Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KASONGO: Simba, Yanga zinatuvuruga

MASHABIKI wengi wa soka nchini hupenda kutupa madongo kwa Shirikisho la Soka (TFF) na wakati mwingine Bodi ya Ligi (TPLB) pale kunapokuwa na mkanganyiko juu ya uamuzi unaozihusu Simba na Yanga.

Wapo wanaoamini kuwa klabu hizo kongwe zinabebwa au kuogopwa pale zinapozingua kwenye ishu za nidhamu na masuala mengine mengi.

Hata hivyo, Bodi ya Ligi imefichua ukweli na kukiri vichwa huwauma pale wanapotaka kuchukua uamuzi dhidi ya klabu hizo kwa kuhofia wasiumbuke.

Mtendaji Mkuu wa TPLB, Almas Kasongo amefanya mahojiano maalumu na Mwanaspoti ambapo pia amefunguka mambo mengi wanayokabiliana nayo katika kuendesha ligi mbalimbali nchini.


SIMBA, YANGA PASUA KICHWA

“Bodi ni wasimamizi wa Ligi Kuu Bara nikiwa na maana ya timu zote zinazoshiriki lakini katika mapitio ya adhabu kwa klabu tumekuwa tukiwa na wakati mgumu zaidi pale tunapokuwa na kesi za Simba na Yanga,” anasema Kasongo na kuongeza;

“Hizi timu ni pasua kichwa, hata upitiaji wa sheria pale tunapobaini makosa yao tunaangalia kwa usahihi zaidi ili wakati wa kutoa uamuzi isije ikaibuka mijadala ambayo itatufanya tukaonekana hatutendi haki.”

“Mfano suala la hivi karibuni lililokuwa likiwahusu Clatous Chama na Stephan Aziz Ki ni kosa kabisa kisheria na lipo kwenye kanuni zilizotumwa kwa klabu zote, lakini bado wachezaji wao wakubwa na wa kigeni wamelifanya mashabiki wakatujia juu wakidai kuwa tunafanya makosa.”

Kasongo anasema timu hizo sio za kwanza kuadhibiwa kwasababu tayari walikuwa wamefanya hivyo kwa mchezaji wa Dodoma Jiji, Hussein Masalanga waliyemtoza faini na kumfungia mechi tatu kwa kosa la kugoma kusalimiana na wachezaji wa Geita Gold FC wakati wa mchezo wa Ligi Kuu.


UTATA WA MEI 8

Kuliahirishwa dabi ya Simba na Yanga; “Tangu nimeanza kujihusisha na soka tukio la Mei 8 ndilo lililonitikisa zaidi. Sitakaa nisahau na nimeshaandika kwenye kitabu changu cha kumbukumbu, ni tukio ambalo lilikuwa kubwa mno kwa upande wangu,” anasema na kuongeza;

“Naishukuru Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye aliingilia kati na kulitolea ufafanuzi Bungeni, taarifa ambayo ilipunguza makali yaliyokuwa yakiendelea kutoka pande mbili Simba na Yanga”.

“Siwezi kufunguka shida iliyotokea lakini ninachoweza kusema tukio hilo halitakaa likafutika kwenye maisha yangu ya mpira, mimi nikiwa kama kiongozi wa soka lilinikuta kipindi ambacho hata sikutarajia nashukuru lilipita na kuisha salama acha maisha mengine yaendelee,” anasema.

Mechi hiyo baada ya kushindikana kuchezwa Mei 8 iliahirishwa na kuchezwa Julai 3 mwaka jana na Yanga ikaibuka na ushindi wa bao 1-0.


RATIBA CHANGAMOTO

“Ndani ya misimu miwili mfululizo kuna mabadiliko makubwa sana kwenye suala la ratiba japo hatuwezi kumridhisha kila mmoja lakini hadi tulipofikia kwa upande wetu tunamshukuru Mungu na tunaendelea kuboresha,” anasema na kuongeza;

“Ratiba ndo ligi, kwahiyo tukikosea kwenye ratiba tumekosea mashindano na bado imebaki kuwa ngumu kwetu lakini tumepambana hadi hapa tulipo, suala la mabadiliko litaendelea kuwepo pale tutakapoona kuna ulazima lakini msingi wake mkubwa ni kunufaisha klabu na maslahi ya wadhamini ambao ndio wadau wakubwa,” anasema.

