Kilichomponza Dabo na wengine 16 Azam FC

Muktasari:

Yousouph Dabo amekuwa mhanga mwingine wa machinjio katili zaidi ya makocha hapa nchini, Azam FC. Katika misimu yake 16 kwenye ligi kuu, Azam FC ‘imechinja’ makocha 17, huku wengine wakienda na kurudi mara kadhaa. Ukijumlisha makocha wakuu na wa muda inafikisha idadi za zaidi ya makocha 20, ambao ndiyo umri wa klabu hiyo.

Pumzi ya Moto inakuletea makocha walioifundisha Azam FC tangu inaanza na sababu za kuondolewa.


ATHUMAN KIKILA 2004-2005

Huyu ndiyo kocha wa kwanza wa Azam FC, wakati iliitwa Mzizima. Azam FC ilianzishwa na wafanyakazi wa kampuni za SSB (Said Salim Bakhresa), wakiongozwa na kiwanda cha kusaga ngano cha Mzizima. Na ndiyo maana timu ilianza kwa jina la Mzizima.

Akiwa mmoja wa waanzilishi wa kiwanda cha Mzizima, Kikila akawa kocha mwaka wa kwanza hadi alipojiweka pembeni.


MOHAMED SEIF 2005-2008

Mfanyakazi mwingine wa kiwandani aliyepokea kijiti cha Kikila. Akiwa kijana aliichukua Mzizima ikiwa haipo katika daraja lolote na akaipandisha hadi Ligi Kuu. Hata mabadiliko ya jina kutoka Mzizima hadi Azam FC yalikuja akiwa kocha.

Baada ya kuipandisha 2008 akaonekana hatoshi kwa kukosa sifaakakaa pembeni kama meneja wa timu.


NEIDER DOS SANTOS                      2008-2009

Kocha wa kwanza wa kigeni. Raia huyo wa Brazil ambaye 2006 alikuja kuifundisha Simba na kuondoka baada ya kuona mazonge. Aliifundisha Azam hadi Machi 2009 alipofukuzwa. Sababu ya kufukuzwa ni kuzidiwa nguvu na wachezaji waandamizi.


SYLVESTER MARSH

2009 (kocha wa muda)

Alikuwa msaidizi wa Dos Santos na kuondoka kwa bosi wake kukampa nafasi ya kumalizia msimu kama kocha wa muda. Mwana Mwanza huyo ambaye sasa ni marehemu aliiongoza Azam hadi mwisho wa msimu na kuinusuru kushuka.


ITAMAR AMORIN 2009-2010

Raia wa Brazil aliyekuja kama kocha wa viungo wa timu ya taifa ya Tanzania chini ya Marcio Maximo na baadaye kuwa kocha wa timu za vijana. Azam FC ikavutiwa naye na kumpa usukani aiongoze 2009/10. Lakini hata hivyo safari yake ilimalizwa baada ya mgogoro wake na Patrice Mafisango. Azam ilienda Dodoma kucheza na Polisi Dodoma,  Oktoba 27, 2010 na kushinda 1-0.

Siku iliyofuata, Azam FC ilitakiwa kuwahi kurudi Dar es Salaam. Basi la timu lilitakiwa kuondoka saa 12:00 asubuhi na muda ulipofika kila mchezaji alikuwa ndani ya basi kasoro Mafisango. Basi likashindwa kuondoka ili kumsubiri, akafuatwa chumbani lakini hakuwepo. Akasubiriwa hadi saa mbili asubuhi ndipo akarudi. Akaingia chumbani, akachukua vitu vyake na kupanda ndani ya basi. Kocha Amorin akamtaka awaombe radhi wachezaji wenzake kwa kuwachelewesha, lakini Mafisango akakataa.

