Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fainali AFCON na maandalizi ya kisaikolojia

DOKTA Pict

Muktasari:

  • Fainali hizi za mara ya 35 ya mashindano hayo makubwa barani Afrika, yanayofanyika kila baada ya miaka miwili, yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).

MASHABIKI na wapenzi wa soka barani Afrika wanatarajia kujua bingwa mpya wa michuano ya Kombe la Afrika (AFCON) 2025 Jumapili hii. Ndiyo ile fainali ya michuano hiyo ya 35 tangu ilipoasisiwa 1957 inatarajiwa kupigwa Jumapili, ambapo bingwa mpya atafahamika kwani waliokuwa watetezi, Ivory Coast, waliaga mapema.

Fainali hizi za mara ya 35 ya mashindano hayo makubwa barani Afrika, yanayofanyika kila baada ya miaka miwili, yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).

Kila mara tumezoea zaidi kuona maandalizi ya nje, ambayo mara nyingi ni zile mbinu za kiufundi na mafunzo mbalimbali, ikiwamo mafunzo ya kukaa na mpira zaidi, kukaba zaidi au kujilinda.

Lakini ukiacha mbinu za kiufundi zinazotolewa na kocha pamoja na benchi lake la ufundi, kuna mbinu nyingine kwa upande wa saikolojia. Hii ni moja ya mbinu kubwa na muhimu, hasa kuelekea fainali yoyote ile.

Wachezaji, kama walivyo binadamu wengine, kuelekea katika jukumu kubwa la fainali hupatwa na hali ya wasiwasi au hofu na kutokujiamini. Vitu kama hivyo vinaweza kukosesha ushindi hata kama mchezaji ni timamu kimwili.

Maandalizi ya kisaikolojia yanaweza kufanywa na wachezaji binafsi au wao wenyewe pamoja na manahodha wao, kocha na benchi lake la ufundi, viongozi wa timu, wachezaji wastaafu na watu maarufu wenye ushawishi.

Klabu au timu za taifa, kwa kulipa umuhimu wa kipekee eneo hili, huamua kuajiri wataalamu waliosomea au kubobea katika mambo ya kisaikolojia kwa wachezaji.

Njia za kisaikolojia katika mpira wa miguu zinahusisha kutumia mbinu mbalimbali za kiakili kama vile kutumia picha mnato au video, sauti au kwa vitendo binafsi.

Lengo ni kuwapa uzoefu wachezaji kabla ya kwenda kufanya majukumu yao makubwa katika mechi za fainali, ambazo huleta shinikizo kubwa la kiakili kiasi cha kuweza kuwaletea hofu au wasiwasi.

DOKT 01

MBINU MUHIMU ZA KISAIKOLOJIA

Ni kawaida mchezaji katika kambi zao au hoteli walizofikia kuonyeshwa video au picha za michezo ya hapo awali. Lengo ni kuwazoesha kiakili michezo na matokeo yaliyofanikiwa ili kupanga akili kwa ajili ya mafanikio yajayo.

Hapa ndipo huonyeshwa video za zamani za manguli wa soka wa nchi zao au nyingine. Huweza kujifunza mengi na kupata hamasa ya kushinda.

Hupewa nafasi ya kujieleza binafsi kwa kutumia lugha chanya ya kujifundisha ili kuongeza kujiamini na kubaki makini wakati wote, hata kama yuko katika shinikizo kali.

Tazama mara nyingi pale mchezaji anapokwenda kupiga penati au mkwaju wa faulo, ambayo ni muhimu kwa timu, huzingatia na kupumua kwa kina tumboni ili kutuliza mwili na kubaki mtulivu bila wasiwasi.

Mbinu ya kuvuta pumzi kubwa husaidia kupunguza mkazo wa akili, hatimaye kuleta utulivu, hivyo kutekeleza jukumu la uwanjani kwa umakini mkubwa na uamuzi sahihi.

Huzoeshwa kushikamana na malengo ya timu hata pale inaponekana kuwa hakuna uwezekano wa kushinda. Inaweza kutokea timu imekosa goli katika dakika 15 za mwanzo kama walivyopanga.

DOKT 02

Huweza kuanzisha malengo mapya yasiyopishana na yale ya awali ili kuendana na hali iliyopo, yanayozingatia mchakato maalum ili kudumisha motisha na mwelekeo sahihi wakati wa kucheza.

Hufundishwa kuwa na akili stahimilivu na kutokutetereka, kukuza uwezo wa kukabiliana na vikwazo, kudumisha umakini na kujirekebisha haraka kutokana na makosa ya awali.

Mfano, mchezaji aliyekuwa na nafasi ya wazi huzoeshwa kujisamehe na kurudi tena katika lengo kuu la timu. Hufundishwa kumpa faraja yule aliyekosea ili arudi katika lengo kuu.

DOKT 03

UJUZI KIAKILI ILI KUCHEZA KWA KIWANGO

Kujiamini kila wakati, kwa kuamini katika uwezo wake wa kufanya vizuri bila kuogopa uwezo wa timu pinzani au historia ya mafanikio ya wapinzani wao.

Kuzingatia kwa umakini ili kuzuia vitu au mambo yanayoweza kumtoa mchezoni na kuzingatia kazi iliyopo mbele yake. Ndiyo maana wapo wachezaji wanaweza kuzomewa mwanzo hadi mwisho, lakini wala hawatetereki.

Udhibiti wa kihisia, ikiwamo kudhibiti hofu, woga au wasiwasi, ili kuleta matokeo chanya uwanjani. Ndani ya uwanja kuna vitisho vingi, ikiwamo kukutana na mchezaji staa mwenye jina kubwa na kiwango cha juu.

Kufanya maamuzi sahihi kwa uwazi, ya haraka na yenye ufanisi chini ya shinikizo lolote, ikiwamo wakati wakiwa wamefungwa huku dakika zimebaki chache.

DOKT 04

FAIDA ZA MAANDALIZI YA KISAIKOLOJIA

Ufanyaji uamuzi ulioboreshwa; husaidia wachezaji kuchakata taarifa wanazopewa na walimu wao, kuchagua majibu sahihi na kutumia mbinu chini ya shinikizo.

Uboreshaji wa uzingatiaji na umakini, kwa kukuza uwezo wa kudumisha umakini licha ya vikwazo kadhaa na hatari kubwa zilizo mbele.

Kuweza kudhibiti msongo wa mawazo na wasiwasi; makocha huwafundisha wachezaji kudhibiti hisia, kupunguza wasiwasi wa utendaji na kudhibiti hali zenye mkazo au shinikizo.

Kuongezeka kwa kujiamini; hali hii hukuza imani katika uwezo wa mchezaji mwenyewe na kusababisha kujihatarisha pasipo kuharibu uwezo wake au kujipa majeraha.

Kuwa na ustahimilivu na ujasiri; hii huwafanya kujenga uwezo wa kushinda utendaji mbaya, vikwazo na majeraha yatokanayo na michezo, vilevile kutokubali kushindwa kirahisi.

Kuwa na hamasa na kujitolea; hii humarisha ari ya ndani na kujitolea kwa mafunzo na malengo yaliyowekwa na timu zao za taifa, ingawa hali hii huchochewa na uongozi mzuri wa timu.

Mkusanyiko wa mambo haya ndiyo yanayokwenda kuleta ushindi kirahisi, hata kama wanashindana na timu iliyosheheni mastaa wenye viwango vya juu.