Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haya ndo majeraha yanayosumbua AFCON

DOKTA Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa ratiba ni kwamba kesho Ijumaa zitapigwa mechi mbili za kwanza mapema saa 1:00 usiku ikiwa ni kati ya Mali na Senegal kabla ya Cameroon kuvaana na wenyeji Morocco saa 4:00 usiku.

MICHUANO ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 yanayofanyika Morocco kuanzia kesho inaingia hatua ya robo fainali ambapo timu nane zilizopenya zitaanza kusaka tiketi ya kwenda nusu fainali.

Kwa mujibu wa ratiba ni kwamba kesho Ijumaa zitapigwa mechi mbili za kwanza mapema saa 1:00 usiku ikiwa ni kati ya Mali na Senegal kabla ya Cameroon kuvaana na wenyeji Morocco saa 4:00 usiku.

Keshokutwa Jumamosi itakuwa zamu ya Nigeria na Algeria kabla ya Misri kumalizana na watetezi Ivory Coast.

Hii ni robo fainali iliyobeba vigogo vya soka Afrika kukiwa na wachezaji maarufu duniani kama Mohamed Salah wa Misri, Sadio Mane wa Senegal, Amad Diallo wa Ivory Coast na Victor Osmhen wa Nigeria.

Mastaa ambao hadi sasa wameonyesha ni moto wa kuotea mbali katika hatua za makundi ni Ademola Lookman wa Nigeria, Brahim Diaz wa Morocco na Riyad Mahrez wa Algeria.

Nyota hao wote wameonekana kufanya vizuri katika hatua hiyo wakiwa timamu kimwili. Bahati mbaya majeraha ndio yaliyomemweka nje mchezaji bora wa Afrika 2025 na staa wa timu ya Morocco, Achraf Hakimi, kwa muda.

Mara nyingi ni kawaida wachezaji wanaocheza ligi za kulipwa kucheza mashindano ya Afcon na huwa wakiwa na tahadhari kubwa dhidi ya majeraha yatokanayo na kucheza soka.

Ingawa zipo mbinu zinazosaidia kuepukana na majeraha, lakini kwa mashindano kama hayo ni vigumu kukosekana kwa majeraha kwani mchezo wa soka unahusisha kukumbana kimwili.

Mpaka hatua hii bado mastaa wengi wako timamu wakiwa wamekwepa kupata majeraha  makubwa na leo tutayaona mambo hatarishi na aina ya majeraha yanayojitokeza AFCON 2025.

DOKT 01

MAMBO HATARISHI KWA MAJERAHA

Wachezaji ambao wako katika hatari ya kupata majeraha hayo ni pamoja na wale wanaotumika sana klabuni na timu za taifa, umri mkubwa na majeraha ya mara kwa mara.

Vilevile wale wenye miili isiyo na ustahimilivu, kuwa na mazoezi yasiyo na kipimo, wasiopasha moto mwili, wasiopumzimka, lishe duni, vifaa vya mazoezi visivyo bora na mbinu zisizo sahihi

Majeraha hayo yanajitokeza kwa wanasoka hasa katika eneo la miguuni ikiwamo misuli, maungio, nyuzi za ligamenti na tendoni. Majeraha mengi mpaka hatua hii ni ya wastani, na yanayopona.


AINA YA MAJERAHA


1. Majeraha ya misuli

Kuvutika kwa misuli ya mwili ni kazi ya mara mara katika soka. Ni kawaida kukimbia kasi mara kwa mara. Misuli huvutika kupita kiwango chake na kusababisha vijeraha vya ndani kwa ndani.

Baadaye vijeraha hivyo huwa vikubwa endapo mchezaji atacheza akiwa hajapona vizuri. Majeraha ya misuli huwa ni kuchanika msuli na kuvutika kupita kiasi, majeraha ya kamba za miishilio ya misuli yaani tendoni, uchovu wa misuli na kubanwa na msuli.

DOKT 02

2. Majeraha ya kifundo

Eneo la kifundo cha mguu huwa na harakati nyingi ikiwamo kupiga mpira, kujijeruhi kwa kujipinda vibaya au kukanyagwa. Ni kawaida kuwaona wachezaji wakichechemea wakati wa mwisho wa mchezo.

Majeraha ya kifundo cha mguu yanahusisha kuvunjika vifupa vya vidole vya miguu, majeraha ya tishu laini ikiwamo kuvutika kupitiliza, kukwanyuka na kuchanika kwa ligamenti.

