Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

2026 afya na utimamu ndio kila kitu

DOKTA Pict

Muktasari:

  • Tumewaona wanasoka kadhaa wanaocheza ligi za ndani na zile za kulipwa za majuu ambako wachezaji wanalipwa pesa nyingi ikiwamo wale wanaocheza Ulaya kama EPL, La liga, Serie A, Bundesliga na Ligue 1.

NI sikukuu ya mwaka mpya wa 2026, huku tukiwa sasa tunafuatilia mashindano ya Afcon 2025 kuitazama timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ iliyopambana na kuvuka kutoka hatua ya makundi hadi 16 bora kwa mara ya kwanza.

Tumewaona wanasoka kadhaa wanaocheza ligi za ndani na zile za kulipwa za majuu ambako wachezaji wanalipwa pesa nyingi ikiwamo wale wanaocheza Ulaya kama EPL, La liga, Serie A, Bundesliga na Ligue 1.

Katika kuupokea mwaka huu na huku tukiendelea kufuatilia mashindano ya Afcon, hebu kwa wivu mkubwa tazama miili ya wa wachezaji wanaoshiriki mashindano hayo.

Kwa sisi wa Tanzania, mtazame nahodha wa timu ya taifa, Mbwana Samatta ambaye anakipiga katika timu ya Le Havre inayoshiriki Ligi Kuu Ufaransa.

DOKT 01

Hata kama huwezi kufanana na wachezaji hao, basi 2026 angalau jipange uweze kuwa na mwili bora wenye afya na utimamu thabiti. Kuwa na mwili wa mwanamichezo ni faida kubwa kiafya.

Ni kweli mashabiki wanalipa viingilio kwenda kupata burudani iwe soka au matamasha ya mziki, lakini wanapaswa kutazama afya na utimamu wa miili yao.

Hii ni kwa sababu vitu hivyo viwili ndivyo kila kitu katika maisha yanayotuwezesha kupata pesa za kwenda kutazama michezo na burudani. Kumbuka ukiwa mgonjwa huwezi kufanya shughuli.

Vilevile unaweza usiwe mgonjwa, lakini pale unapokuwa na mwili usio na utimamu thabiti ni vigumu kuweza kutimiza majukumu ya kila siku ikiwamo kutembea kwenda kazini.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya duniani Afya (WHO), maana yake ni hali kamili ya ustawi kamili wa kimwili, kiakili na kijamii. Siyo tu kutokuwapo kwa magonjwa, bali inayohusisha uwezo wa kubadilika na kustawi.

DOKT 02

Afya ni hali inayoungwa mkono na mienendo na mtindo wa maisha, mazingira na miunganisho ya kijamii na kuwezesha ushiriki hai katika maisha ya kila siku.

Wakati utimamu wa mwili ni uwezo wa mwili kufanya kazi kwa ufanisi katika kazi za kila siku, michezo na dharura, unaoonyeshwa na nishati, nguvu na ustahimilivu bila uchovu usio wa lazima.

Utimamu unapatikana kupitia shughuli, lishe na kupumzika. Kwa kawaida unaojumuisha vipengele kama vile afya ya moyo, nguvu au ustahimilivu wa misuli, kunyumbulika na muundo wa mwili.

Inahusisha kuwa na nguvu za kutosha kwa ajili ya kazi, kucheza, burudani na hali mbalimbali zisizotarajiwa. Ieleweke pia si tu uwezo wa kushiriki michezo bali hata kazi za kila siku kama vile kutembea, kufanya kazi na kusoma.

DOKT 03

Maana hizo mbili zinatupa picha kuwa afya na utimamu ndio kila kitu kwa wachezaji, wasanii wa burudani na watazamaji au mashabiki. Ndio msingi wa mwili kutimiza majukumu yake.