Waliporudi Dar es Salaam, kocha akatoa taarifa kwa viongozi kuwa hamtaki Mafisango. Viongozi hawakukubaliana naye wakataka amsamehe, kocha akasema hawezi, lakini Mafisango akakataa kuomba radhi. Kocha akasema kama haondoki basi ataondoka yeye. Viongozi wakamkubalia, akaandika barua ya kujiuzulu na kusepa.


STEWART HALL 2010-2012

Raia wa Uingereza alikuja kama kocha wa timu ya taifa ya Zanzibar kurithi mikoba ya Souleman Sane, baba mzazi wa Reloy Sane, nyota wa Bayern Munich na Ujerumani.

Hall akadumu hadi 2012 na kitumbua kikaingia mchanga kwenye Kombe la Kagame. Kwenye nusu fainali dhidi ya AS Vita, Mrisho akitokea benchi aliifungia Azam bao la ushindi na baada ya mchezo akaibusu jezi ya Yanga aliyopewa na mashabiki. Kitendo hicho kiliwakera viongozi wa Azam na kumwambia kocha asimpange kwenye fainali. Lakini kocha akakaidi na kumpanga, baada ya fainali akafukuzwa.


BORIS BUNJAK 2012

Raia wa Serbia aliyekuja kurithi mikoba ya Hall, lakini alikaa muda mfupi sana. Alifukuzwa baada ya kipigo cha 3-1 kutoka kwa Simba. Lakini baadaye baadhi ya wachezaji walidaiwa kuihujumu timu wakasimamishwa kupisha uchunguzi. Hata hivyo, uchunguzi wa Takukuru haukuwakuta na hatia, wakasamehewa, lakini kocha hakurudi.


STEWART HALL 2012-2013

Azam waligundua walifanya kosa na kumrudisha Hall baada ya kumtimua Bunjak. Safari hii Hall akaja na programu iliyoleta ubingwa 2013/14 japo hakuumaliza. Kibarua kiliota nyasi Novemba 7, 2013 baada ya mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Mbeya City uliofanyikaAzam Complex na kuisha kwa sare ya 3-3.


JOSEPH OMOG 2013-2015

Azam ikaivamia AS Leopards ya Jamhuri ya Kongo na kumchukua kocha raia wa Cameroon, Joseph Omog ambaye alitoka kuipatia ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CAF. Omog akamalizia mzunguko wa pili wa ligi na kuipatia ubingwa Azam. Huu unabaki kuwa ubingwa pekee wa klabu hiyo. Hata hivyo, kutolewa na El Merreikh ya Sudan kwenye Ligi ya Mabingwa kukamgharimu mshindi huyo wa Afcon 2002 akiwa na Cameroon kama kocha msaidizi.

Azam iliupoteza ushindi wa 2-0 nyumbani na kuruhusu kufungwa 3-0 kwa mabao ya jioni.


GEORGE ‘BEST’ NSIMBE 2015 (KOCHA WA MUDA)

Raia wa Uganda alikuja kama msaidizi wa Omog. Kwa hiyo bosi wake alipoondoka akarithi mikoba kumalizia 2014/15.


STEWART HALL 2015-2016

Kwa mara ya tatu Stewart Hall akarudi tena Chamazi na akaiongoza Azam hadi 2016, wiki chache kabla ya kumalizika kwa msimu. Hall aliondoka baada ya mivutano na mabosi iliyotokana na kutokubaliana nao kwa mambo kadhaa ya uendeshaji.


DENNIS KITAMBI - 2016

(KOCHA WA MUDA)

Kitambi ambaye Azam FC ilimchomoa kutoka Azam TV kama mchambuzi, alienda kuwa msaidizi wa George Nsimbe alipoondoka Omog na akaendelea kubaki hadi alipokuja Hall, naye akamfanywa kuwa msaidizi wake.

Hall alipoondoka akamuachia timu amalizie sehemu ndogo ya msimu iliyobaki, ikiwemo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.


