Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kaseja: Simba, Yanga hazitaki ukweli

New Content Item (1)
New Content Item (1)

JANA kwenye mfululizo wa makala iliyotokana na mahojiano maalumu na kipa nyota wa soka nchini aliyewahi kutamba, Simba, Yanga na Taifa Stars, Juma Kaseja tuliona namna alivyoikacha Mtibwa Sugar na kusajiliwa Simba kwa kuvutwa na ushawishi wa gari aliloahidiwa na vigogo wa Msimbazi.

Kaseja alifichua namna Simba, Yanga na Mtibwa zilivyokuwa zikimpigia hesabu za kumsajili, kabda ya Merey Balhabou aliyekuwa mmiliki wa Moro United anayeizimia Simba alivyochangia kumpeka Msimbazi na kuanza kumiliki gari tangu mwaka 2002 na jinsi alivyokuwa na mastaa katika kikosi hicho kilichoweka heshima Afrika 2003 kwa kuivua taji la Afrika, Zamalek ya Misri.

Aligusia jinsi alivyokutana na kipa wa zamani wa Twiga Stars ambaye kwa sasa kocha wa makipa maarufu nchini, Fatma Omary na kumfundisha!
Leo anafunguka namna Fatma Omary alivyokutana naye KMC na jinsi alivyofanya tukio la kutoroka shuleni ili akasaini mkataba, mbali na kuanika ukweli juu ya sajili zinazofanywa na klabu za Simba na Yanga kwa michuano ya kimataifa, akisema klabu hizo huwa hazipendi kuambiwa ukweli ila kutaka kusifiwa tu. Kivipi? Endelea naye kwenye hitimimisho la mahojiano yake na Mwanaspoti.


FATMA KUINGIA KMC
"Mchakato wa Fatma kuajiriwa KMC ni kama ulipitia kwangu, kwasababu nilikuwa nimefanyiwa upasuaji wa goti na kutakiwa kuanza mazoezi kidogo kidogo, hivyo yeye ndiye alianza kunifanyia mazoezi hayo kwa kumkaribisha kwenye viwanja wa KMC pale viwanja vya Kijitonyama Bora.
"Baadaye alionekana ni mtu anayeweza kufanya ile kazi, makipa wote wakaanza kufanya mazoezi nami chini ya Fatma, hivyo viongozi waliona kama anaweza kwa nini asiajiliwe, naamini ni mtu anayeweza sema kuna ile kasumba tu ya watu kuwa mwanamke hawezi ila Fatuma anaweza na anatushinda wengi wanaume," anaeleza Kaseja.


ALITOROKA SHULE
Kuonyesha kwa soka lipo kwenye damu yake, Kaseja aliwahi kufanya tukio ambalo halikumsaidia kutokana na umri wake kuwa mdogo.
"Nilitokea Kigoma kwenye Umitamshumta, baadaye Makongo (Umiseta), nimecheza timu ya Mashariki Umiseta, na kipindi hicho ukicheza kwenye kanda basi unakuwa mchezaji haswa mwenye kiwango kizuri.
"Baadaye tulienda kucheza mechi ya kirafiki nikiwa na Shule ya Sekondari Makongo, mechi hiyo ilikuwa kati ya Mtibwa Sugar na Polisi Moro za huko Morogoro ndipo Reli Moro waliniona.
"Sasa waliponitafuta nikatoroka shule kwenda Reli kusajiliwa lakini nilirudishwa shuleni kwani waliona bado umri wangu mdogo, ilibidi nirudi Makongo, nikaendelea na shule ndipo baadaye Moro United waliniona hivyo nikaenda kucheza 2001-2002, mwishoni mwa 2002 nikacheza Mtibwa Sugar.
"Watu wengi hawajui kama nimecheza Mtibwa Sugar, nilicheza pale mechi moja kwenye mashindano ya Kombe la Nyerere 2002, mechi niliyocheza ni Mtibwa Sugar na Yanga." anasema


MAFANIKIO YAKE
Kaseja ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwa na mafanikio makubwa nje ya soka ambapo yeye anasema ni kujipanga na kuweka malengo.
"Mimi sikusoma na hakuna urithi ambao naringia, niliamini njia rahisi ya kuishi vizuri na kupata mafanikio makubwa ni kujituma na kuheshimu kile ninachokipata, maendeleo sio kitu rahisi inahitaji uvumilivu, kukaa na watu wanaoweza kukuambia maisha ya baadaye.
"Maendeleo pia sio akili yangu ni jambo la kumshukuru Mungu, hata yule ambaye hajapata si wa kumlaumu kupata sio ujanja wetu, Mungu amenielekeza huko na kupitia jitihada za watu wa karibu, familia, unaangalia nyuma unaona hauna msaada.
"Unaweza usipate sana kama unavyotaka lakini hata kwa kile kidogo nilichonacho huwa namshukuru Mungu maana hata baadaye watoto watakuwa na cha kusema kuwa baba alicheza mpira ametuachia nyumba hii, hata wao wakipata pesa nyingi hapo baadaye wanaweza kuamua cha kufanya."


