Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

MASON; Dogo bingwa wa dunia mwenye ngumi za 'chuma'

NGUMI Pict

Muktasari:

  • Dogo Abdullah anatisha zaidi na kwa sasa ndiye bingwa wa dunia wa uzito wa WBO Lightweight alioutwaa mwezi huu.

ALIZALIWA Aprili 5, 2004 katika jiji dogo la Bedford, Ohio, Marekani. Lakini unaposoma hapa miaka 21 ya uhai wake duniani imetosha kushinda mapambano 20 aliyopigana, akishinda 17 kwa knockout huku matatu tu akitoka sare.

Dogo Abdullah anatisha zaidi na kwa sasa ndiye bingwa wa dunia wa uzito wa WBO Lightweight alioutwaa mwezi huu.

Mason ni mmoja wa ndugu watano wa familia moja pamoja na Amir, Adel, Abdur-Rahman na Ibrahim wote kutoka Cleveland ambao wanafundishwa ngumi na baba yao Valiant Mason.

Katika pambano lake la kwanza la ubingwa wa dunia, Novemba 22, mwaka huu, Mason alikabiliana na bondia ambaye hakuwa amepoteza pambano, Sam Noakes kuwania ubingwa wa WBO Lightweight uliokuwa wazi.

Katika pambano hilo lililopigwa kwenye Uwanja wa ANB huko Riyadh, Saudi Arabia alishinda kwa uamuzi wa pamoja wa majaji ambao walitoa pointi 115–113, 115–113 na 117–111. Ushindi huo ulimfanya Mason kuwa bingwa wa dunia mdogo zaidi akiwa na umri wa miaka 21.

NGUM 01

Kabla ya kipigo Noakes alikuwa amepigana mapambano 17 akishinda yote huku akilambisha watu mchanga kwa knockout mara 15. Lakini mbele ya Mason alikaa, na inaelezwa kwa pointi nyingi ingawa uamuzi wa majaji ulitaka kulifanya pambano hilo kuonekana kuwa walitofautiana kwa alama chache.

Mkali huyo wa ndondi anakuwa bingwa wa dunia mdogo zaidi aliye hai katika pambano kali linaloweza kuwa la mwaka.

Mike 'Iron' Tyson aliyezaliwa Juni 30, 1966, Brooklyn, New York, Marekani ni bondia wa Marekani ambaye akiwa na umri wa miaka 20 aliwahi kuwa bingwa wa ngumi za uzito wa juu (heavyweight) katika historia.

Tyson alimchapa Trevor Berbick mwenye umri wa miaka 33 kwa dakika tano na sekunde 35, na kuwa mmiliki wa taji akiwa kijana zaidi katika historia ya uzito wa juu.

NGUM 02

Baada ya pambano hilo, Tyson alimwambia meneja wake, “mimi ndiye bingwa wa uzito wa juu kijana zaidi katika historia, na nitakuwa nzee zaidi.”

Hata hivyo, mafanikio yake ulingoni mara nyingi yalifunikwa na maisha binafsi yenye misukosuko na matatizo mengi.

Bondia wa uzito wa juu, Muingereza Moses Itauma mwenye rekodi ya kushinda mapambano 11, tisa ikiwa ni kwa knockout ana umri wa miaka 19 na anaonekana yupo kwenye njia ya kuvunja rekodi ya Tyson.

NGUM 03

Kuanzia 16 Agosti 2025, matarajio yamekuwa makubwa kuwa Itauma anaweza kuwa bingwa wa uzito wa juu mdogo zaidi katika historia, endapo ataendelea kushinda na kupata nafasi ya kupigania taji, lakini kwa sasa rekodi za Mason zinamkalisha kwa wingi wa mapambano.

Kwa Mason rekodi za dunia hivi sasa zinamtaja kuwa ndiye kijana mdogo zaidi licha ya kwamba ana mwaka mmoja zaidi ya Tyson, lakini ukweli unabakia kuwa ngumi za dogo huyo zimeanza kuonyesha wingu jeupe mbele ya safari yake katika masumbwi.

Licha ya kwamba pambano lililopa taji lilikuwa kwenye 'undercard' ya pambano kuu kati ya David Benavidez dhidi ya Anthony Yarde, ubora wa mpinzani wake, Noakes ambaye alikuwa hajawahi kupoteza ni wa kipekee.

NGUM 04

Noakes alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kubeba ubingwa lightweight ulio chini ya WBO, ikizingatiwa kwamba ni mkubwa kiumri, lakini pia anatumia akili zaidi katika kupigana ulingoni.

Hata hivyo, ngumi nzito za dogo mwenye uzito wa kilo 72, zilimjeruhi Noakes na kulifanya pambano baina yako kuwa lililokuwa la kikatili, likijaa damu na ustadi wa hali ya juu uliowasimamisha mashabiki muda mwingi kushangilia hususan wakati Mason akimpelekea moto mpinzani wake.

Kwa mashabiki wa ngumi wa Uarabuni wanalitaja kuwa moja ya mapambano bora ya mwaka huu. Kwa wachambuzi wa ndondi duniani haikuwa ajabu kwamba dogo angefanya yake, kwani amekuwa akitajwa kuwa na kasi muda wote wa pambano na pia ubora katika ukwepaji masumbwi ya wapinzani wake.

NGUM 05

NINI KILITOKEA?

Noakes, mkali wa KO ambaye hakuwa amepoteza pambano alikuwa anatafuta kuboresha rekodi alikuwa anazichapa katika pambano lake la kwanza la raundi 12, na alianza kwa raundi ya kuvutia. Noakes alijaribu kumrudisha Mason nyuma mapema katika raundi ya pili, lakini Mmarekani huyo alimsogeza ukutani mwa kamba za ulingo na kumfumua vilivyo usoni.

Makonde ya kushoto aliyopiga kwa wakati Mason kwenye raundi ya tatu yalimsababishia kuvuja damu jichoni Noakes, lakini baadaye ilielezwa kwamba hali hiyo iliyokana na kugongana vichwa; na pambano liliendelea, huku jeraha dogo pia likionekana kichwani kwa Mason.

Ingawa raundi ya tano Noakes aliibuka na kusukuma makonde flani ya mopto, lakini dogo Mason alihimili kabla ya kumgeuzia kibao 'kaka yake' na kumchapa mfululizo mwisho wa raundi, na kisha kutawala iliyofuata.

Noakes alikuwa na raundi ya saba bora baada ya makonde mawili makali, lakini dogo alikomaa kupambana kwa ujasiri akiongeza kasi katika raundi ya nane na kumrudisha nyuma Noakes akimfanya ajilinde huku makonde mazito yakimwingia.

Raundi ya kumi ilikuwa ya kusisimua ikishuhudia wote wakipiga ngumi nzito, na Mason alimshtua Noakes mwishoni mwa raundi. Kwa mshangao wa wengi, Noakes alisimama na hakudondoka, na pambano likaingia kwenye raundi muhimu za ubingwa. Hata muda raundi zilizofuata dogo alikuwa yuleyule, spidi ileile, ubora na umahiri pia vilibaki kuwa vilevile.