Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ibenge na ndoto ya uandishi iliyozimwa na ubaguzi Ufaransa

Muktasari:

  • Naam Taoussi na Ibenge walisoma darasa moja la ukocha 2021 huko Morocco kwa ajili ya kozi ya leseni ya juu zaidi ya ukocha inayoitwa Pro License iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika.

KLABU ya Azam FC imemtangaza Jean-Florent Ikwange Ibenge kuwa kocha mkuu mpya kwa msimu wa 2025/26 akirithi mikoba ya ‘classmate’ wake Mmorocco Rachid Taoussi.


Naam Taoussi na Ibenge walisoma darasa moja la ukocha 2021 huko Morocco kwa ajili ya kozi ya leseni ya juu zaidi ya ukocha inayoitwa Pro License iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika.


Ibenge, raia wa Ufaransa mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DR Congo), ni mmoja wa makocha wenye uzoefu na mafanikio makubwa Afrika.

Amefundisha soka China, India na Afrika akishinda mataji makubwa ya ndani na nje.

Akiwa na umri wa miaka 63, Ibenge alizaliwa Desemba 4, 1961 katika mji wa Leopoldville ambao sasa ni Kinshasa, DR Congo.

Alihamia Ufaransa na baba yake miaka ya 1970 akiwa bado kijana mdogo na kupata elimu yake huko.

Japo alipenda sana kucheza mpira, lakini baba yake alimtaka asome hivyo hakuweza kuwekeza sana kwenye mpira.

Naye mwenyewe akachagua kusomea uandishi wa habari kazi ambayo aliipenda sana.

Lakini bahati mbaya kwake akiwa kama mhamiaji wa Kiafrika, Ufaransa ilikuwa na ubaguzi sana wakati huo na haikuruhusiwa wahamiaji hasa weusi kusomea uandishi kwenye vyuo vya serikali.

Nafasi pekee ilikuwa kwenye vyuo binafsi ambavyo vilikuwa ghali sana - akashindwa.

Akachagua kusomea uchumi na kuhitimu shahada, lakini ubaguzi ukasababisha akose kazi.

Alisambaza barua za kuomba kazi kila sehemu, lakini alijibiwa sehemu moja tu - akaambiwa sio kazi aliyoomba bali ya kutunza bustani ndio pekee ambayo ingemfaa.

Baada ya kutembea na vyeti muda mrefu bila kupata kazi ndipo akaamua kurudi katika mpira - mchezo aliokatazwa na baba yake.

Akaanza kucheza tena katika timu mbalimbali za mtaani kwake na kupata timu za madaraja ya kati nchini Ufaransa na baadaye Ujerumani. Nafasi yake ilikuwa beki wa kati. Alicheza soka kuanzia 1979 hadi 2003 alipostafu.

Wakati akicheza soka akafanikiwa kupata uraia wa Ufaransa, angalau sasa akaanza kupata haki fulani za kiraia ambazo alizikosa awali.

Alipostaafu kucheza akaanza kusomea ukocha na kufundisha timu za watoto, vijana, madaraja ya chini huku akipanda kidogokidogo.

Wakati China inafungua milango kwa uwekezaji katika mpira kama inavyofanya Saudi Arabia sasa hivi na yeye akakimbilia huko.

Akafundisha moja ya klabu kubwa za China - Shanghai Shenhua akianza kama kocha msaidizi wa Jean Tigana mmoja wa makocha wakubwa Ufaransa na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa.

Hapa Tanzania kuna mchezaji aliitwa Tigana kwa heshima ya huyu, japo jina lake halisi lilikuwa Ally Yusuf.

Tigana akaondoka klabuni hapo na Ibenge akawa kocha mkuu akiwafundisha nyota kama Didier Drogba na Nicolas Anelka.

Itakumbukwa kwamba Drogba alitoka kuisaidia Chelsea kushinda Ligi ya Mabingwa Ulaya Mei 2012 na baadaye Julai kujiunga na Shanghai Shenhua akakutana na Ibenge.

Mwaka 2014 Ibenge akajiunga na AS Vita, timu aliyoifundisha kwa miaka tisa akiisaidia kushinda mataji ya Ligi Kuu DR Congo na kufika fainali mbili za Afrika - Ligi ya Mabingwa 2014 na Shirikisho Afrika 2018.

Wakati akiwa kocha wa AS Vita pia aliifundisha timu ya taifa ya DRC na kuisaidia kushinda Chan 2016. Baada ya miaka tisa na AS Vita mwaka 2021 akatimkia RS Berkane ya Morocco aliyoiongoza kushinda Kombe la Shirikisho Afrika 2022.

Mwaka huohuo akatimkia Al Hilal ya Sudan aliyoitumikia hadi hivi karibuni alioondoka na kupojiunga na Azam FC.