Uwezo wa wachezaji toka kwa wachezaji wanaoshiriki Afcon ambao wanaotumika sana ikiwamo wale wa ligi kubwa mfano Mohamed Salah ni kwa sababu ya kuwa na afya njema na utimamu bora.

Pia katika burudani unamuona mwanamuziki kama Harmonize, Diamond, Marioo wanacheza kwa muda wa saa mciili mfululizo jukwaani ni kwa sababu ya vitu hivyo viwili.

Hivi sasa huwezi kumwona nguli wa mistari ya Rap Bongofleva, Joseph Haule ‘Profesa Jay’ akipanda jukwaani kuimba na kucheza na biti, hii ni kwa sababu hivi sasa ana tatizo la kiafya ambalo ni kikwazo.

Vilevile mwanamiziki mkongwe Hassan Rehani Bichuka, hivi sasa huwezi kumuona akipanda jukwaa la Sikinde kuimba pale bendi hiyo kongwe ikitumbuiza, hii ni kwa sababu za kiafya na utimamu.

DOKT 04

SABABU NA UMUHIMU WAKE

Unaweza kuwa na utimamu bora kimwili lakini usipokuwa na afya njema ikiwamo lishe duni au kuwa na afya njema, lakini si ustawi wa kitamaduni kama vile hali nzuri ya kiakili lakini uwezo mdogo wa kimwili.

Afya na utimamu vina faida za muda mrefu kwasababu husababisha maisha marefu na yenye nguvu zaidi, kupunguza hatari za magonjwa makubwa na kuboresha ubora wa maisha.


UHUSIANO WA AFYA NA UTIMAMU

Mazoezi ya kimwili ya kawaida huimarisha moyo wako, hujenga misuli, huboresha kimetaboliki, hudhibiti uzito na hutoa endorfini ambazo zote zikichangia afya bora ya kimwili na kiakili.

Mwili na akili yenye afya yaani lishe nzuri, mapumziko, msongo wa mawazo mdogo hutoa msingi na nishati inayohitajika kwa mafunzo bora ya mwili. Mfano mchezaji mwenye Afya ndio atakuwa katika kiwango kizuri.

Afya njema huwezesha utimamu wa mwili ambayo huwezesha kufanya mazoezi, ambayo huboresha afya zaidi, na kutengeneza mzunguko mzuri wa kiakili.

DOKT 05

FANYA HAYA UTOBOE

1.Pima afya na zingatia kanuni za afya angalau kwa mwaka upime afya mara mbili. Ukishindwa hata mara moja sio mbaya.

2.Fanya mazoezi mchanganyiko. Shirika la Afya Duniani (WHO) linapendekeza kutumia dakika 150 kwa wiki kwa ajili ya mazoezi ili kupata matokeo chanya kiafya.

3.Dhibiti uzito. Zingatia ulaji bora kwa kuepuka vyakula vyenye mafuta mengi na wanga au sukari nyingi.

4.Burudika, pumzika na lala angalau saa 8-10 kwa usiku mmoja.

5.Jihami na magonjwa ya akili. Unapoona dalili kama vile huzuni kubwa, mawazo ya muda mrefu, kujichukia, kuwaza kujizuru au kujiua fika mapema katika huduma za afya.

6.Epuka ajali na majeraha. Zingatia sheria za barabarani na mchezaji zingatia mbinu za kuepuka majeraha.

7.Jiunge na bima afya. Kuwa na bima ya afya kunakusaidia wewe na jamii yako katika kupata huduma bora za afya.

8.Jiimarishe kiimani, kijamii na ustawi. Hii inakupa utulivu wa akili.

9.Jenga mtandao wako wa huduma za afya, hakikisha angalau unajua vituo vya afya vilivyo jirani.

10. Epuka mienendo na mitindo mibaya kimaisha ikiwamo kutofanya mazoezi au shughuli, ulaji holela wa vyakula, unywaji pombe kupita kiasi na matumizi ya tumbaku. Shikamana na kanuni zote za afya za kujikinga na magonjwa.