Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Haya ndo majina ya kushangaza katika soka

Muktasari:

  • Tokea binadamu kuja ulimwenguni, kila mtu anapewa jina na hulitumia pamoja na la baba, babu au familia, na wengine huwa na jina la utani na huwa maarufu zaidi kuliko kwa jina lake rasmi.

FIKIRIA tungekuwa tunaishi vipi kama tungekuwa hatuna majina na kutambulika tu kama binadamu, yaani watoto wa Adam na Hawa.

Tokea binadamu kuja ulimwenguni, kila mtu anapewa jina na hulitumia pamoja na la baba, babu au familia, na wengine huwa na jina la utani na huwa maarufu zaidi kuliko kwa jina lake rasmi.

Hata miti, wanyama, ndege, wadudu, vijiji na miji, majengo, barabara, taasisi, vyama na vilabu huwa na majina.

Majina ni kielelezo kikuu cha utambulisho, ambao ni muhimu kwa mawasiliano, kujenga uhusiano, na mara nyingi majina ya watu au taasisi huwa na uhusiano na historia, mila au utamaduni wa watu au asili yao.

Wakati mwingine tunasikia baadhi ya majina ya watu, hushangaa na kujiuliza kwa nini huyo mtu alipewa jina hilo; huliona si zuri, methali ya tusi au lenye viashiria vya udhalilishaji.

Majina mengine ambayo chanzo chake ni katika mila na tamaduni za watu hao huwa na maana tofauti na ya lugha ya Kiswahili, lakini ukilisikia unashituka, na unapotaka kulitumia ulimi hukataa kulitamka.

Majina ya ajabu pia yapo kwa timu za soka katika nchi nyingi, na leo nitayaelezea machache. Nilipokuwa Ghana mwaka 1975 na kufika nchi za jirani kwa kazi au matembezi, nilikutana na majina yaliyonishangaza ya klabu za soka.

Ghana kuna klabu nyingi zenye majina ya aina hiyo, yaani yanayostaajabisha. Kwa mfano, katika mji wa Cape Coast ipo klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya Ghana inayoitwa Dwarfs (vijeba/mabilikimo).

Wengi wa hawa mabilikimo wapo Congo (zaidi ya milioni 1.5), na wachache wapo katika milima iliyopo Brazil. Urefu wa watu hawa ni wa kati ya futi 3 na inchi 10 na futi 4 na inchi 10.

Kilichonishangaza ni kwamba wengi wa wachezaji wa timu hiyo ya mji wa Cape Coast, ambao wakazi wake wengi ni wa kabila la Fante, walikuwa warefu zaidi kuliko wa makabila ya nchi hiyo; Ashanti, Ga na Ewe.

Vilevile ipo timu inayoitwa Hasaacas, jina ambalo halipo katika msamiati wa watu wa nchi yote ya Afrika Magharibi.

Nilipouliza niliambiwa jina hilo lilizuka mwaka 1931 pale kikundi cha wafanyakazi wa reli walipounda timu hiyo ya kandanda. Watu hawa waliamua kuunganisha herufi za kwanza za majina ya waanzilishi wa timu hiyo. Kilichopatikana ni neno H.A.S.A.A.C.A.S, likimaanisha majina ya Hammond, Amua, Sakyi, Adotei, Allotey, Cann, Adotey na Sackey.

Timu nyingine inayocheza Ligi Kuu ni Eleven Wise (Watu Werevu 11) ya mji wa Sekondi-Takoradi uliopo magharibi ya nchi hiyo.

Timu nyingine zenye majina ya ajabu Ghana ni pamoja na Kokomlemle Witch Doctors (Wachawi wa Kokomlemle), Mankaoable Beautiful Hurricane (Kimbunga Kizuri cha Mankaoable) na God’s Ladies (Watoto wa Kike wa Mungu).

Nchi jirani ya Nigeria imetia fora kwa majina ya ajabu ya timu za kandanda. Huko zipo timu zenye majina kama Box 2 Box FC (Sanduku hadi Sanduku). Mashabiki wa timu hii huenda uwanjani wakiwa wamebeba masanduku.

Katika mji wa Ife, ambapo watu wake wengi ni wa kabila la Yoruba, ipo timu inaitwa No No No FC (Hapana Hapana Hapana).

Timu nyingine yenye jina la ajabu ni God Delivered Me Bible Church FC (Mungu Kanijaalia Kanisa la Biblia), ambayo ipo katika mji wa Ogun, Kusini Magharibi. Gambia zipo timu zenye majina kama The Loyal Hooligans (Wahuni Watiifu), Saint FC (Klabu ya Watakatifu) na We Die Here (Tutakufa Hapa Hapa).

Botswana ipo timu inayoitwa Naughty Boys (Watoto Watundu), na nyingine inaitwa Eleven Angels (Malaika 11).

Timu ya kandanda ya Chuo Kikuu cha Gloucestershire, England, ni Egg Fried FC (Yai la Kukaanga), na Marekani timu ya chuo kimoja inaitwa How I Met Your Mata FC (Namna Nilipokutana na Mama Yako), na katika jiji la Atlanta ipo timu inayoitwa Sons of Pitches (Watoto wa Kiume wa Viraka vya Lami).

Katika Chuo Kikuu cha London ipo timu yenye jina la Who Ate All the Depays (Nani Amekula Sadaka Yote).

Katika jiji la Nottingham Forest ipo timu inaitwa Chicken Tikka Mo-Salah (Kuku wa Kuchoma wa Mo Salah, mchezaji wa Liverpool). Timu moja iliyopo Sussex, England, inaitwa Earth and Wind FC (Ardhi na Upepo), na ipo timu Hispania inayoitwa Tea and Biscuits (Chai na Biskuti).

Katika nchi nyingine zipo klabu za michezo zinazoitwa Devils (Mashetani), Robbers (Wezi), Hooligans (Wahuni), Stupid (Wapumbavu), Fools (Maajuha) au Cheaters (Matapeli).

Klabu nyingine zinatumia majina ya wanyama, ndege na wadudu, wakiwemo konokono, panya, konokono na siafu. Pia zipo klabu zenye majina ambayo ukiyataja pumzi zitakwisha kutokana na urefu wake, na kazi itakuwa pevu zaidi kwa mtu mwenye maradhi ya pumu.

Miaka kama 15 hivi iliyopita iliundwa timu Poland ambayo jina lake ni refu na imekuwa kazi pevu kuliandika katika tiketi ya mchezo. Timu hii inaitwa Szczakowianka Jaworzno.

Ifuatayo ni orodha ya baadhi ya majina ambayo ningependa wasomaji wafanye mazoezi au washindane kuyatamka:

Genclerbirligi Spor Kulubu (ni klabu ya Uturuki iliyoundwa mwaka 1923 na inashiriki Ligi Kuu);

Taumatawhakatangihangakoauauotamateapokaiwhenuakitanatahu (usishangae, hili ni neno moja). Klabu hii, ambayo jina lake ndilo refu kuliko la klabu yoyote ya mchezo duniani, ipo New Zealand. Jina hili linatokana na jina la mlima wenye urefu wa mita 305 uliopo katika nchi hiyo; na Clwb Pel Droed. Hicho ni kifupisho cha klabu inayoitwa Llanfairpwllgwyngyllgogerychwyrndrobwllllantysiliogogogoch FC. Klabu hiyo ni ya Daraja la Kwanza Wales, Uingereza, iliyoundwa mwaka 1899.