Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hizi hapa 'Facti' za AFCON 2025, Morocco

Muktasari:

  • 5 – BAO la ushindi la Mohamed Salah katika dakika za nyongeza dhidi ya Zimbabwe linamaanisha kuwa yeye ndiye Mmisri wa kwanza kufunga katika mashindano matano tofauti ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). Farao. 

6 – MASHUTI sita ya Sadio Mane yaliyolenga goli dhidi ya Botswana ndiyo mengi zaidi kuwahi kupigwa na mchezaji mmoja kwenye mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) tangu mwaka 2010.   


5 – BAO la ushindi la Mohamed Salah katika dakika za nyongeza dhidi ya Zimbabwe linamaanisha kuwa yeye ndiye Mmisri wa kwanza kufunga katika mashindano matano tofauti ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). Farao. 


3 – NI wachezaji watatu tu waliowahi kufunga mabao 2 au zaidi katika mechi moja ya AFCON wakiichezea Tunisia katika karne ya 21.

- Francileudo Santos 

- Wahbi Khazri 

- Elias Achouri 


17/9 – MASHUTI 17 ya Senegal yaliyolenga lango na nafasi tisa kubwa walizotengeneza dhidi ya Botswana ni rekodi ya juu zaidi kwa timu yoyote katika mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) tangu mwaka 2010. Kiwango cha juu kabisa. 


1 - KWA bao lake la ushindi dhidi ya Angola jana, Lyle Foster amekuwa mchezaji wa kwanza kutoka Afrika Kusini kufunga bao katika Kombe la Mataifa ya Afrika huku akichezea klabu ya Ligi Kuu ya England, tangu Phil Masinga wa Leeds United alipofunga dhidi ya Cameroon mwaka 1996. Bafana.


5+5 - MAMADOU Sangare wa Mali katika mechi ya kwanza (MD1) dhidi ya Zambia amekuwa mchezaji wa kwanza kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika kupiga chenga 5+ kimafanikio  (6) na kuingia uvunguni (tackles) mara 5+ (7), tangu Abdelaziz Barrada wa Morocco alipofanya hivyo dhidi ya Cape Verde mwaka 2013.


8 - BAO la ushindi la Mohamed Salah kwa Misri dhidi ya Zimbabwe katika dakika za nyongeza lilikuwa bao lake la nane kwenye AFCON – ni wachezaji wawili tu waliowahi kufunga zaidi yake kwa Misri kwenye mashindano haya: Hassan El-Shazly (mabao 12) na Hossam Hassan (mabao 11).


8 + 7 – OMAR Marmoush amekuwa mchezaji wa kwanza kupiga mashuti 8+ na kupiga chenga 7+ kimafanikio katika mechi moja ya AFCON tangu rekodi za Opta zilipoanza kutunza. Akashinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi (MVP).


35 – MISRI ilipiga jumla ya mashuti 35 kuelekea kwenye lango na kupika nafasi kubwa 8 dhidi ya Zimbabwe, zote zikiwa ni idadi kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa kwenye mechi moja ya Kombe la Mataifa ya Afrika tangu Opta ilipoanza kuchambua mashindano hayo mwaka 2010. Mvua ya mashambulizi.


92 - BAO la kuwasawazisha la Patson Daka katika dakika ya 92 dhidi ya Mali lilikuwa goli la kwanza kabisa la Zambia kubadilisha matokeo katika dakika ya 90 au baadaye katika Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). Dakika za jioooni.


206 - MOROCCO ilipiga pasi 206 zilizowafikia walengwa katika sehemu ya mwisho ya uwanja (final third) dhidi ya Comoros, ikiwa ni rekodi mpya kwa timu moja katika mechi ya AFCON tangu kuanzishwa kwa rekodi za Opta. Walisakwa!