KWAKO KASHASHA: Hawa ndio mabeki wangu wakali pembeni

Wachezaji wengi wameonyesha kiwango bora msimu huu na kutoa mchango mkubwa kwa timu zao katika Ligi Kuu na mashindano mengine.

Katika kundi hilo huwezi ukawakosa walinzi wa pembeni ambao huwa na majukumu ya kudhibiti mawinga na washambuliaji wa timu pinzani lakini pia kusaidia mashambulizi.

Kwenye kundi hilo wapo wachezaji wanne wa pembeni ambao hapana shaka wameonekana kuwa vizuri pengine kuzidi wenzao.

Nikianza na walinzi wa upande wa kulia, jina la kwanza ni la beki wa Simba, Shomari Kapombe. Ni jina kubwa lililozoeleka katika masikio ya wapenzi wa soka Tanzania.

Mchezaji aliyekuwa katika kiwango bora endelevu kwa muda mrefu pasipo kupungua ubora. Anasaidiwa na nidhamu yake. Sio mchezaji mwenye hekaheka na vituko. Hachezi faulo za makusudi (intended fouls). Sio mchezaji mwenye jaziba. Ni mchezaji muungwana na hilo linatoa ishara kwamba amekuwa hivyo hata akiwa nje ya timu kwani tabia za uwanjani zinaweza kureflect alivyo nje ya uwanja.

Muonekano wa sura wa Kapombe unaonyesha ni mchezaji mwenye haiba nzuri. Yuko smati. Muonekano wa nje na utendaji kazi wake kiwanjani vinaenda sambamba nayuko makini na anachokifanya. Amekuwa ni mchezaji mwandamizi na muhimu (senior and key player)

Ni mzuri katika kuanzisha mashambulizi kutokea pembeni. Ni mwepesi anajua kukaa katika nafasi yake (positional play), anaweza kufunga na anajua kudribo, kupunguza mmoja mmoja akatoa asisti au akafunga yeye mwenyewe.

Mzuri kwenye kupiga krosi kwa wakati unaotakiwa. Yuko focused. Muda wote anaelewa anatakiwa afanye nini kwa wakati gani. Ni mchezaji wa kudumu kwenye kikosi cha Simba. Ana uzoefu wa kutosha kwenye mechi kubwa. Ana uzoefu wa kimataifa kutosha na ana muendelezo kwenye timu ya taifa. Anaionekana anajitunza, anajitambua na anaonekana anaipenda kazi yake.

Mchezaji mwingine bora upande wa beki wa kulia ni Nico Wadada wa Azam FC. Mchezaji huyo wwa kimataifa wa Uganda amekuwa ni mchezaji ambaye amedumu kwenye timu ya Azam kwa kiwango cha juu tangu alipoingia.

Ni mchezaji mwandamizi na muhimu. Ameonekana kuwa msaada mkubwa kwa Azam

Ana kasi, anapunguza, anapiga mashuti na anafunga pia kwa sababu sio mchezaji mchoyo. Anatumia nguvu pale inapobidi lakini ana uwezo wa kupiga vichwa pale inapobidi. Sio mchezaji ambaye amekuwa na matatizo ya kinidhamu. Kadi anazopata ni zile za kawaida.

Sifa nyingine ni mchezaji anayeonekana kuelewa yeye ni mchezaji wa kigeni. Amekuwa na efforts kubwa muda wote. Asipocheza Azam imekuwa ikionekana kupata matatizo upande wa kulia. Ni mwepesi kucope na mchezaji mwingine.

Anapovuka anakuwa ni kiungo mshambuliaji kutokea pembeni.

Upande wa mabeki wa kushoto naanzia kwa David Charles Luhende. Ni jina kongwe katika soka la Tanzania na amepata mafanikio ingawa kwa Tanzania kufanikiwa ni kucheza Simba na Yanga lakini wanaojua hawaangalii ametokea timu gani.

Luhende ni mchezaji mwandamizi na muhimu. amecheza mechi nyingi za Kagera. Anapanda vizuri, mzuri kwenye kupiga krosi na ni dead ball specialist.

Amekuwa pia ni mchezeshaji wa timu na amekuwa mchezaji kiongozi na ni mtulivu. Anaweza kucheza timu yoyote kwenye nchi hii. Sio mchezaji mlalamishi.

Mchezaji mwingine kwenye nafasi ya kushoto ni Mohammed Hussein ‘Zimbwe Junior’. Mchezaji mtulivu, ana behaviour nzuri, commitment yake ni ya hali ya juu na ameweza kuaminiwa akapewa unahodha.

Kwa timu kama Simba kupewa unahodha sio jambo rahisi. Unahiodha lazima uwe na uwezo wa kuwasilisha maoni na maono ya wachezaji. Ni kiungo kati ya wachezaji na benchi la ufundi na viongozi.

Kiwanjani ni mchezaji ambaye anapanda kama wenzake. Ni mwepesi wa kusoma mchezo. anaweza kuoverlap akapiga krosi na akafunga. Anaweza kupiga chenga na ana ball control, calculation na timing nzuri

Kwa ujumla ni mchezaji ambaye anaweza kuipa timu mafanikio kutokana na hulka yake

Ameonyesha utofauti katika kukaba, timu inapioshambuliwa anarudi haraka kukaba nafasi. Ni mchezaji anayeonekana kuwa makini wakati wote na anapenda kufunga. Sio mchezaji anayependa kupoteza mechi.


IMEANDIKWA NA ALEX KASHASHA