ZEBEN HERNANDEZ 2016-2017

Mhispania aliyeanza kwa ushindi wa Ngao ya Jamii na baadaye kuvuna alama sita kutoka Nyanda za Juu Kusini. Lakini baadaye mambo yalimkataa na matokeo yakayumba kufika Desemba 2016 akafukuzwa.


IDD CHECHE 2017 (MSAIDIZI)

Kuondoka kwa Zeben kukampa nafasi kocha msaidizi wa muda mrefu Idd Nassor Cheche kuiongoza Azam kwenye Kombe la Mapinduzi na kushinda ubingwa. Baada ya mashindano akakaa pembeni.


ARISTICA CIOABA

2017-2018

Raia wa Romania Aristica aliichukua timu katika msimu ambao waandamizi wengi waliondoka kama John Bocco, Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Michael na Shomary Kapombe.

Akaanza kujenga kikosi lakini akashindwa kumaliza, akaondoka wiki chache kabla ya kumalizika 2017/18. Kisa cha kuondoka kilikuwa kwenda kumalizia masomo ya UEFA Pro Licence.


IDD NASSOR 2018

Kocha msaidizi ‘Babu Cheche’ akamalizia msimu uliobaki kwa staili ya aina yake ikiwemo ushindi wa 3-1 dhidi ya Yanga katika mechi ya mwisho ya msimu iliyokutanisha timu zinazowania nafasi ya pili.


HANS PLUIJM - 2018 - 2019

Raia wa Uholanzi aliyelowea Ghana alipata umaarufu mkubwa akiwa Yanga alipoiongoza Yanga kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika huku ikitawala soka la ndani.

Lakini maisha yake Azam  yalikuwa ya kupanda na kushuka na baada ya kichapo cha 3-1 kutoka Simba akatimuliwa.


ABDUL MINGANGE 2019

Akiwa na msaidizi Cheche wawili hao wakaiongoza Azam kumaliza 2018/19 kwa kishindo baada ya kushinda Kombe la Shirikisho la Azam. Hiki kilikuwa kipindi ambacho Manchester United ilikuwa chini ya Ole Gunnar Solskjaar, na Idd Cheche akaitwa Ole Gunnar Cheche kwa sababu ndiye aliyeonekana kinara japo alikuwa msaidizi.


NDAYIRAGIJE 2019

Ettiene Ndayiragije aliyevuma akiwa Mbao na baadaye kutimkia KMC akaichukua Azam kwa ajili ya msimu wa 2019/20.

Hata hivyo raia huyo wa Burundi alifukuzwa mara tu baada ya kutolewa na Triangle ya Zimbabwe kwa vipigo vya 1-0 nje ndani. Bahati yake ni kwamba wakati akiifundisha Azam FC pia alikuwa akiifundisha timu ya taifa, hivyo alipofukuzwa akabaki na timu ya taifa na watu hawakujua kwamba alifukuzwa.


CIOABA 2019-2020

Mwamba kutoka Romania akarudi tena baada ya kukamilisha masomo yake. Akamalizia msimu uliokumbwa na Uviko 19. Msimu mpya wa 2020/21 akauanza kwa kishindo baada ya kushinda mechi saba mfululizo kabla ya kiwango kuanguka ghafla na kutimuliwa kufuatia kipigo cha 1-0 kutoka kwa Yanga.


VIVIER BAHATI 2019 (KOCHA WA MUDA)

Alikuja kama kocha wa utimamu wa mwili chini ya Ndayiragije na baadaye kuwa msaidizi wa Aristica Cioaba baada ya kuondoka kwa Cheche. Akaiongoza Azam mechi mbili za Kanda ya Ziwa dhidi ya Biashara United na Gwambina zote ziliisha kwa sare.


GEORGE LWANDAMINA 2019-2021

Raia huyo wa Zambia aliletwa kuokoa msimu huo ambao licha ya kuyumba lakini Azam ilikuwa kileleni mwa msimamo, shukrani kwa fomu nzuri ya mwanzo wa msimu. Lwandamina akadumu hadi Novemba 2021 alipotimuliwa baada ya kuuanza vibaya msimu wa 2021/22.


