Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo 10 ya kufanya kabla hujashika simu

UREMBO Pict

Muktasari:

  • Ukweli ni kwamba, urembo hauanzi kwenye kopo la krimu. Mara nyingi huanzia kwenye tabia ndogo unazofanya kila asubuhi. Wataalamu wa afya wanasema ukianza siku kwa mtindo mzuri wa maisha, si mwili pekee unaonufaika, hata ngozi yako huonekana yenye afya na kuvutia.

JAMANI, kuna watu wanaamka asubuhi halafu kitu cha kwanza kushika ni simu. Dakika 30 zimeisha kwenye mitandao ya kijamii, kifungua kinywa hakijaliwa, maji hajanywa, hata uso haujaoshwa. Jioni akiona uso umechoka au mwili hauna nguvu, anaanza kulaumu bidhaa za urembo.

Ukweli ni kwamba, urembo hauanzi kwenye kopo la krimu. Mara nyingi huanzia kwenye tabia ndogo unazofanya kila asubuhi. Wataalamu wa afya wanasema ukianza siku kwa mtindo mzuri wa maisha, si mwili pekee unaonufaika, hata ngozi yako huonekana yenye afya na kuvutia.

URE 01

ANZA SIKU KWA KUNYWA MAJI

Baada ya kulala usiku kucha, mwili huwa umekaa muda mrefu bila kupata maji. Kunywa glasi moja au mbili za maji mara tu unapoamka husaidia kuupa mwili nguvu ya kuanza siku.

Daktari bingwa wa lishe, Dk. Neema Mushi anasema watu wengi hutumia fedha nyingi kununua bidhaa za urembo, lakini husahau jambo rahisi kama kunywa maji ya kutosha.

“Maji husaidia mwili kufanya kazi vizuri na ngozi hubaki na unyevunyevu wake wa asili,” anasema.


OSHA USO

Unapoamka, osha uso kwa maji safi au sabuni laini inayofaa ngozi yako. Epuka kutumia maji ya moto sana kwa sababu yanaweza kufanya ngozi ikauke.

Kusafisha uso kila asubuhi huondoa uchafu na mafuta yaliyokusanyika usiku.

URE 02

KULA VIZURI ASUBUHI

Usiondoke nyumbani ukiwa na tumbo tupu kila siku. Kula mayai, matunda, uji wa lishe au vyakula vingine vyenye virutubisho muhimu.

Kifungua kinywa kizuri huupa mwili nguvu na husaidia ngozi kupata virutubisho vinavyohitaji ili ibaki yenye afya.


JILINDE DHIDI YA JUA

Hata kama huendi ufukweni, jua linaweza kuathiri ngozi yako. Kupaka mafuta ya kujikinga na jua kabla ya kutoka nyumbani kunaweza kusaidia kulinda ngozi.

Daktari wa ngozi, Dk. Asha Kweka anasema kujikinga na jua kila siku ni moja ya njia bora za kuhifadhi afya ya ngozi.

“Miale mikali ya jua inaweza kuharibu ngozi taratibu bila mtu kutambua. Ndiyo maana ni muhimu kuilinda kila siku,” anasema.

URE 05

FANYA MAZOEZI HATA KIDOGO TU

Si lazima kwenda ‘gym’ kufanya mazoezi kila siku. Unaweza kutembea kwa kasi, kuruka kamba au kufanya mazoezi mepesi nyumbani kwa dakika 15 hadi 30.

Mazoezi husaidia damu kuzunguka vizuri mwilini, jambo linalochangia mwili kuwa na nguvu na ngozi kuonekana yenye afya.

URE 03

LAINISHA NGOZI

Baada ya kuosha uso, paka mafuta ya kulainisha ngozi. Hii husaidia ngozi kubaki laini na isikauke.

Chagua mafuta yanayokufaa kulingana na aina ya ngozi yako, kwenye eneo hili ni bora uwaulize wataalamu ni aina gani ya kipako unatakiwa kutumia ili usiharibu uso wako ukashindwa kuonekana vizuri au hata kupata chunusi.


PUNGUZA MAKASIRIKO

Usianze siku kwa hasira au mawazo mengi. Tenga dakika chache kusali, kutafakari au kupanga shughuli zako za siku.

Utulivu wa akili unaweza kusaidia kupunguza msongo wa mawazo ambao kwa baadhi ya watu huathiri hata afya ya ngozi.


PUNGUZA MUDA WA KUSHIKA SIMU UNAPOAMKA

Watu wengi huanza siku kwa kutumia simu kwa muda mrefu. Hali hiyo huwafanya wasahau kunywa maji, kula kifungua kinywa au kujiandaa vizuri.

Ni vizuri kuanza kwanza na mahitaji muhimu ya mwili kabla ya kutumia muda mwingi kwenye simu.

URE 04

LALA VIZURI

Afya nzuri huanza na usingizi mzuri. Ukilala saa zinazotosha, utaamka ukiwa na nguvu na ngozi yako pia itaonekana yenye afya.

Kukosa usingizi mara kwa mara kunaweza kufanya uso uonekane umechoka.


FANYA KILA SIKU

Usitarajie matokeo kwa siku moja. Ukiendelea kufanya tabia hizi kila siku, mwili na ngozi vitaanza kuonyesha mabadiliko mazuri kadiri muda unavyopita.

Urembo wa kweli haupatikani kwa vipodozi pekee. Hutokana pia na jinsi unavyoujali mwili wako kila siku.

Anza kubadili tabia zako za asubuhi, kula vizuri, kunywa maji ya kutosha, kufanya mazoezi na kupata usingizi wa kutosha. Hata bila kutumia bidhaa za gharama kubwa, unaweza kuwa na ngozi yenye afya na mwili wenye nguvu.