Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MJUAJI: Maajabu ya Yanga Afrika Mashariki

HAKUNA ubishi, Yanga ndio timu ya kwanza kufika ya robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika (sasa Ligi ya Mabingwa Afrika) kwa timu za Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.

Yanga iliandika historia hiyo mwaka 1969 pale ilipocheza dhidi ya Asante Kotoka ya Ghana rekodi ambayo ilikuja kuvunjwa mwaka 1974 na watani wao wa jadi Simba.

Mwaka huo Simba iliweka rekodi ya kufika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Mehallah el Kubra ya Misri.

Rekodi ya Yanga ilikuja baada ya Tanzania kujiunga rasmi na Chama cha Soka Afrika (AFA) kabla ya kuwa CAF mwaka 1964.

Hadi kufika robo fainali hiyo mwaka 1969, Yanga ilizotoa timu za Fitarikandro ya Madagascar kwa jumla ya mabao 4-3 kisha St George ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 5-0.

Pia, ilirudia tena kutinga robo fainali ya pili mfululizo 1970 na kukwaa kisiki kile kile cha Asante Kotoko ya Ghana baada ya awali kuzing’oa US Fonctionnaires ya Madagascar kwa jumla ya mabao 6-4 na baadaye kuifunga Nakuru All Stars kwa mabao 3-2.

Licha ya rekodi hizo tamu, lakini Yanga bado ina historia ambayo imeifanya timu pekee kunyakua taji nje ya mipaka ya Tanzania.


SIO MARA MOJA

Mwaka 1993, Yanga ilitwaa Kombe la ubingwa wa Afrika Mashariki na ya Kati (Kombe la Kagame) nchini Uganda.

Katika michuano hiyo, Tanzania iliwakilishwa na Simba na Yanga. Mnyama alienda kama bingwa mtetezi wa taji hilo baada ya kulibeba mara mbili mfululizo.

Mwaka 1991 akilibeba baada ya kuifunga Sports Club Villa jijini Dar es Salaam na mwaka 1992 baada ya kuifunga Yanga kwa penalti pale Zanzibar.

Hata hivyo, Simba ilitolewa mapema katika michuano hiyo ya Uganda. Upo?


YANGA KINYONGE

Yanga ilienda Uganda kwa usafiri wa meli ambayo ulionekana kutumiwa na timu isiyokuwa na fedha baada ya wafadhili wake kina Abbas Gulamali, Mohammed Viran, Ramesh Patwa, Murtazar Dewji na Muhsin Hassanali ‘kuisusa’ timu.

Hiyo ilifuatia baada ya klabu hiyo chini ya uongozi wa George Mpondela kutaka kuanzisha Yanga kampuni. Timu ilipanda meli kwa msaada wa Mfanyabiashara Reginald Mengi aliyeokoa jahazi. Wakati Yanga ikipanda meli, Simba ilipanda ndege kwenda Kampala.

Lakini cha ajabu, Yanga ilirudi na ndege na Simba ikarudi na meli hadi Mwanza ambako iliweka kambi ya kucheza mchezo wa Kombe la Caf katika Uwanja wa CCM Kirumba.


MAAJABU YA YANGA

Katika kundi lake Yanga ilikuwa na timu za Sports Club Villa, Malindi ya Zanzibar. Mchezo wa kwanza ilifungwa na Villa mabao 3-1, mchezo wa pili ikaifunga Malindi 2-1 na kutinga nusu fainali na kuitoa Express ya Uganda kwa mabao 3-1 na kutinga fainali.

Yanga ilifanya mambo hayo nchini Uganda baada ya kushinda mchezo wa fainali kwa kuilaza Sports Club Villa mabao 2-1 yaliyofungwa na Edibily Lunyamila na Said Mwamba Kizota. Yanga ilitoka nyuma baada ya kutanguliwa kwa bao la Sports Club Villa la George Akena katika dakika ya nne.

Kizota alisawazisha dakika nne baadaye na Lunyamila akahitimisha shughuli dakika ya 44. Gulamali aliibuka na zawadi ya televisheni kwa wachezaji wa Yanga.

Kwenye mechi ya Mwaka 1999, Yanga ilibeba tena kombe hilo nchini Uganda kwa kuishinda tena SC Villa kwa matuta baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 120. Villa ilitangulia kufunga na Lunyamila akasawazisha bao.


VITU VYA AJABU

Katika mashindano yote hayo, Yanga ilianza vibaya lakini ilimaliza ikiwa mabingwa wa michuano hiyo. Kitu kingine cha kushangaza fainali ya michuano hiyo zote ilishirikisha timu mbili yaani Sports Club Villa ya Uganda na Yanga


KUTANGULIA SI KUFIKA

Yaani SC Villa ilitangulia kufunga katika fainali zote mbili lakini ilijikuta ikichezea vichapo na kupoteza kombe.

Kitu kingine wachezaji wa Yanga, Lunyamila na Kizota waliupiga mwingi katika fainali zote ambapo za mwaka 1993 Kizota alikuwa mshambuliaji wa kati akicheza na Jonas Lunyamila aliyekuwa winga wa kushoto. Wakati Lunyamila akiendelea kucheza nafasi yake katika fainali ya mwaka 1999, Kizota alikuwa beki wa kati wa Yanga.

Yanga iliacha historia kwa kufikia hatua hata baadhi ya wenye mabasi kuyaandika jina la Lunyamila.


SC VILLA FAINALI 3 - 1

Sports Club Villa ilicheza fainali nne za ubingwa wa Afrika Mashariki na ya Kati na timu za Tanzania. Mwaka 1991 ililikosa kombe hilo jijini Dar baada ya kuchapwa 3-0 na Simba kwa mabao ya Zamoyoni Mogella na Hassan Afif kocha mchezaji aliyeasisti kwa Golden Boy kabla ya mwenyewe kutupia nyavuni.

Januari 30, 1993 ilicheza fainali na Yanga na kukosa kombe kwa kulala 2-1 katika fainali na mwaka 1999 ililikosa kombe tena katika uwanja wa nyumbani wa Nakivubo. Mwaka 1993 ikifungwa ndani ya dakika 90 na mwaka 1999 ikifungwa tena na Yanga kwa matuta 4-1 baada ya kumaliza dakika 90 zikiwa zimefunga bao 1-1.


2003 IKAMGOMEA MNYAMA

Mwaka 2003 Sports Club Villa ilifika tena fainali , lakini safari hii ikagoma kuruhusu kombe hilo kuondoka Kampala, ilimvimbia Mnyama na kubeba kombe hilo kwa kuifunga Simba bao 1-0 Uwanja wa Nakivubo jijini Kampala Uganda. . Hapa ndipo ilipogundulika Villa ilikuwa na kiungo mmoja matata sana raia wa Tanzania, Shaban Kisiga ‘Malone’.