KWAKO KASHASHA: Mawinga hawa ni moto mkali Ligi Kuu Bara

KATIKA mpira wa kisasa (modern football), wachezaji wa mstari wa mbele ukiondoa wachezaji wawili wa kati ambao hucheza namba tisa na kumi, hao wengine ni viungo.

Kwenye ligi ya Tanzania wachezaji wengi wamejitahidi kufanya vizuri msimu huu kulingana na mifumo ya timu wanazochezea.

Wako wachezaji wa pembeni ama wide midfielders ambao wameonekana kufanya vizuri kuliko wengine na wanne kati yao ni wafuatao.

Wa kwanza ni Luis Miquissone. Ni versatile player. Anaweza kucheza popote akawa na madhara.

Ni mchezaji mwenye football intelligence na by nature ni talented. Mchezaji ambaye mahali popote anaweza kuingia mahali popote. Ana fine physical qualities. Ana uwezo wa kufanya chochote katika eneo lolote na mazingira yoyote.

Ni mchezaji ambaye ana uthubutu. Sio mwoga na haangalii jina wala ukubwa wa mchezaji au timu. Anachokifanya ni kuangalia timu yake. Ana high acceleration na tactical knowledge.

Mchezaji ambaye ana uwezo mkubwa wa kupiga miguu yote ndio maana amekuwa n msaada katika kufunga mabao. Lakini pia ni mfungaji na ndio maana walinzi wamekuwa wakipata tabu kumkabili Miquissone.

Pia ni mtu mwenye msaada. Ni mzuri kwenye majukumu ya kukaba, kusaidia ulinzi na kutengeneza mashambulizi na kufunga.

Ana nidhamu kubwa. Ni mchezaji ambaye hana matatizo, hana hasira licha ya kukabwa na kuchezewa rafu, hana hasira au emotional stress uwanjani na inamsaidia awe na hii inamsaidia awe na high concentration.

Ni mchezaji mwenye high commitment level. Hapendi wafungwe na anajitolea kwa asilimia 100.

Mchezaji mwingine ni Tuisila Kisinda. Ana sifa ya pekee. Anakimbia mno lakini pia anapenda kucheza na wenzake.

Bahati mbaya Kisinda kazi yake haina wamaliziaji. Anapiga mipira mingi katika eneo la hatari ambayo imekuwa haitumiwi vizuri. Kukosa wamaliziaji kumemfanya akose thamani kubwa.

Ni mfungaji na kwa sababu ya kasi yake anaonekana yuko aggressive. Anajivunia kasi yake.

Ni mchezaji mjanja mjanja na hatulii sehemu moja na ni mchezaji mwenye nidhamu sana. Huwezi mkuta anagombana na waamuzi au wenzake.

Ukiondoa nidhamu ya hali ya juu aliyonayo, pia hana hasira na sio rahisi kutoka mchezoni hata pale wachezaji wa timu pinzani wanapojaribu kumvuruga.

Ana high concentration pale timu yake inapokuwa na mpira na inapokuwa haina mpira. Akili yake muda wote inakuwa katika mchezo.

Sio muoga na ni fighter ana ball control nzuri japo huwa anatumia sana mguu wa kulia.

Anawalazimisha wachezaji wengine waende kama yeye ili waweze kutengeneza nafasi.

Ukiondoa Miquissone na Kisinda, kuna Ayoub Lyanga wa Azam. Mtulivu mpole anaweza kuswitch kulia au kushoto, kote huko anafiti.

Ana kasi, unyumbufu na ana nguvu. Mzuri katika kupiga krosi na anaweza kupiga miguu yote.

Ni mzuri kwenye ufungaji na mipira ya hewani (aerial balls) na ya chini (ground balls) Ni mchezaji anayejua kuziona angles.

Na pia ana nidhamu. Hana tabia chafu. Umakini na utulivu wa hali ya juu. Ana ball control nzuri na ni mzuri katika kusaidia kukaba.

Mchezaji wa mwisho ni Yusuph Mhilu. Ana hamu ya mpira. Anaupenda na anatamani aendelee kucheza commitment yake ni kubwa na anafunga. Ana nidhamu. Hapendi ubishi na ugomvi na refa na anaheshimu refa. Sijawahi kumuona akiwa na tabia ya kubishana na mwamuzi wa mchezo na muda mwingi huwa anafocus na kuhakikisha timu yake inapata ushindi.

Ana ball control na dribbler mzuri. Ni mzuri katika eneo la mwisho na anaweza kuwa na walinzi wawili au watatu na akalazimisha kwenda. Ni mchezaji ambaye bado anakua. Kwa maana hiyo kama atajitunza vyema ana nafasi kubwa ya kufika mbali.


IMEANDIKWA NA ALEX KASHASHA