Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man City ilivyonufaika kwa utata wa VAR Ligi Kuu England

MAN CITY Pict

Muktasari:

  • Man City imenufaika na matukio matatu ya kiutata ya VAR katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo kwenye mechi za Ligi Kuu England.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER City inabebwa? Swali gumu, lakini kwa namna ya mambo yaliyotokea kwa zaidi ya mara tatu majibu yake yanaweza kujibainisha bayana.

Man City imenufaika na matukio matatu ya kiutata ya VAR katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo kwenye mechi za Ligi Kuu England.

Kikosi hicho cha kocha Pep Guardiola kilinufaika kwa msaada huo wa uamuzi wa kutumia video katika mechi ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Liverpool uwanjani Etihad, Jumapili.

Ilikuwaje? Man City ilikuwa mbele kwa bao 1-0 wakati beki wa kati wa Liverpool, Virgil van Dijk alipofunga kwa kichwa kuisawazishia miamba hiyo ya Anfield.

MAN 01

Hata hivyo, bao lake lilikataliwa na VAR kwa madai ya kwamba kulikuwa na kuotea.

Wakati anafunga, Van Dijk hakuwa kwenye eneo la kuotea, lakini mchezaji mwenzake Andy Robertson ndiye aliyekuwa kwenye eneo la kuotea. Beki huyo wa kushoto alisimama kwenye eneo ambalo mpira wa kichwa wa Van Dijk ulipita hapo wakati unakwenda kwenye nyavu za Man City.

Licha ya kwamba Robertson hakugusa mpira huo uliozama nyavuni, lakini VAR ililifuta bao hilo kwa sababu mahali alipokuwa alionekana kuingilia mchezo, kwa sababu aliinama kupisha mpira na hivyo kumfanya kipa Gianluigi Donnarumma afungwe.

Kukataliwa kwa bao hilo la Liverpool kulimfanya kocha Arne Slot kukasirisha na kuonyesha hilo bayana baada ya filimbi ya mwisho ya mchezo.

MAN 02

Kocha Slot alimnyooshea kidole refa Chris Kavanagh kwa sababu aliruhusu bao kama hilo ilipofunga Man City msimu uliopita kwenye mechi dhidi ya Wolves.

Mpira wa kichwa wa John Stones uliisaidia Man City kufunga bao la ushindi dhidi ya Wolves kwenye dakika za majeruhi msimu uliopita.

Bao hilo lilikubalika baada ya kurudia picha zake kwenye VAR kwa muda mrefu. Katika mechi hiyo, kiungo wa Man City, Bernardo Silva, aliyekuwa kwenye eneo la kuotea, alifanya kama ambacho amefanya Robertson, aliinama kupisha mpira na kumpoteza kipa Jose Sa, lakini bao lilikubalika na Man City ikatoka uwanjani kwa ushindi dhidi ya Wolves.

MAN 03

Ukirudi mwaka mwingine nyuma, chama hilo la Guardiola lilinufaika kwenye tukio jingine la aina hiyo.

Nathan Ake alifunga bao la ushindi dhidi ya Fulham, Septemba 2023, jambo lililowaacha Cottagers kwenye hasira kubwa.

Malalamiko ya Fulham ni kwamba Manuel Akanji aliingilia mchezo alipojaribu kuucheza mpira wakati akiwa kwenye eneo la kuotea.

Lakini, VAR iliamua isiingilia uamuzi wa mwamuzi wa kati Michael Oliver, aliyeamua kuwa bao hilo la Ake likubalike.

MAN 04

Slot hakuwa kwenye kuelewa kabisa uamuzi wa kukataliwa kwa bao la timu yake ya Liverpool, Jumapili iliyopita, aliposema: “Ni ngumu kwangu kutolea maoni lile tukio. Nadhani ni dhahiri kabisa ulikuwa uamuzi wa hovyo, walau huo unaweza kuwa uamuzi wangu.

“Kwanini nafikiria hivyo? Kwa sababu Robertson hakuingilia mchezo kwa maana ya kumzuia kipa asifanye alichotaka kufanya. Baada ya mechi, nilionyeshwa lile bao na kwamba alikuwa mwamuzi yuleyule aliyewahi kulikubali bao la Man City dhidi ya Wolves msimu uliopita.

MAN 05

“Ilimchukua mwamuzi wa pembeni sekunde 13 kunyoosha kibendera juu kwamba kuna tukio la kuotea. Hivyo, unaona wazi kabisa kulikuwa na mawasiliano.

“Lakini, kama nilivyosema, ile ingeweza kurudisha mchezoni, kwa sababu kipindi cha kwanza tulikuwa hovyo sana.”