Mastaa wapya waongeza warembo EPL

New Content Item (1)
New Content Item (1)

LONDON, ENGLAND. DIRISHA la usajili limefungwa na tumewaona mastaa ambao wamesajiliwa kwenda timu katika January mwaka huu. Lakini mbali ya usajili wa wachezaji pia kuna usajili mwingine wa nje ya uwanja ambao umefanywa.
Huu ni ule wa wanawake warembo wenye uhusiano wa kimapenzi na wachezaji hao waliosajiliwa katika dirisha hili. Hawa hapa ni baadhi ya wachumba wa wachezaji waliosajiliwa katika dirisha hili ambao nao watakuwa nchini England.

Claudia Kowalczyk
 Claudia, 30, yupo kwenuye uhusiano  wa kimapenzi na staa wa  Arsenal  Jakub Kiwior. Kowalczyk yeye ni densa wa  twerker na aliwahi kushinda tuzo ya malkia wa  twerker -mwaka 2017 katika mashindano yaliyofanyika nchini Ujerumani, Vilevile alifika hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Ulaya mwaka  2018.
Alionekana akiwa sambamba na Kiwior jukwaani wakati Arsenal inaibamiza mabao 3-2.

Katja Kuhne
Umri wake wa miaka 36 hauendani na umri wa mpenzi wake ambaye ni kiungo mpya wa Manchester United Marcel Sabitzer mwenye miaka 28.

Mrembo huyu kutoka Ukraine anafanya kazi kama mtangazaji wa kipindi cha  TV cha The Bachelor, pia anamiliki kampuni yake ya mavazi ambayo huwa inavalisha madensa.
Waliingia kwenye uhusiano mwaka 2017 na wakavalishana pete miaka mitatu baadaye kwenye visiwa vya  Maldives.
Hadi sasa wana mtoto mmoja ambaye ni wakike aliyezaliwa mwaka  2019. Mtoto huyo anaitwa Mary Lou.

Andrea Salas
Huyu ni raia wa Costa Rican na anafanya kazi kama muogeleaji na mwana mitindo.
Vilevile aliwahi kuchukua taji la  Miss Hawaiian Tropic mwaka 2006.
Alifunga ndoa na golikipa wa sasa wa  Nottingham Forest  Keylor Navas mwaka 2009 na hadi sasa wamefanikiwa kupata watoto wawili ambao wote ni wakiume  Mateo na Thiago.

Valentina Cervantes
Cervantes, 22, kwa sasa huenda anajisifia kwamba mpenzi wake ndio mchezaji ghali zaidi nchini England.
Ndio huyu kwa sasa yupo kwenye uhusiano na mchezaji mpya wa Chelsea Enzo Fernandez  ambaye alianza kutoka naye mwaka 2019 na wakafanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza mwaka 2020, wakike aitwaye Olivia. Valentina alikuwa akifanya kazi kama mwalimu wa Kiingereza huko Ureno.

Noa van der Bij
Wakati Cody Gakpo anahama kutoka Uholanzi kwenda nchini England katika msafara wake alikuwepo pia mrembo huyu.
Noa ni muajiriwa wa kampuni ya mitindo ya Cachet Models aliyojiunga nato mara tu baada ya kumaliza masomo yake ya  Management katika chuo kikuu cha Avans University of Applied Sciences.
Kwa sasa ana umri wa miaka 23 na kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamoii wa Instagram ana wafuasi 17,000.
Naye pia anapenda kweli kweli kula bata kwani kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Insta amekuwa akitupia picha zinazomuonyesha yupo kwenye maeneo mbali mbali ya starehe.

Liberty Litchfield
Anafanya kazi kama nesi wa magonjwa ya akili, huyu ni mchumba wa mchezaji mpya wa Leicester City , Harry Souttar.
Ni miongoni mwa watu wanaopenda sana starehe, amekuwa akionekana kwenye fukwe mbali mbali akila maisha sambamba na matamasha mbali mbali.
Pia anaonekana kuwa ni mtu wa fasheni sana kwani mitupio yake ya sio yakitoto.

Angelina Zabarnyi
Huyu ni mrembo mwingine kutoka Ukraine, kwa sasa yupo kwenye uhusiano na mchezaji mpya wa Bournemouth  Illya Zabarnyi, wapenda nao hawa wapo kwenye uhusiano kwa mwaka wa tatu sasa, Mrembo huyu alisoma masuala ya philology katika chuo kikuu cha  Kyiv University.