Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NINAVYOJUA : Uwazi unahitajika kipindi kigumu cha uendeshaji soka

Muktasari:

Tatizo la wenye timu hizo zinazogombania kuchukua ubingwa na zinazotaka zisishuke daraja hazipiganii vita hii ndani ya viwanja tu, wanatoka na kupigana hadi nje ya uwanja wa kuchezea na nje ya dakika 90. Wanafanya haya kabla ya michezo yao na kuelekea michezo mingine!

INAWEZEKANA kabisa wadau wa soka nchini hawataki kufuatilia kwa umakini kujua nini kinachoendelea kwenye soka letu. Wao wanataka kuona timu zao kubwa za Simba, Yanga na Azam zikishinda mechi zao kuelekea kwenye ubingwa wa Ligi Kuu Bara na pia kupambana ili timu zao zisishuke daraja.

Tatizo la wenye timu hizo zinazogombania kuchukua ubingwa na zinazotaka zisishuke daraja hazipiganii vita hii ndani ya viwanja tu, wanatoka na kupigana hadi nje ya uwanja wa kuchezea na nje ya dakika 90. Wanafanya haya kabla ya michezo yao na kuelekea michezo mingine!

Nchi inatakiwa kuwa makini kweli, kama tunataka tutoke hapa tulipo na tufike hatua mbili tatu mbele, tukiendelea kuachia uharibifu huu uendele kufanyika tutavinyima haki ya kupata maendeleo ya kweli ya soka vizazi vijavyo.

Tukiendelea kufanya haya kuna siku wadhamini wakubwa wa ligi wakielewa hilo watakimbia kama wenzetu Kenya walivyokimbiwa na wadhamini kabla ya sasa kurejea tena baada ya kuingia madarakani uongozi mpya wa FKF.

Tatizo kubwa ni kwamba wadau hawataki kujua ukweli zaidi ya kuweka ushabiki mbele, huku wakiwa hawataki kupata suluhisho la kudumu la kuifanya ligi yetu kuwa imara.

Kuna mambo machache makubwa ambayo yanakifanya kipindi hiki kuonekana kama kigumu, hivyo kunatakiwa juhudi za makusudi kuepusha kuporomoka kwa soka letu.

Kwanza tuzungumzie suala la upangaji wa matokeo, ambalo wadau wanapolisikia wanachoelewa ni kwamba upangaji wa matokeo hutumika kwenye ligi za madaraja ya chini tu, yaani Daraja la Tatu Kanda, la Pili ama la kwanza, lakini wamesahau kuwa hata huku kwenye Ligi Kuu kuna upangaji wa matokeo!

Hali sasa iko hivi timu zimesalia na michezo michache kama za raundi sita hivi ingawa Azam na Yanga zitaendela kubakia na michezo mitatu kibindoni, timu kubwa zinautaka ushindi uwanjani kwa hali na mali huku baadhi ya wachezaji wa timu zinazocheza dhidi timu kubwa zenye uwezo na uthubutu wa kutumia pesa kupata ushindi, wakiwaza utajiri.

Wakitumia michezo hiyo kama mitaji ya kupata vipato nje ya mishahara na posho zao, wapo tayari kuuza thamani ya kazi zao ili tu kupisha ushindi rahisi kwa timu zinazoutaka ubingwa kwa udi na uvumba.

Kuna kazi kubwa pia ya kuzuia wimbi la pesa za mlango wa nyuma zisiwafikie baadhi ya waamuzi wenye udhaifu wa kuweza kuisaliti thamani ya utu wa kazi zao.

Lakini kikubwa katika hili na ambacho kipo na sasa kilifikia kufanyika hadharani ni jinsi timu zetu zinazotoka madaraja ya chini zinavyohangaika kupata ushindi kwa kufanya mipango nje ya uwanja. Huku chini kuliko daraja la pili, la kwanza wanaotafuta nafasi ya kupanda daraja hawaoni aibu kuinunua timu nzima kwa kuigharamia ili iweze kufika na kucheza chini ya viwango kuwapa nafasi wale wanaotaka kupanda na walio na pesa mkononi!

Unafikiri unaweza kupanda daraja bila kuwa na fungu rasmi la pesa itakayoweza kukurahisishia safari hiyo? Huwezi hata kidogo! Katika hili tunahitaji uendeshaji wa ligi ya uwazi hasa zikifuatiliwa na watu wengi walio juu kutoka Bodi ya Ligi (TPLB) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Pili ni jinsi TFF linavyotumia muda mwingi kufikia uamuzi wa kujua nani anahusika na nani hahusiki katika sakata zima la upangaji wa matokeo unaozungumziwa kuzihusu timu za JKT Kanembwa, Geita Gold, Polisi Tabora na Oljoro JKT.

Katika mazingira ya soka la Tanzania huwezi kulifanya jambo kubwa kama hilo kwa kushirikisha wajumbe wanaounda Kamati ya Nidhamu tu peke yao bila kuvishirikisha vyombo vikubwa vya uchunguzi nchini.

Suala hilo ni tata linalohitaji watu wasio na aibu na viongozi wa soka nchini ili kutoa uamuzi utakaokuwa wa haki. Lakini katika kushughulikia suala hili bila uwazi wadau wengine wa soka wataendelea kuteseka.

Kwani iwapo suluhisho la upangaji matokeo lingekuwa limeshaisha bila shaka wadau wote tungeshajua kama ni timu ngapi zinashuka na ngapi zinapanda kwa utaratibu upi. Ndio maana nasisitiza kuwa inahitajika uwazi ili kufikia maendeleo ya soka.