ABDIHAMID MOALLIN

2021-2022

Raia wa Marekani mwenye asili ya Somalia, alikuja Tanzania kama mkuu wa maendeleo ya ufundi wa timu za vijana wa Azam baada ya kuvutiwa naye alipokuja na Horseed ya Somalia kucheza na Azam kwenye Kombe la Shirikisho. Alianza vizuri lakini akamalizia msimu kwa kiwango hafifu. Alipouanza msimu mpya wa 2022/23 akafukuzwa baada ya mechi mbili tu kufuatia kiwango kibovu.


MOHAMED  BADRU 2022

Kocha wa vijana wa Azam aliyepewa kuiongoza kwa mechi moja dhidi ya Yanga na kuisha kwa sare ya 2-2.


DENIS LAVAGNE 2022

Kocha Mfaransa aliyekuja kuleta uzoefu ili kuisaidia Azam kupiga hatua. Lakini alifukuzwa baada ya miezi mitatu kufuatia maelewano mabaya na wachezaji kiasi cha kumhujumu.


KALI ONGALA 2022-2023 (KOCHA WA MUDA)

Alirudi Azam 2022 kama kocha wa washambuliaji tangu aondoke 2014 akiwa msaidizi. Akaiongoza Azam hadi Julai 2023 kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports. Kali atakumbukwa kwa kuvunja uteja kwa Simba, timu iliyoitesa Azam FC tangu 2018.


YOUSOUPH DABO 2023-2024

Sasa imekuwa zamu ya Dabo, kocha mtaalamu wa mbinu lakini mwenye kiburi mbele ya wachezaji na mabosi. Baada ya msimu mzuri wa 2023/24 ilitarajiwa 2024/25 ingekuwa bora zaidi, lakini imekuwa kinyume.Tusubiri anayekuja!

Yousouph Dabo amekuwa mhanga mwingine wa machinjio katili zaidi ya makocha hapa nchini, Azam FC. Katika misimu yake 16 kwenye ligi kuu, Azam FC ‘imechinja’ makocha 17, huku wengine wakienda na kurudi mara kadhaa.

Ukijumlisha makocha wakuu na wale wa muda, Azam FC inafikisha idadi za zaidi ya makocha 20, ambao ndiyo umri wa klabu hiyo.

Katika makala hii, tunakuletea makocha wote waliowahi kuifundisha Azam FC tangu inaanza, na sababu za kuondolewa kwao.


ATHUMAN KIKILA 2004-2005

Huyu ndiyo kocha wa kwanza kabisa wa Azam FC, wakati iliitwa Mzizima FC.

Itakumbukwa kuwa Azam FC ilianzishwa na wafanyakazi wa makampuni ya SSB (Said Salim Bakhresa), wakiongozwa na kiwanda cha kusaga ngano cha Mzizima. Na ndiyo maana timu ilianza kwa jina la Mzizima.

Akiwa mmoja wa waanzilishi wa kiwanda cha Mzizima, Kikila akawa kocha kwa mwaka wa kwanza, hadi yeye mwenyewe alipojiweka pembeni kupisha damu changa.


MOHAMED SEIF ‘KING’ 2005-2008

Mfanyakazi mwingine wa kiwandani aliyepokea kijiti cha mzee Kikila. Yeye akiwa kijana mwenye nguvu za kutosha, aliichukua Mzizima FC ikiwa haipo katika daraja lolote na akaipandisha hadi ligi kuu.

Hata mabadiliko ya jina kutoka Mzizima FC hadi Azam FC yalikuja yeye akiwa kocha.

Baada ya kuipandusha timu mwaka 2008, akaonekana hatoshi kwa ligi kuu kutokana na kukosa sifa, ndipo akakaa pembeni kama meneja wa timu.


