Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

FILIMBI:Kifaa kidogo chenye kazi kubwa uwanjani

FILIMBI Pict

Muktasari:

  • Hadi leo tunaona baadhi ya watu hutumia mluzi ili kumwita mtu aliye mbali au kuelezea pahala alipo.

BINADAMU alipoona sauti yake haifiki mbali aliamua kutumia mluzi kwa kutumia mdomo wake na hii ilianza tokea dahari na enzi.

Hadi leo tunaona baadhi ya watu hutumia mluzi ili kumwita mtu aliye mbali au kuelezea pahala alipo.

Siku hizi kinachotumika sana ni filimbi ambayo kwa mujibu wa kumbukumbu za historia aina ya filimbi kama hizi tunazoziona leo katika michezo iliundwa zaidi ya miaka 5,000 iliyopita, lakini ukweli wa nani hasa aliiunda ya kwanza umejaa utata.

Filimbi ni nyenzo muhimu inayotumiwa na mwamuzi, lakini haizungumziwi habari zake isipokuwa maelezo juu ya mchezo, matokeo na habari za wachezaji.

Mambo yakienda na kupelekea kutokea vurugu ndio utaona habari za mwamuzi na mara nyingi hutupiwa lawama…lawama...lawama, kama vile yeye ndiye aliyewataka wachezaji waache kulisakta kabumbu na badala yake wagombane na hata kuchapana makonde.

Kinachowaponza waamuzi ni kufanya uamuzi mbalimbali ni namna walivyoitumia filimbi kusimamia mchezo.

Filimbi ni ndogo kwa umbo, lakini sauti yake katika mchezo ina nguvu kubwa na ni yenye historia ndefu.

Zipo simulizi nyingi juu ya filimbi, lakini nyingi zinaeleza kuwa fiimbi ya mwanzo ilivumbuliwa na kutumika China ya kale katika karne ya tatu, yaani miaka katika 2000 iliyopita.

Walitumia walinzi wa vijiji ambao waliokaa juu ya milima na kuzipuliza kwa nguvu kuwaonya wana vijiji juu ya uvamizi wa majeshi ya Wamongolia. Wakati ule kulikuwepo na uhasama  kati ya watu wa jamii hizi mbili ambazo zilipigana mara kwa mara na kusababisha maafa makubwa.

FILI 01

Hatimaye, Muingereza mmoja aitwaye Joseph Hudson wa Birmingham, akaja kuiingiza filimbi kutumiwa na waamuzi wa mchezo wa kandanda katika mwaka 1868 katika mchezo uliofanyika katika mji mdogo wa Nottingham Forest.

Kabla ya hapo wamuzi walitumia vitambaa vya mkono au bendera ndogo kuonyesha ishara za uamuzi wao na wakati mwengine mkono  kwa kuupunga au kupiga makofi au kupiga kelele.

Lakini walikuwapo waamuzi waliobeba ngoma ndogo walipoingia uwanjani na kuipiga kuelezea uamuzi wao.

Katika mchezo wa raga, William Atack, mwamuzi wa  New Zealand alikuwa wa kwanza kutumia filimbi katika mchezo huu mnamo mwaka 1884.

Kabla ya hapo waamuzi walitumia sauti zao na moja ya sifa ya kuwa mwamuzi zama zile ni kuwa na sauti kali kama ya bomba la kupazia sauti.

Tokea zama za kale filimbi zimekuwa za kila umbo, ukubwa, rangi na sauti. Filimbi za zamani zilitegemea zaidi pumzi za aliyepuliza na baadhi yao zilikuwa zikijaa mate hazifanyi kazi vizuri au hazitoi sauti.

FILI 02

Matatizo pia yaliibuka filimbi ilipolowa maji au kuwa na vumbi, lakini ukuaji wa teknolojia umesaidia kutengeza filimbi zisizokwa na matatizo hata mpulizaji akiimiminia shehena ya mate au udenda.

Tofauti nyingine ni kuwapo filimbi kwa michezo ya ndani na ile ya katika viwanja vya wazi.

Abraham Klein, mwamuzi mwandamizi wa kandanda wa Israel aliyechezesha michezo mingi ya kimataifa, ikiwa pamoja na fainali za Kombe la Dunia za Mexico 1970 na zile za Argentina   1978 alipostaafu miaka 40 iliyopita, alionyesha zaidi ya filimbi  100 alizotumia, zote zikiwa zinatofautiana.

Siku hizi zipo kila aina ya filimbi na bei zake ni kati ya shlingi 1,000 za Tanzania hadi shilingi 50,000. Kampuni maarufi itengenzayo filimbi za kisasa na ambazo hutumika katika mashindano ya kimataifa, kama Kombe la Dunia, ni Fox 40 International ya Canada.

Filimbi hizi ambazo ni za rangi mbalimbali zina milio na sauti tofauti kama vile tunavyoona kwa simu za mkononi.

Hapo zamani ilikuwa kawaida kuona mwamuzi kaweka filmbi mdomoni wakati wote kama mtoto anayenyonya chupa ya maziwa, lakini teknolojia imeondoa hili siku hizi.

FILI 03

Siku hizi filimbi huwekwa kwenye kiungo cha kiganja au shingoni na zipo ambazo hazipulizwi kwa mdomo bali kwa kubonyeza kitufe kama unavyofungua simu.

Katika siku za nyuma muamuzi aliingia uwanjani na filimbi moja tu, lakini siku hizi wengi huwa na ya akiba na yapo maelekezo ya wakati gani na vipi filimbi ipulizwe kuashiria kuanza mpira, panapokuwepo mchezo mbaya, mchezaji akiotea, linapoingia goli au kulikataa goli na vipi ipulizwe kuashiria mchezo umemalizika.

Waamuzi hushauriwa wasipulize filimbi ovyo na wafanye hivyo tu pale inapokuwa lazima kuchukua hatua.

Fikiria mchezo wa kandanda ungekuwaje hii leo kama ungechezwa bila ya kuwepo au  waamuzi au ungeendelea vipi kama ungechezwa bila ya filimbi.