WATOTO
Ana watoto mapacha (kike na kiume) lakini anakwamba mwanaye wa kiume ndiye amefuata nyayo zake.
"Mwanangu wa kiume anapenda sana mpira, yaani anapenda mno hivyo huwa namfundisha mazoezi namna ya kuchezea mpira, ila siwezi kumzungumzia sana kuwa atapenda mpira hadi akiwa mkubwa maana huenda akabadilika hapo baadaye na kuona kwamba soka sio kitu anachokipenda.
"Kwasasa anapenda ila akikua ataamua mwenyewe kuwa anaupenda ama kitu kingine anakipenda nje ya mpira."


UKUTA WAKE
"Nimecheza na wachezaji wengi sana, nimekutana na safu mbalimbali za ulinzi na kwa nyakati tofauti kama kipindi cha akina Boniface Pawasa, Amri Said, Kassim Issa, kikaja kizazi cha akina Nyosso, Joseph Owino, Ntiro, Canavaro, Agrey Morris, Yondani, kizazi cha sasa akina Mfuko, Andrew Vincent 'Dante' nimekutana karibu na vizazi vyote na vizuri.
"Watu wote niliocheza nao ni bora na kila kizazi nilichocheza nacho kilikuwa bora na hakuna straika aliyekuwa hatari, straika ili atimize majukumu yake ni kufunga na kipa ili atimize yake ni kuokoa."


SIMBA, YANGA CAF
Tanzania inawakilishwa na timu nne kwenye michuano ya CAF ambapo Simba na Yanga wanacheza Ligi ya Mabingwa wakati Azam FC na Singida Fountain Gate watashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.
Lakini kuelekea kipindi cha usajili na maandalizi yao Kaseja anasema;
"Unajua Simba na Yanga hawapendi kuambiwa ukweli, wao wanapenda kusikia mambo mazuri tu ndio maana sipendi sana kuwazungumzia, ni timu ambazo mashabiki wao hawapendi kusikia baya lolote, ukiongea tu unaonekana msaliti, hivyo tunawaachia  wao wanajua mipango yao na wakiamua kutimua kikosi kizima ni wao.
"Sisi tutaendelea kuwa wadau wao, wakifanya vizuri tutawasifia wakikosea tutakaa kimya, lakini hawa Singida Fountain Gate hii ni nafasi yao ya kuandaa kikosi vizuri ili iwe timu ya ushindani maana Azam FC tayari wao wapo kwenye ushindani."


MIPIRA MIGUMU
Anasema kila kipa ana mipira yake anayoona migumu kuidaka lakini kwake ni hivi; "Mipira ile inayotokea moja kwa moja (One v One) kwa sababu kila mtu anakuwa na nafasi ya kufanya kile anachoweza kufanya kwa wakati huo, hiyo ni mipira migumu kwangu."
Juu ya ishu ya kuwa mwanachama wa Simba, Kaseja anasema kwa ufupi;
"Kila mtu ana nafasi ya kuzungumza, nikiwa Simba kuna baadhi ya watu walisema mimi ni Yanga, nilienda Yanga wakanambia mimi ni Simba, hivyo unapaswa kuwasikiliza na kuendelea na majukumu yako."


BIFU NA MAXIMO
Alipoulizwa juu ya bifu lake na Maximo akiwa Taifa Stars kasema anasema; "Hata ukiniambia shida ilikuwa nini sijui hadi leo, maana sikuwahi kugombana naye, sikuwahi kuonywa kwa utovu wa nidhamu lakini nilishangaa ilikotokea kuwa nilicheka tulipofungwa mechi na Senegal, ikaja nikasikia kuwa niliambiwa niingine nikakataa.
"Hivyo kulikuwepo na vitu vingi sana hadi kocha alipoondoka japo nilimuomba nikutane naye ili kumuuliza kuna shida gani, niombe msahama lakini hakuwahi kunipa hiyo nafasi, basi maisha yakaendelea hivyo.
"Baadaye alirudi Yanga akanambia tuendelee na maisha yale yaliyotokea Stars yaliishapita na hakuniambia shida ilikuwa nini. Sisi wabongo tunajua maisha yetu naamini kuna watu walimpelekea maneno ya uongo kutokana na ushindani uliokuwepo.
"Kulikuwepo na ushindani mkubwa, mashabiki wa Yanga walitaka Ivo Mapunda adake na wa Simba walitaka nidake mimi, inawezekana kuna baadhi ya wachezaji walipeleka maneno kutokana na ukaribu wao na kocha," anasema na kuongeza;
"Hivyo niliona sina sababu tena ya kubembeleza suluhu maana niliomba ila hakunipa nafasi bahati nzuri aliondoka akaja kocha mwingine aliniita Stars. Bahati mbaya haya matukio yamekuwa yakinitokea mara kwa mara na nikirudi nakuwa shujaa, Jan Poulsen akaniita nikachukuwa kombe la CECAFA akaondoka wakachukuwa wazawa nikawa nje kwa muda mrefu sana nao wakaondoka.
"Alipokuja Ettiene Ndayigarije akaniita tukaipeleka timu CHAN na makundi kufuzu Kombe la Dunia, kwa hiyo unamshukuru yanayotokea yanakuwa ni mafunzo katika maisha yangu." anasema Kaseja
Kaseja anawashauri vijana na wachezaji kwa ujumla kuwa kila jambo lina wakati wake, hivyo ni kujituma, kujitunza na kuheshimu mazoezi.