Santos
Santos

NEIDER DOS SANTOS 2008-2009

Kocha wa kwanza wa kigeni kuifundisha Azam FC. Raia huyo wa Brazil ambaye mwaka 2006 alikuja nchini kuifundisha Simba na kuondoka hapo hapo baada ya kuona mazonge ikiwemo kutangazwa amesaini mkataba ilihali ilikuwa bado, aliifundisha Azam FC hadi Machi 2009 alipofukuzwa.

Sababu ya kufukuzwa kwake ni kuzidiwa nguvu na wachezaji waandamizi wakiongozwa na Shaaban Kisiga ‘Malone’.

Aliondoka baada ya kufungwa 3-0 na Simba katika mchezo uliofanyika siku mbili kutokaka na mvua kubwa kunyesa Dar es Salaam.

Mchezo wa kwanza ulifanyika Machi 29, 2009, na kuvunjika baada ya dakika 45 za kwanza kufuatia mvua kubwa iliyojaza maji uwanja wa Uhuru.

Hadi mechi inavunjika, Simba walikuwa wakiongoza 1-0.

Mechi hiyo ikarudiwa Machi 30, 2009 na Simba kushinda 3-0 huku Cyprian Odura wa Azam FC akiweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kupata kadi nyekundu kwenye ligi kuu.

Baada ya mchezo huu, Dos Santos aliwalaumu wachezaji wake waandamizi akiwemo Kisiga ambaye alimuweka benchi siku hiyo, na kusema wanajiona mastaa ilhali hawajacheza hata fainali moja ya kombe la dunia.

Akasema msimu unaokuja kama atabaki atawatoa wachezaji wote wanaojiona mastaa na kupandisha vijana, akiwataja Himid Mao na Tumba Sued kuwa tegemeo lake lijalo.

Lakini baada ya mchezo huo tu, akafukuzwa.


SYLVESTER MARSH 2009 (kocha wa muda)

Alikuwa msaidizi wa Dos Santos na kuondoka kwa bosi wake kukampa nafasi ya kumalizia msimu kama kocha wa muda.

Mwana Mwanza huyo ambaye sasa ni marehemu aliiongoza Azam FC hadi mwisho wa msimu na kuinusuru kushuka daraja.


ITAMAR AMORIN 2009-2010

Huyu naye alikuwa raia wa Brazil ambaye alikuja kama kocha wa viungo wa timu ya taifa ya Tanzania chini ya Marcio Maximo na baadaye kuwa kocha wa timu za vijana.

Azam FC ikavutiwa naye na kumpa usukani aiongoze timu katika msimu wa 2009/10. Lakini hata hivyo safari yake ilimalizwa baada ya mgogoro wake na Patrice Mutesa Mafisango. Azam FC ilienda Dodoma kucheza na Polisi Dodoma,  Oktoba 27, 2010 na kushinda 1-0 kwa bao la Peter Senyonjo, mchezaji mrefu kuliko goli.

Siku iliyofuata, Azam FC ilitakiwa kuwahi kurudi Dar es Salaam kuendelea na ratiba zingine. Basi la timu lilitakiwa kuondoka saa 12:00 asubuhi, na muda ulipofika kila mchezaji alikuwa ndani ya basi kasoro Patrice Mafisango.

Basi likashindwa kuondoka ili kumsubiri, akafuatwa chumbani kwake lakini hakuwepo. Akasubiriwa hadi saa mbili asubuhi ndipo akarudi akiwa amelewa. Akaingia chumbani kwake, akachukua vitu vyake na kupanda ndani ya basi.

Kocha Amorin akamtaka awaombe radhi wachezaji wenzake kwa kuwachelewesha, lakini Mafisango akakataa.

Waliporudi Dar es Salaam, kocha akatoa taarifa kwa viongozi kuwa hamtaki Mafisango kwenye timu yake.