Wakati wa kutembea, kukimbia kuruka na kutua, kifundo huweza kutua vibaya na kujipinda hivyo kujeruhi tishu laini ikiwamo nyuzi ngumu ambazo hujivuta kupita kiasi na kusababisha kupata majeraha.

DOKT 03

3. Majeraha ya goti

Ungio la goti linalobeba shinikizo kubwa na huwa na harakati nyingi wakati wa kucheza. Hii inalifanya kuwa katika hatari ya kujeruhiwa

Majeraha ya kati ya goti ikiwamo tishu laini, ligamenti kuu za goti na mifupa plastiki hupata maumivu sehemu ya goti eneo la mbele na shambulizi la nyuzi ngumu za miishilio ya misuli ya goti yaani tendoni

Majeraha makubwa ya goti yanahusisha madhara au michubuko katika mfupa wa plastiki wa goti na nyuzi ngumu za ligamenti  zinazounga mfupa na mfupa.

Hadi sasa mchezaji aliyepata majeraha mabaya ya goti ni Mohamed Hamdy wa Misri baada nyuzi ya mbele katikati ya goti kukwanyuka, hivyo atakosa mechi zote zilizobaki za mashindano hayo.

DOKT 05

4. Majeraha ya ugoko

Majeraha ya ugoko pamoja na maumivu yake ni moja ya yale yanayotokea kwa wanasoka. Hii ni kwa sababu huvaa kikinga ugoko maarufu kama shin Gurd.

Sehemu hii ambayo iko chini ya goti maumivu yake yanatokea mbele ambako kuna mfupa mkubwa wa mguu chini ya goti unaoitwa kitabibu Tibia.

Vilevile maumivu ya eneo hilo yanaweza kutokea katika makutano ya mifupa ya miguuni na sehemu ya mbele ya kifundo cha miguu.

Majeraha hayo kitabibu hujulikana kama shin splints. Mara kwa mara yamekuwa yakiwapata wanasoka wanaoshiriki mashindano kama hayo.

Umbile hilo husababisha majeraha ya mara kwa mara katika eneo la ugoko sehemu ya chini karibu na kifundo cha mguu.


DOKT 04

5. Majeraha ya mifupa

Mpaka sasa hakuna mchezaji aliyepata mvunjiko wala kuteguka mifupa mikubwa ya maungio makubwa mwili. Ingawa kupata majeraha kwa vijifupa vya funiko la mguu ni kawaida.

Kuvunjika kwa mfupa kunahusisha nyufa au kuvunjika kabisa vijipande viwili au zaidi wakati kuteguka ni kulazimishwa kuhama kwa mfupa kutoka katika pango la maungio. Kuteguka mabega ndiko huwapata wanasoka.

Wachezaji wa mpira wa miguu wamekuwa wakipata mivunjiko midogo katika eneo la kifundo na magoti kwa kuanguka au kugongwa na mchezaji wa timu pinzani. Matukio ya mvunjiko na au kuteguka yameripotiwa mawili katika fainali hizo.

Staa anayecheza Girona ya Italia, Azzedine Ounahi ni miongoni mwa waathiriwa wakubwa wa majeraha alipowasili katika Uwanja wa Prince Moulay Abdellah huko Rabat akiwa anatembea kwa magongo.

Alikuwa amevaa kiatu tiba cha kujikinga kwenye mguu wake wa kushoto kabla ya pambano la raundi ya 16 la Morocco dhidi ya Tanzania. Ilielezwa aliumia wakati wa mazoezi.

DOKT 06

6. Majeraha ya kiakili

Tazama kilichowapata mashabiki na wachezaji wa DR Congo wakati wakipoteza mchezo dhidi ya Algeria Jumanne usiku katika dakika 120 za nyongeza ikiwa zimebaki mbili ili mchezo uishe. Tukio hilo limewaumiza kihisia na kuwaachia majeraha ya kiakili ambayo ni athari mojawapo kubwa katika masiha yao.


7. Maeneo mengine ya mwili

Ni kawaida pia maeneo mengine ya mwili kugongwa na kupata majeraha ikiwamo yale ya kichwa na kifua hasa katika kuwania mpira wa juu. Vilevile mikono na vidole, hasa kwa makipa wakati wa kudaka.