Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ngumi zilivyotusua mbele ya soka

NGUMI Pict

Muktasari:

  • Mbali hao lakini upande wa tuzo ya mwamuzi bora wa kike kwa mwaka 2023 ilienda pia katika mchezo wa ngumi za kulipwa kwa mwamuzi Pendo Njau kushinda tuzo hiyo.

WIKIENDI iliyopita wadau wa michezo nchini walishuhudia msimu wa tatu wa tuzo za Baraza la Michezo la Taifa (BMT), kwa mwaka 2024 ambapo wanamichezo mbalimbali walifanikiwa kushinda.

Katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo ambazo zilifanyika kwenye Ukumbi wa Super Dome, Masaki, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa ambaye alikuwa mgeni rasmi, mchezo wa ngumi umeonyesha kuwa na nguvu na ushawishi msimu wa pili mfululizo kutokana kufanya vizuri kwa washiriki wake kuweza kushinda tuzo mbalimbali kwenye tuzo hizo.

Katika msimu uliopita, tumeshuhudia katika mchezo wa ngumi za ridhaa ukitoa mwanamichezo bora wa mwaka 2023 wa kiume ambaye alikuwa Yusufu Changalawe na tuzo ya mwanamichezo bora wa kike kwa mwaka 2023 ikienda pia kwenye ngumi za ridhaa kwa mshindi akiwa Grace Mwakamele.

Mbali hao lakini upande wa tuzo ya mwamuzi bora wa kike kwa mwaka 2023 ilienda pia katika mchezo wa ngumi za kulipwa kwa mwamuzi Pendo Njau kushinda tuzo hiyo.

NGUM 05

Katika tuzo zilizotolewa mwaka huu ambazo ni msimu wake wa tatu kuandaliwa na baraza hilo kwa kujumuisha michezo yote  ambayo washiriki wake hupatikana kupitia vyama shiriki vya michezo ambavyo vipo chini ya baraza kwa mujibu wa sheria za nchi.

Mchezo wa ngumi za kulipwa na ridhaa 2024 umetoa washiriki katika vipengele vitano ambavyo tuzo ya kocha bora wa mwaka 2024 ambayo ilikuwa ikiwaniwa na Hemedi Moroco ambaye ni kocha wa timu ya taifa 'Taifa Stars' na kocha wa timu ya taifa ya ngumi za ridhaa, Samwel Kapungu 'Batman'.

Lakini kipengele cha mwamuzi bora wa kike 2024, ngumi za kulipwa zilikuwa na mwakilishi mmoja ambaye ni Pendo Njau, Tatu Malogo wa mchezo wa soka na Nasma Kiranga wa kikapu.

Kipengele cha mwanamichezo bora wa kike ambacho ngumi za kulipwa zilikuwa na mwakilishi mmoja mbaye ni Rehema Abdallah huku washiriki wengine wakiwa ni Aisha Masaka wa soka na Madina Iddi wa gofu.

NGUM 01

Upande wa mwanamichezo bora 2024 ngumi ilionyesha nguvu kutokana na kutoa washiriki wawili ambao Yusufu Changalawe (ngumi za ridhaa) na Fadhili Majiha zile za kulipwa na mshiriki mwingine akiwa Alphonce Simbu wa riadha.

Lakini mchezo wa ngumi ukachomoza tena kwenye kipengele cha timu bora ya taifa ambayo ilikuwa ikichuana na Taifa Stars pamoja na kriketi.

Sasa basi, tuzo ya Mwanamichezo Bora 2024 ngumi za kulipwa zimevunja rekodi ya ngumi za ridhaa 2023 kufuatia bondia wa ngumi za kulipwa, Majiha kushinda tuzo mbele ya mshindani wake aliyekuwa akitetea tuzo hiyo, Changalawe.

Majiha alishinda tuzo hiyo kutokana na mwaka 2024 kutetea mkanda wake wa ubingwa wa Baraza la Ngumi Duniani kwa kanda ya Afrika (WBC Afrika) ambaye amekuwa bondia kwanza kubeba ubingwa huo tangu kuanzishwa kwake.

