Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiafya mashabiki Simba, Arsenal kuna tatizo

DOKTA Pict

Muktasari:

  • Tukianza na klabu ya Simba ya siku ya jumamosi katika mchezo wa klabu Bingwa CAF uliochezwa katika uwanja wa  ya dhidi ya ES Tunis ya nchini Tunisia iliambulia kipigo cha mabao 1-0.

WIKI hii iliyoanza siku tano zilizopita imekuwa ngumu kwa mashabiki wa Arsenal na Simba ya hapa nchini, hii ni kutokana na kupokea kipigo katika michezo yao ya mwanzoni mwa wiki hii.

Tukianza na klabu ya Simba ya siku ya jumamosi katika mchezo wa klabu Bingwa CAF uliochezwa katika uwanja wa  ya dhidi ya ES Tunis ya nchini Tunisia iliambulia kipigo cha mabao 1-0.

Tofauti na Yanga ambao na wamepoteza mchezo Ijumaa iliyopita kwa bao 2-0 dhidi ya Al Ahly lakini matokeo mazuri ya ligi yanawabeba. lakini Simba imekuwa na matokeo mabaya  katika ligi kuu ya bara.

Mechi ya marudiano ya Mashindano hayo ya CAF iliendelea tena hapo jana kwa Simba dhidi ya ES Tunis na Yanga dhidi AL Ahly keshokutwa siku ya jumamosi.

DOK 01

Kwa upande wa kimataifa, klabu ya Arsenal ambayo ipo kileleni katika ligi kuu ya EPL ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani siku ya jumapili ilipokea kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Manchester United.

Kama mnavyojua nchini Tanzania, soka ni mchezo unaopendwa sana na kufuatiliwa. Pata picha hali ya mshabiki anayeshabikia Simba na kule EPL ni shabiki wa Arsenal.

Mtakumbuka mara nyingi mechi hizi kwa Tanzania zinatazamwa katika mabanda maarufu kama spoti Arena za kitaani, klabu, Bar au lounge na majumbani. Utani wakuudhi huwa ni mwingi sana na unaweza kukuzidishia maumivu ya kufungwa.WIKI hii iliyoanza siku tano zilizopita imekuwa ngumu kwa mashabiki wa Arsenal na Simba ya hapa nchini. Hii ni kutokana na kupokea vipigo katika michezo yao ya mwanzoni mwa wiki hii.

Tukianza na klabu ya Simba, siku ya Jumamosi katika mchezo wa Klabu Bingwa Afrika (CAF) uliochezwa ugenini dhidi ya ES Tunis ya Tunisia, iliambulia kipigo cha bao 1-0.

Tofauti na Yanga ambao nao walipoteza mchezo Ijumaa iliyopita kwa bao 2-0 dhidi ya Al Ahly, lakini matokeo mazuri ya ligi yanawabeba, Simba imekuwa na matokeo mabaya katika ligi kuu ya bara.

DOK 02

Mechi za marudiano za mashindano hayo ya CAF ziliendelea tena hapo jana kwa Simba dhidi ya ES Tunis na Yanga dhidi ya Al Ahly keshokutwa, siku ya Jumamosi.

Kwa upande wa kimataifa, klabu ya Arsenal, ambayo ipo kileleni mwa Ligi Kuu ya England (EPL), ilipokea kipigo cha mabao 3-2 dhidi ya Manchester United katika uwanja wake wa nyumbani siku ya Jumapili.

Kama mnavyojua, nchini Tanzania soka ni mchezo unaopendwa sana na kufuatiliwa kwa karibu. Pata picha hali ya mshabiki anayeshabikia Simba, huku upande wa EPL akiwa ni shabiki wa Arsenal.

DOK 03

Mtakumbuka mara nyingi mechi hizi hutazamwa katika mabanda maarufu kama vile Spoti Arena za mitaani, klabu, baa au lounge, pamoja na majumbani. Utani wa kuudhi huwa mwingi sana na unaweza kuzidisha maumivu ya kufungwa.

Tangu kupatikana kwa matokeo hayo mabaya, baadhi ya mashabiki wamepata mgogoro wa kiafya kwa upande wa kiakili na kimwili.

Katika baadhi ya maeneo kama vile baa, baadhi yao walionekana kuwa na hasira na huzuni kali. Walionyesha dalili za mpasuko wa hisia, ikiwamo kukosa furaha, huzuni kali na kuwa katika hali ya ukimya.

Nchini Uingereza katika uwanja wa Emirates maelfu ya mashabiki walionyesha hasira kwa kocha wao Mikel Arteta kwa kumzomea na kumkejeli.

DOK 04

Baadhi ya mashabiki walionekana kumwaga machozi, huku wengine wakiamua kutoka mapema uwanjani kabla ya mpira kuisha, na wengine kubaki wakiwa wamejaa hasira kali. Leo tutaangalia jinsi hali ya kufungwa inavyoweza kuleta mgogoro wa kiafya kwa mashabiki.


WABUGIA KINYWAJI INAKUWAJE?

Kwa kuwa mechi hizi wengi huzitazama wakiwa katika maeneo ya starehe kama vile baa, lounge na klabu, baadhi yao waliamua kubugia pombe nyingi ili kujiondolea msongo wa mawazo wa kufungwa.