“Kwa mujibu wa mkataba tulioingia na wadhamini, katika mechi 240 za ligi kila mchezo unatakiwa kurushwa ‘live’ hivyo hatuwezi kuonyesha mechi za raundi moja zote kwa siku moja na ndio maana ratiba imepangwa kwa mgawanyiko,” alisema na kuongeza;

“Kila timu inatakiwa kupata haki ya kuonyeshwa pia na anayerusha matangazo anataka kupata haki yake hivyo hiyo ndio sababu kubwa hata ukiangalia mataifa mengine makubwa yaliyoendelea pia yana chaneli zao maalum za kuonyesha mpira.”

Anasema wadhamini walioingia nao mikataba pia wana haki kwenye upangaji wa ratiba kwasababu wamewekeza hivyo haina maana kwamba ni kitu ambacho kimeibuliwa tu ni mipango iliyowekewa mikakati.

“Ndani ya miaka mitano kuna uwekezaji mkubwa umefanyika kwenye soka la Tanzania kuna watu wamewekeza kwenye kuonyesha mechi ‘live’, kutangaza na wadhamini wakuu wamesaidia kupunguza baadhi ya changamoto za klabu zetu zinazoshiriki ligi,” alisema na kuongeza;

“Tumepunguza changamoto za timu kufika eneo la kituo cha kucheza siku moja kabla ya mchezo au timu kushindwa kulipia hoteli walizokuwa wamefikia hiyo ni kutokana na uwekezaji ambao unatulazimisha tutengeneze ratiba ya hivyo.”


UEFA WAMEHUSIKA

“Kuna mafuzo tuliyapata ya namna ya uandaji wa ratiba, Januari tulikuwa kwenye mafunzo na watu wa UEFA yalikuwa yanaitwa ‘League Development Program’ tumejifunza utengenezaji wa ratiba ambayo itakuwa rafiki kwa wadau wote pamoja klabu za michezo na mashabiki,” anasema na kuongeza;

“Suala la ratiba ni mchakato ukitazama kule tulipotoka mpaka tumefikia kuna madiliko ni makubwa katika upande wa ratiba ni imani yetu sisi itafika wakati hili suala la ratiba litakuwa limekakaa sawa na tutakuwa tumefikia matarajio ya mashabiki, lakini kwasasa

tupo kwenye maboresho ya changamoto tunazipokea kutoka kwa wadau, klabu na mashabiki wa mpira wa miguu.”


FUNGIA VIWANJA

“Ni kweli tunafungia viwanja, shida inatokea katikati ya ligi na sisi hatuwezi kuacha kufungia kwa kuhofia maneno,” anasema na kuongeza;

“Changamoto ya viwanja vyetu ni nyasi asilia na vingi vinakosa huduma kwahiyo wamiliki na watumiaji wa viwanja watunze viwanja ili wakaguzi wanapofika waone viwanja bado vinastahili kutumika na viwanja vingi vinasimamiwa na watu ambao hawana taaluma ya utunzaji,” anasema.

Kasongo anasema kiwanja ni kigezo namba mbili cha leseni ya klabu na wao kama bodi wanalazimika kuvifungia viwanja ambavyo havikidhi vigezo vilivyowekwa huku akisisitiza kuwa katika mkutano mkuu wa mwaka juzi (2020) klabu ziliazimia kwenda kwenye utekelezaji wa leseni ya viwanja ikiwa ni mojawapo ya kanuni na hilo ni suala endelevu.

“Tumekuwa wakali kwasababu tunaamini ubora wa viwanja utapelekea ushindani ulio wa haki na pia tunaondoa hatari ya wachezaji kuumia pamoja na usalama wa mashabiki,” anasema.


FIFA KUWEKEZA CHAMPIONSHIP

“Tunaendelea kutafuta wadhamini kwaajili ya kuongeza nguvu kwenye soka la wanawake, Championship na First League ambayo hadi sasa imeweza kupata udhamini wa ligi yao kuanza kuonyeshwa baada ya FIFA Plus kumwaga fedha huko,” anasema na kuongeza;


FAINI MARA DUFU

“Pamoja na faini kutolewa lakini bado makosa yamekuwa yakijirudia na timu na wachezaji wala hawajali kwasababu wanaona watalipa faini na mambo yataendelea na sisi tumekuwa na utaratibu wa kupandisha dau pia tunawaza namna ya kuongeza adhabu ili kuepukana na marudio ya makosa hayo.”


BODI IJITEGEMEE

“Mchakato unaoendelea upo chini ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia ambaye ameahidi kumaliza miaka yake ya uongozi akiwa ametusaidia kuhakikisha bodi inajisimamia.”