.
“Najua kuwa siku za mwanzoni mazingira ya Izimir yalitakua changamoto kwake lakini licha ya hivyo bado alionyesha kiwango chake siku ya kwanza katika uwanja wa mazoezi hivyo ninatarajia kuona mengi kutoka kwake,” anasema Uyanik.
Klabu hiyo ya Izmiri BBSK inayoshiriki ligi kuu ya soka la walemavu nchini Uturuki ipo nafasi ya nne katika msimamo na inashikilia vikombe takribani kumi za ligi hiyo huku ikwa na makombe mbalimbali yasoka la walemavu nchini humo na barani Ulaya.
WATATU WAMFUATA
Wakati kikosi cha Tembo Warriors kikijichimbia kambini kwaajili ya kujiandaa na kombe la dunia mwaka huu, wachezaji watatu wa kikosi hicho nao wanajiandaa kutimkia Uturuki kwaajili ya kwenda kucheza soka la kulipwa katika Ligi Kuu ya soka la walemavu nchini humo.
Shirikisho la soka la walemavu nchini (TAFF) liliithibitishia Nje ya Bongo kuwepo kwa ofa hiyo kutoka kwa vigogo wa soka la wamelavu nchini Uturuki ambapo walibainisha kuwa ni wachezaji watatu pekee waliopata nafasi ya kwenda kuungana na mwenzao Ngailo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na safu hii, Kiyanga ambaye ni mshambuliaji anaenda kujiunga na Sisli Yeditepe anasema kuwa kwake ni fahari kubwa katika historia yake ya soka la walemavu kwani anaamini ataenda kuafanya makubwa zaidi na kutambulika Duniani kote.
“Ilikua ni moja ya ndoto zangu kuwa siku moja niweze kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi na sasa inaenda kutimia hivyi lazima niwe na furaha kubwa ingawa siku tegemea kwa wakati huu kama ningeweza kuvuna ofa hii kubwa katika masiha yangu ya soka” anasema Majani mwenye jumla ya mabao 20 katika kikosi cha Tembo warriors.
Naye pia Sherdrack Hebron beki wa kati wa Tembo Warriors ambaye anakwenda timu moja na Majani anasema kuwa anaamini kuwa hii nafasi imekuja muda sahihi kwake ingawa pia hakutarajia kama angekua mmoja wa safari hio.
Aidha pia Ramadhani Chomelo maarufu kama ‘Chama’ wa kikosi hicho yeye atakwenda kuichezea timu ya Konya ianayopatikana katika mkoa wa konya nchini hum ambapo hakua tofauti na wachezaji wenzake kuhusina na usajili wao kulekelekea nchini Uturuki.
“Kikubwa wadau wa soka la walemavu watuombee dua ili kuhakikisha tunapata nafasi katika vikosi vyetu ili kuhakikisha tunafanya makubwa ndani na nje ya Ligi hiyo pendwa nchini humo jambo ambalo litaweza pia kuchochea ujio wa watanzania wengine kuutazama soka letu.”