Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mugalu: Kama si majeraha, wangenikoma

Mugalu: Napitia kipindi kigumu

STRAIKA wa Simba Chris Mugalu (32) ni miongoni mwa wachezaji wanaomaliza mikataba yao mwisho wa msimu huu ndani ya kikosi hicho huku kukiwa na mazungumzo ya kumwongezea mkataba mpya.

Mugalu pia ni mmoja wa mastraika wenye uwezo wa kufunga na amefanya hivyo akianzia Ligi Kuu ya Zambia na hata msimu wake wa kwanza hapa Tanzania amedhihirisha ubora wake baada ya kumaliza na mabao 15 huku akikosa mechi nyingi.

Kwa sasa kuelekea mzunguko wa pili, Mugalu ana kazi ya kuonyesha kiwango zaidi ili kusalia ndani ya timu hiyo msimu ujao licha ya mazungumzo ya mkataba mpya kuendelea.

Katika mahojiano maalumu na Mwanaspoti amefunguka mambo mbalimbali aliyokutana nayo misimu miwili akiwa na kikosi hicho.


USAJILI WAKE

Anasema Yanga alizungumza nayo lakini wakati wanarudi ili kumalizana naye, tayari alishatua Simba; “Wakati Yanga wanarudi tena kwangu kwa mara ya pili kuuliza kama nipo tayari juu ya suala lao, tayari nilishamalizana na Simba na nilikuwa nasubiria tu tiketi ili nije Tanzania,” anasema na kuongeza Simba ilianza kumfuatilia tangu msimu wa 2018/19 na kilichokuwa kikikwamisha usajili ni Lusaka Dynamos ilikuwa bado inamhitaji zaidi, lakini baada ya mawasiliano na aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi Simba wakati huo, Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ walikubaliana na msala ukaachwa kwa Mugalu kuamua mwenyewe kucheza Tanzania, kabla ya kukubali dili hilo.


MSIMU WA KWANZA

“Nashukuru Mungu licha ya kuanzia ligi katikati na kukosa michezo mingine ikiwamo ya kimataifa, nilifunga katika michezo ya ligi niliyocheza na kumaliza mfungaji bora namba mbili.”


SIMBA vs AS VITA

Msimu uliopita katika mashindano ya kimataifa Simba walicheza Ligi ya mabingwa Afrika na waliishia robo fainali na katika hatua ya makundi miongoni mwa timu waliyochukua pointi zote ni AS Vita ya DR Congo.

Katika mechi ya Dar es Salaam, ya mzunguko wa pili Simba walishinda mabao 4-1, ila Mugalu hakufunga hata moja na stori kubwa kwake ulikuwa ule mchezo wa kwanza kule Kinshasa DR Congo. Anasema mara zote anapokutana na Kocha, Florent Ibenge anatamani kumfunga na amefanya hivyo mara mbili kabla ya kufika Simba na ile ile kuwa awamu ya tatu.

“Si unakumbuka mechi ya kwanza kule DR Congo tuliwafunga AS Vita ya Ibenge bao 1-0, ambalo nilifunga mimi lilikuwa na maana kubwa mno lile bao kutokana na maisha yangu dhidi ya kocha wao,” anasema Mugalu.


MSIMU ULIOPITA

“Binafsi nilifanikiwa malengo yangu kufunga zaidi ya mabao 15 katika mashindano yote na hapo sikuwa na mwanzo mzuri kwa sababu ya majeraha. Pia timu ilichukua mataji mawili makubwa ligi na kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).”


MECHI 15 BILA BAO

Simba wamemaliza michezo 15 ya Ligi Kuu Bara bila huku mastraika wawili, John Bocco na Mugalu ambao walishika nafasi za juu katika msimamo wa ufungaji msimu uliopita lakini hadi sasa hakuna aliyefunga huku akiwa na bao moja alilofunga kwenye ASFC dhidi ya Dar City.

“Katika maisha yangu ya soka hakuna wakati napitia katika maumivu makali na kuumia kama hivi sasa sijawahi kucheza mechi 15, bila kufunga bao lolote kwenye ligi na huu ndio msimu wa kwanza,” anasema Mugalu.