Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MEZA YA UFUNDI: Tunahitaji sura mpya zaidi Taifa Stars

Muktasari:

  • Ni rahisi kumwita Mponda na Mussa kwa kuwa ni mastraika na wanafunga  kila mara, lakini ni vigumu kumwita Dilunga, Kenny kwa sababu takwimu zao hazilinganishwi

TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inajiandaa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe, The Mighty Warriors’ kesho Jumapili mjini Harare, ambao unaotambuliwa na kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (Fifa). Pambano hilo ni muhimu katika kudhibiti viwango vya Fifa zaidi ya matokeo uwanjani hasa ya kupoteza mchezo, ndio maana Kocha Mkuu wa Stars, Boniface Mkwasa ameamua kuwaita wachezaji karibuni wote aliokuwa akiwaita siku za nyuma ukimuondoa Kelvin Yondani.

Kikosi hicho pia kimeongezewa nyota wachache mno ambao ni sura mpya zikiwa ambao ni Omary Mponda anayekipiga Ndanda, Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting na Ismail Michael wa Prisons Mbeya. Hakuna makosa ya kiufundi katika kuchagua kikosi hicho kwani, bado wengi walioitwa kikosini ni vijana wenye muda mrefu wa kulitumikia Taifa, pia bado ni rahisi na itaendelea kuwa rahisi kuwachagua wengine wanaocheza katika timu za Azam, Simba na Yanga kwa sababu nimewahi kueleza ubora wa timu hizo unavyowabeba wachezai wengi wanaojiunga nazo. Nani alikuwa anamjua vizuri Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya ama Mzamiru Yassin walipokuwa Mtibwa Sugar? Ni macho ya wachache waliopo Simba na kocha aliyewatengeneza Manungu, Mecky Mexime ndio waliokuwa wakijua ubora wao uwanjani.

Hakuna mtu aliyekuwa akimjua vizuri Juma Mahadhi na Andrew Vincent wakati wakizichezea Coastal Union na Mtibwa? Lakini baada ya kujiunga na Yanga, timu yenye mkusanyiko wa nyota wa ndani na nje ya nchi walio na ubora tofauti kila mtu anaweza kuwaona vizuri kwa sasa. Hata kama Kocha Mkwasa atatembea mikoa yote huko kuhudhuria michezo kati ya Toto na Mwadui, Prisons na Kagera bado hawezi kuona ubora wa mchezo wenyewe, hivyo kuona ubora wa wachezaji husika mpaka watakapoonyesha ubora wao pale hasa wanapokutana na wachezaji wengine bora hasa waliopo katika vikosi vya Yanga, Simba na Azam FC. Pamoja na urahisi huo, lakini bado Mkwasa anaweza kuanza kulinganisha takwimu chache kwa baadhi ya wachezaji wake wengi wanaoitwa mara nyingi kwenye kikosi hicho kama kina Himid Mao, Mudathir Yahya, Aggrey Morris, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Simon Msuva na wengineo wengi ambao wako vizuri.

Ni rahisi kumwita Mponda na Mussa kwa sababu ni washambuliaji na unawaona wakifunga kila mara, lakini inakuwa vigumu kumwita Hassan Dilunga, Kenny Ali na Rafael Daudi kwa sababu takwimu zao hazilinganishwi mara nyingi. Lakini, bado unaweza kumuona jinsi Dilunga alivyobadilika kwa sasa, kwenye mchezo wao uliowakutanisha Azam dhidi ya Ruvu Shooting pale Chamazi hakuna ubishi nyota ya mchezo ule pengine angeweza kuwa Dilunga.

Akicheza mbele ya viungo hao wa timu ya Taifa, Himid, Mudathir na wenzao kina Salum Abubakar, Frank Domayo ambao ni viungo wa kimataifa, bado Dilunga alikuwa bora mara kadhaa zaidi yao huku akipiga mashuti mengi langoni mwa Azam. Alitengeneza pasi nyingi za mwisho kwa washambuliaji wake na kucheza kwa uwezo mkubwa kitu ambacho tayari ni takwimu zinazoweza kumbeba. Ukimlinganisha Daudi na magoli yake manne kama kiungo tena akiyafunga kwa mashuti mazuri ya mbali, huku akitoa pasi za hatari kwa wafungaji wake unaweza kuona ni aina gani ya mchezaji anayehitajika ndani ya kikosi cha Taifa Stars. Wanayoyafanya kina Kenny Ali, Daudi na wenzao ambao hawako Taifa Stars huwezi kuyaona wakiyafanya kina Mkude, Himid labda tofauti ni zile pasi za maonyesho zinazopigwa pembeni au ule ukabaji wa kibabe na nguvu nyingi, lakini bado katika nafasi za viungo wa kati wanafanya mambo mengi kwa timu. Unataka nini kama sio mabao ya aina hiyo waliyokuwa wakifunga nyota wetu wa zamani kina Salvatory Edward, Yusuf Macho, Athuman Idd ama kina Hamis Gaga, Juma Mkambi na  wengine huko nyuma. Tunahitaji jicho gani la ziada kuwaona vijana hawa ambao kwenye michezo mingi mikubwa dhidi ya Simba, Yanga na Azam wameendelea kuyafanya haya? Tunaendelea kuwaita kina Mudathir kwa takwimu gani wanazoweza kuwazidi viungo wengine kwa sasa kama kina Daud na wenzake? Ni mtazamo tu lakini!