Viongozi hawakukubaliana naye, wakataka amsamehe, kocha akasema hawezi kumsamehe hadi aombe radhi, lakini Mafisango akakataa kuomba radhi.

Kocha akasema kama Mafisango haondoki basi ataondoka yeye. Viongozi wakamkubalia, akaandika barua ya kujiuzulu na kusepa.


STEWART HALL 2010-2012

Raia huyu wa Uingereza alikuja nchini kama kocha wa timu ya taifa ya Zanzibar kurithi mikoba ya Souleman Sane, baba mzazi wa Reloy Sane, nyota wa Bayern Munich na Ujerumani.

Hall akadumu hadi 2012 na kitumbua chake kikaingia mchanga kwenye mashindano ya Kombe la Kagame.

Kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya AS Vita, Mrisho akitokea benchi, aliifungia Azam FC bao la ushindi na baada ya mchezo akaibusu jezi ya Yanga aliyopewa na mashabiki wa klabu hiyo.

Kitendo hiki kiliwakera viongozi wa Azam FC na kuwambia kocha asimpange mchezaji huyo kwenye fainali.

Lakini kocha akakaidi na kumpanga, baada ya fainali hiyo akafukuzwa kwa kukaidi agizo la wakuu.


BORIS BUNJAK 2012

Raia wa Serbia ambaye alikuja kurithi mikoba ya Hall lakini alikaa muda mfupi sana.

Alifukuzwa baada ya kipigo cha 3-1 kutoka kwa Simba SC.

Lakini baadaye ikabainika kwamba baadhi ya wachezaji waliihujumu timu kwa rushwa, wakasimamishwa kupisha uchunguzi. Wachezaji hao walikuwa nahodha Aggrey Morris, Erasto Nyoni, kipa Deogratius Munishi ‘Dida’ na Said Morad ‘Mweda’. Hata hivyo, uchunguzi wa TAKUKURU haukuwakuta na hatia, wakasamehewa, lakini kocha hakurudi.


STEWART HALL 2012-2013

Azam FC wakagundua kwamba walifanya kosa na kumrudisha Hall baada ya kumtimua Bunjak.

Safari hii Hall akaja na program iliyokuja kuleta ubingwa katika msimu wa 2013/14 japo yeye hakuumaliza.

Kibarua chake kiliota nyasi Novemba 7, 2013 baada tu ya mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa msimu wa 2013/14 dhidi ya Mbeya City uliofanyika Azam Complex na kuisha kwa sare ya 3-3.

Wakuu wa Chamazi hawakufurahishwa na mzunguko wa kwanza wa kusuasua ikiwemo sare ya 0-0 dhidi ya Ashanti, sare ya roho mkononi dhidi ya TZ Prisons Chamazi na zile za ugenini dhidi ya Mtibwa Sugar na Kagera Sugar.


JOSEPH MARIUS OMOG 2013-2015

Azam FC ikaivamia klabu ya AS Leopards ya Jamhuri ya Kongo na kumchukua kocha wao raia wa Cameroon, Joseph Omog ambaye alitoka kuwapatia ubingwa wa Kombe la Shirikisho la CAF. Omog amakamilizia mzunguko wa pili wa ligi ja kuipatia ubingwa Azam FC.

Huu unabaki kuwa ubingwa pekee wa klabu hiyo.

Hata hivyo, kutolewa na El Merreikh ya Sudan kwenye ligi ya mabingwa kukamgharimu mshindi huyo wa AFCON 2002 akiwa na Cameroon kama kocha msaidizi.

Azam FC iliupoteza ushindi wa 2-0 nyumbani na kuruhusu kufungwa 3-0 kwa mabao ya jioni.


GEORGE ‘BEST’ NSIMBE 2015 (Kocha wa muda)

Raia huyu wa Uganda alikuja kama msaidizi wa Omog baada ya kuondoka kwa Kali Ongala. Kwa hiyo bosi wake alipoondoka yeye akarithi mikoba kumalzia msimu wa 2014/15.