Pasipo kujua kuwa kufanya hivyo kuna matokeo hasi kiafya, kwani husababisha mgogoro wa afya ikiwamo kupata uchovu mkali na mning’inio (hangover). Hali hizi huambatana na maumivu ya kichwa na mwili kuumwa.

Wapo ambao walikesha na hatimaye kuharibu ratiba zao za kulala. Hali zote hizo huleta mgogoro wa kiafya siku inayofuata, ambayo ilikuwa ni Jumatatu, siku ya kazi.

Mshabiki aliyepata uchovu na mning’inio ni vigumu kwake kufanya kazi zake kwa utulivu na umakini siku inayofuata. Wengi huelemewa na usingizi na maumivu ya kichwa.

DOK 05

KWANINI USTUMIE PANADOL

Kwa nini ukiamka na mning’inio usitumie paracetamol (panadol)? Mashabiki waliokesha na kunywa pombe kisha kuamka na ‘hangover’ hawapaswi kutumia dawa ya maumivu aina ya paracetamol ili kudhibiti maumivu ya kichwa, kwa kuwa inaweza kusababisha madhara kwenye ini.

Unapokunywa pombe kwa kiasi kikubwa, ini hufanya kazi kubwa kuchakata pombe hiyo. Dawa kama paracetamol inapofika mwilini nayo hulazimika kuchakatwa na ini.

Hali hiyo huongeza mzigo mkubwa kwa ini, hasa ikizingatiwa kuwa siku iliyotangulia lilikuwa limefanya kazi kubwa kuchakata pombe nyingi, hali ambayo huwa mbaya zaidi kama ilikuwa ni pombe kali.

Maumivu ya kichwa husababishwa na unywaji wa pombe kupita kiasi, kupungukiwa na maji mwilini, kukosa usingizi na viambata vilivyomo kwenye pombe.


SHIDA AFYA YA AKILI IKO HAPA

Matokeo mabaya ya kandanda huwapokea vibaya mashabiki kwa sababu ni kitu wanachokipenda sana. Timu kukosa ushindi huwafanya kuwa na hasira, kukosa furaha, huzuni, hofu, kujitenga na kuwa wakimya.

Hali ya kushuka kihisia huwafanya kuwa wepesi kulipuka kwa hasira. Muda mwingi huwa katika hali ya unyong’onyevu na huzuni kali, ambayo ikidumu kwa muda mrefu huweza kuyumbisha afya ya akili.

Baadhi huamua kujitenga na jamii kutokana na hofu ya kusakamwa na utani wa watani wao wa jadi. Mfano ni mashabiki wa Simba wanaokumbana na kejeli kutoka kwa mashabiki wa Yanga, ambao kwa sasa wako vizuri kwenye ligi.

DOK 06

KUKABILIANA NA HASIRA

Tatizo la hasira hujitokeza kwa mashabiki, wachezaji, makocha na hata viongozi wa timu. Pata picha hasira ya kocha wa Arsenal aliyekumbana na zomea-zomea kutoka kwa mashabiki.

Katika vyumba vya kubadilishia nguo, ni kawaida kukuta wachezaji wakipiga au kutupa vifaa kwa hasira. Wengine hulia au kukaripiana kwa jazba.

Makocha nao huweza kufoka na kukemea makosa au uzembe uliosababisha timu kufungwa, hali inayowaacha wachezaji wakiwa na hasira na huzuni.

Moja ya mbinu rahisi za kukabiliana na hasira ni kuepuka au kuwa mbali na chanzo kinachosababisha hasira. Ingawa ni vigumu kwa mashabiki kuacha kuifuatilia timu yao au kuepuka vijiwe vya watani wao.

Kupumua kwa kina, kunyosha viungo vya mwili na kupuuza mawazo yanayopandisha hasira husaidia kupunguza jazba.

Kama hasira itaendelea, zipo mbinu mbalimbali za kuhamisha hisia hizo hasi na kujenga hisia chanya.

Mtu anaweza kufanya shughuli ndogo ndogo, kufanya mazoezi, kutengeneza bustani, kusikiliza muziki au kutazama televisheni, mambo ambayo husaidia kusahaulisha hasira.

Unaweza pia kuacha kuwaza matukio yaliyosababisha timu kufungwa na badala yake kufikiria mechi zijazo.

Zungumza na marafiki wasiokuudhi au wasiopenda kejeli kupita kiasi. Si watani wote hutania vibaya. Kaa kwenye vijiwe vyenye utani wa staha, hali inayosaidia kuondoa maudhi ya moyoni.

Kubadili mazingira kwa kwenda maeneo yenye mandhari nzuri kama ufukweni au sinema pia husaidia. Si lazima kutazama timu yako kila wakati.

Kutazama burudani mbalimbali ikiwamo michezo, muziki, ngoma na maonyesho husaidia kushusha hasira. Vilevile, tazama mechi za timu yako pale inapokuwa inafanya vizuri.

Hata kama wewe ni mtazamaji wa kandanda, ni muhimu kufanya mazoezi ya mwili, kula lishe bora ikiwamo mboga na matunda kwa wingi, kunywa maji ya kutosha, kupumzika sehemu tulivu na kulala angalau saa nane kwa usiku.