Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Amorim ana madeni matano Manchester United

Muktasari:

  • Mastaa kibao walirejea mazoezini huko Carrington, Jumatatu kwenye siku ya kwanza ya pre-season.

MANCHESTER United inakabiliwa na msimu muhimu kweli na mipango ya hiyo inakwenda vizuri.

Mastaa kibao walirejea mazoezini huko Carrington, Jumatatu kwenye siku ya kwanza ya pre-season.

Na bila ya shaka, kocha Ruben Amorim atakuwa na mastaa wake kwenda kuanza maandalizi ya kuweka sawa baada ya kumaliza msimu vibaya. Na kitu kizuri hata kwenye dirisha la usajili, mambo yanakwenda vizuri. Pauni 62.5 milioni ililipwa kunasa saini ya Matheus Cunha aliponyakuliwa kutoka Wolves - wakati Diego Leon naye akitua na kuwa usajili wa pili kwenye dirisha hili.

Lakini, kazi ya Amorim katika kuijenga upya Man United haiishi hapo. Winga mpya, straika mpya na pengine kipa mpya, atahitajika pia kikosini. Swali, je dili hizo zote zitakamilika kwa wakati?

Umebaki muda usiozidi wiki mbili kabla ya Man United kucheza mechi yake ya kwanza ya kirafiki kwenye pre-season dhidi ya Leeds United, hivyo Amorim atahitaji kuwa na watu wake wote hadi wakati huo.

Kwenye hilo, Kocha Amorim kuna mambo muhimu anayopaswa kuyatatua sasa.


1.Kukamilisha dili la Bryan Mbeumo

Staa wa Brentford, Bryan Mbeumo amekuwa kwenye mipango ya Man United na saini yake inasakwa kwa nguvu zote huko Emirates.

Kwenye vita ya kunasa saini ya mkali huyo, Man United ilichuana vikali na Tottenham, lakini mchezaji Mbeumo anataka kutua Old Trafford.

Ofa zao mbili zimegomewa, lakini Man United inaamini itakamilisha dili la Mbeumo kwa Pauni 65 milioni. Kinachoelezwa ni dili hilo linaweza kukamilika kabla ya mechi za kirafiki za pre-soason kuanza.


2.Kupiga bei mastaa vimeo

Dili la Mbeumo litaifanya Man United kufikisha matumizi ya Pauni 130 milioni kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi, hivyo kuweka mambo sawa itahitaji kuuza mastaa ambao haiwahitaji. Na kwenye hilo kuna orodha ndefu ya wachezaji watakaofunguliwa mlango wa kutokea.

Mastaa waliotolewa kwa mkopo msimu uliopita, Jadon Sancho, Marcus Rashford na Antony wote watakuwa kwenye orodha hiyo ya watakaopigwa bei.

Hivyo, Amorim ana matumaini makubwa atapata timu za kuwasajili wakali hao watatu. Ishu ya kuwauza wachezaji haitaishia kwa hao tu. Kipa Andre Onana anaweza kujikuta akitokea kwa mkopo, huku beki wa kushoto Tyrell Malacia naye anaweza kuonyeshwa mlango wa kutokea baada ya kucheza kwa mkopo PSV msimu uliopita. Jambo hilo linamhusu pia Alejandro Garnacho, anayefukuziwa na Chelsea na Napoli.


3.Kuamua kipa namba moja

Ikizungumziwa wachezaji wa kuondoka, kipa Onana anatajwa kuwa miongoni mwa watakaofunguliwa mlango wa kutokea.

Kipa huyo Mcamerooni amekuwa na makosa mengi misimu ya karibuni tangu aliponaswa kwa pesa nyingi kutoka Inter Milan. Ripoti zinafichua Man United inataka kumtoa kwa mkopo na Monaco inahitaji huduma yake.

Sasa huko Old Trafford, makipa wanaotajwa ni Emi Martinez wa Aston Villa na John Victor wa Botafogo.

Kutokana na hilo, kocha Amorim anapaswa kuamua mapema ni nani atakuwa kipa wake namba moja. Kama ataamua Onana aondoke, basi atahitaji mbadala wake, lakini kama atabaki, Amorim atalazimika kuamua, nani awe namba moja.


4.Kuamua nafasi ya straika

Kama ambavyo Amorim atalazimika kuamua nani awe kipa namba moja, jambo hilo pia litahitajika kwenye nafasi ya ushambuliaji. Cunha na Mbeumo watakuja kuongeza kitu muhimu kwenye fowadi ya Man United, lakini ni nani atakuwa mshambuliaji wa kati.

Kwenye ishu ya mshambuliaji wa kati, Man United imekuwa ikihusishwa na mastraika wengi, akiwamo Viktor Gyokeres, ambaye sasa anaripotiwa anakaribia kujiunga na Arsenal.

Shida nyingine ni kwamba mastraika wanauzwa pesa nyingi na Man United kwa sasa kwa sababu wanabanwa na kanuni, hivyo Amorim anaweza kuwa na imani na straika Rasmus Hojlund. Lakini, uamuzi huo anapaswa kuufanya mapema kabla ya msimu haujaanza.


5.Kuamua nani atoke kwa mkopo

Misimu ya karibuni, Man United imekuwa na mambo mengi mabaya, lakini kuna eneo moja ambalo wamekuwa wakifanya vizuri, akademia ya klabu hiyo, ikiibua mastaa wa maana akiwamo Kobbie Mainoo na Toby Collyer.

Lakini, kitendo cha kushindwa kuwamo kwenye michuano yoyote ya Ulaya msimu ujao, hivyo eneo ambalo wanapaswa kuwatoa makinda wao kwenda kupata uzoefu ni kuwapeleka kwa mkopo.

Dan Gore, Harry Amass na Ethan Wheatley wanahitaji kutolewa kwa mkopo wakapate uzoefu hguko kwingine kabla ya kurudi Emirates kwa ajili ya matumizi ya baadaye.