STEWART HALL 2015-2016

Kwa mara ya tatu Stewart Hall akarudi tena Chamazi kama kocha mkuu na akaiongoza Azam FC hadi 2016, wiki chache kabla ya kumalizika kwa msimu wa 2015/16.

Hall aliondoka baada ya mivutano na mabosi wake iliyotokana na kutokubakiana nao kwa mambo kadhaa kuhusu uendeshaji wa timu.


DENNIS KITAMBI - 2016 (Kocha wa muda)

Kitambi ambaye Azam FC ilimchomoa kutoka Azam TV kama mchambuzi, alienda kuwa msaidizi wa George Nsimbe alipondoka Omog na akaendelea kubaki klabu hadi alipokuja Hall, naye akamfanya kuwa mdaidizi wake.

Kwa hiyo Hall alipondoka akamuachia timu amalizie sehemu ndogo ya msimu iliyobaki, ikiwemo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports.


ZEBEN HERNANDEZ 2016-2017

Raia huyu wa Hispania alianza kwa ushindi wa ngao ya jamii na baadaye kuvuna alama sita kutoka nyanda za juu kusini, sehemu ambayo huwa ngumu sana. Lakini baadaye mambo yalimkataa na matokeo yakayumba, kufika Disemba 2016 akafukuzwa.


IDD NASSOR CHECHE 2017 (Msaidizi)

Kuondoka kwa Zeben kukampa nafasi kocha msaidizi wa muda mrefu Idd Nassor Cheche kuiongoza Azam FC kwenye kombe la Mapinduzi na kushinda ubingwa.

Baada ya mashindano hayo, akakaa pembeni.


ARISTICA CIOABA 2017-2018

Raia wa Romania, nchi iliyotuletea mabasi ya IKARUS, wakati wa mwalimu. Aristica aliichukua timu katika msimu ambao waandamizi wengi waliondoka, kama John Bocco, Aishi Manula, Erasto Nyoni, Gadiel Michael na Shomary Kapombe.

Akaanza kukijenga upya kikosi lakini akashindwa kumaliza msimu, akaondoka wiki chache kabla ya kumalizika msimu wa 2017/18. Kisa cha kuondoka kilikuwa kwenda kumalizia masomo yake ya UEFA Pro Licence.


IDD NASSOR 'CHECHE' 2018

Kocha msaidizi ‘babu Cheche’ akamalizia msimu uliobaki, tena kwa staili ya aina yake ikiwemo ushindi wa 3-1 dhidi ya Yanga katika mechi ya mwisho ya msimu iliyokutanisha timu zinazowania nafasi ya pili.


HANS VAN DER PLUIJM - 2018 - 2019

Raia huyu wa Uholanzi aliyelowea Ghana, alipata umaarufu mkubwa sana akiwa Yanga pale alipoingoza Yanga kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF huku ikitawala soka la ndani.

Lakini maisha yake Azam FC yalikuwa ya kupanda na kushuka na baada ya kichapo cha 3-1 kutoka Simba, akatimuliwa.


MEJA MSTAAFU ABDUL MINGANGE 2019

Akiwa na msaidizi Idd Cheche ambaye hapo nyuma alikuwa kocha wa muda mara kadhaa, wawili hawa wakaiongoza Azam FC kumalizia msimu wa 2018/19 kwa kishindo baada ya kushinda Kombe la Shirikisho la Azam Sports.

Hiki kilikuwa kipindi ambacho Manchester United ilikuwa chini ya Ole Gunnar Solskjaar, na Idd Cheche akaitwa Ole Gunnar Cheche kwa sababu yeye ndiye aliyeonekana kinara japo alikuwa msaidizi wa Mingange.


ETIENNE NDAYIRAGIJE 2019

Kocha aliyevuma akiwa Mbao FC na baadaye kutimkia KMC, akaichukua Azam FC kwa ajili ya msimu wa 2019/20.