NGUM 04

Lakini, kwenye nafasi ya viwango vya ubora alipanda hadi kuwa namba moja Afrika katika mabondia 150 wa uzani wake (bantam) na bondia namba moja Tanzania katika mabondia wote hadi sasa, huku akiwa namba moja kwenye uzani wake nchini katika mabondia 58, ilhali akiweka rekodi ya kuwa bondia wa kwanza wa Tanzania kuwa ndani ya 10 bora ya mabondia bora duniani kati ya mabondia 1175.

Ushindi huo umemfanya Majiha kutoa neno,"Nashukuru Mungu kwa sababu nimefanikiwa kushinda na hii ni heshima kubwa kwetu watu wa ngumi kuona serikali inatambua mchango wetu katika huu mchezo. Binafsi naweza kusema kwamba wakati wa Mungu ni wakati sahihi kwa sababu hii tuzo nilikuwa nastahili kushinda muda mrefu kwa rekodi ambayo nimeweka kwenye huu mchezo, lakini pengine haukuwa wakati wangu kama ulivyokuwa sasa.

NGUM 02

"Niseme tu kwamba jambo kubwa ambalo kwa sasa limefanyika nadhani ni wakati wa kuendelea kuongeza juhudi kufanya makubwa zaidi ya haya. Nimekuwa nikiitwa Tanzania One na wengine wamekuwa wakipinga lakini ujio wa hii tuzo ya mwanamichezo bora wa kiume mwaka 2024 itavunja kila kitu."

Lakini, mambo yalikuwa pia matamu zaidi upande wa kocha bora 2024, kwani sehemu kubwa ya wanamichezo waliamini na kuona tuzo moja kwa moja itakwenda kwa Morocco kutokana na mambo makubwa aliyofanya Taifa Stars, lakini wakasahau jina la  Kapungu 'Batman' aliyeibuka mshindi kutokana kuipa mafanikio makubwa timu ya taifa ya ngumi za riadhaa 2024.

Mwaka 2024 kocha huyo aliipa Tanzania medali ya shaba kwenye mashindano ya Afrika yaliyofanyika DR Congo kupitia bondia Najma Isike, lakini ameipa medali nyingine sita kupitia mashandano ya All Africa Games yaliyofanyika DR Congo na mashindano ya Mandela yaliyofanyika Afrika Kusini.

Kwa upande wake, kocha huyo anasema kuwa ushindi umekuja kama miujiza kwa kuwa hakutegemea kuupata mbele ya soka ambayo imekuwa ikipendwa na watu wengi, lakini imekuwa ukifanya vizuri pia.

NGUM 03

"Binafsi sikutegemea kama nitaweza kushinda hii tuzo. Upinzani ulikuwa upande wa mtu ambaye nilikuwa nawania naye, lakini nashukuru Mungu nimefanikiwa. Hii imekuwa deni kwa mwaka huu tuweze kufanya vizuri ili mwakani tuchukue tena,"  anasema.

Kwa wanaume nako mambo yalikuwa bambam kwani tuzo ya timu bora ya taifa iliangukia kwa ile ya ngumi za ridhaa maarufu kama Faru Weusi wa Ngorongoro ikifanikiwa kuibuka mshindi mbele ya Taifa Stars na ile ya kriketi.

Timu hiyo ambayo ipo chini ya Shirikisho la Ngumi za Ridhaa ilishinda tuzo kutokana na ushindi wa medali za shaba katika mashindano ya Afrika ambayo Tanzania ilipata moja ya shaba kupitia bondia Najma Isike.

Pia Faru Weusi wa Ngorongoro walifanikiwa kushinda medali za shaba kwenye michuano ya All Africa Game ambapo washindi walikuwa ni Changalawe, Mussa Maregesi na Ezra Paul kisha ikashinda medali zingine kwenye michuano ya Mandela, Afrika Kusini.