Hata hivyo raia huyo wa Burundi alifukuzwa mara tu baada ya kutolewa na Triangle ya Zimbabwe kwa vipigo vya 1-0 nje ndani. Bahati yake ni kwamba wakati akiifundisha Azam FC pia alikuwa akiifundisha timu ya taifa, hivyo alipofukuzwa akabaki na timu ya taifa na watu hawakujua kwamba alifukuzwa.


ARISTICA CIOABA 2019-2020

Mwamba kutoka Romania akarudi tena mwaka 2019 baada ya kukamilisha masomo yake. Akamalizia msimu huo uliokumbwa na mlipuko wa UVIKO 19. Msimu mpya wa 2020/21 akauanza kwa kishindo baada ya kushinda mechi 7 mfululizo kabla ya kiwango kuanguka ghafla na kutumiwa kufuatia kipigo cha 1-0 kutoka kwa Yanga.


VIVIER BAHATI 2019 (Kocha wa muda)

Alikuja kama kocha wa utimamu wa mwili chini ya Etienne Ndayiragije na baadaye kuwa msaidizi wa Aristica Cioaba baada ya kuondoka kwa babu Cheche. Akaiongoza Azam FC katika mechi mbili za kanda ya ziwa, dhidi ya Biashara United Mara na Gwambina FC…zote ziliisha kwa sare.


GEORGE LWANDAMINA 2019-2021

Maarufu kama Chicken, akifananishwa na George Chicken wa kwenye filamu maarufu ya Marekani, raia huyo wa Zambia aliletwa kuokoa msimu huo ambao licha ya kuyumba lakini Azam FV ilikuwa bado kileleni mwa msimamo, shukrani kwa fomu nzuri ya mwanzo wa msimu. Lwandamina akadumu hadi Novemba 2021 alipotimuliwa baada ya kuuanza vibaya sana msimu wa 2021/22.


ABDIHAMID MOALLIN 2021-2022

Raia wa Marekani mwenye asili ya Somalia, alikuja Tanzania kama mkuu wa maendeleo ya ufundi wa timu za vijana wa Azam FC baada ya kuvutiwa naye alipokuja na Horseed ya Somalia kucheza na Azam FC kwenye Kombe la Shirikisho.

Alianza vizuri lakini akamalizia msimu kwa kiwango hafifu.

Alipouanza msimu mpya wa 2022/23 akafukuzwa baada ya mechi mbili tu kufuatia kiwango kibovu, siyo tu matokeo.


MOHAMED BADRU 2022

Kocha wa vijana wa Azam FC aliyepewa mikoba kuiongoza timu hiyo kwa mechi moja tu dhidi ya Yanga, na kuisha kwa sare ya 2-2.


DENIS LAVAGNE 2022

Kocha mkubwa raia wa Ufaransa aliyekuja kuleta uzoefu wake ili kuisaidia Azam FC kupiga hatua.

Lakini alifikuzwa baada ya miezi mitatu tu kufuatia maelewano yake mabaya na wachezaji kiasi cha kumhujumu.


KALI ONGALA 2022-2023 (Kocha wa muda)

Alirudi Azam FC mwaka 2022 kama kocha wa washambuliaji tangu aondoke mwaka 2014 kama kocha msaidizi.

Akaiongoza Azam FC hadi Julai 2023 kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports. Kali atakumbukwa kwa kuvunja uteja kwa Simba, timu iliyoitesa Azam FC tangu 2018.


YOUSOUPH DABO 2023-2024

Sasa imekuwa zamu ya Dabo, kocha mtaalamu wa mbinu lakini mwenye kiburi mbele ya wachezaji na mabosi wake.

Baada ya msimu mzuri wa 2023/24, ilitarajiwa 2024/25 ingekuwa bora zaidi, lakini imekuwa kinyume.

Tusubiri anayekuja!