Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dabi na madhara ya kiafya kwa mashabiki

DOKTA Pict

Muktasari:

  • Kwa Tanzania katika Ligi Kuu Bara upinzani wa jadi ni kati ya watani wa jadi Simba na Yanga maarufu kama ‘Kariakoo Derby’. Ndio mechi pekee inayobeba hisia za mashabiki nchini.

SOKA ni mchezo maarufu duniani wenye mamilioni ya mashabiki waliobeba hisia kali katika kushabikia timu zao hasa katika zile mechi kali maarufu kama derby zinazokutanisha wapinzani wa jadi.

Kwa Tanzania katika Ligi Kuu Bara upinzani wa jadi ni kati ya watani wa jadi Simba na Yanga maarufu kama ‘Kariakoo Derby’. Ndio mechi pekee inayobeba hisia za mashabiki nchini.

Kupenda timu na kuitazama inapocheza huku ikikupa matokeo chanya ni jambo la kufurahisha kwa wengi, lakini mambo huwa ovyo pale matokeo yanapokuwa mabaya.

Ni muhimu kutambua kwamba baadhi ya mambo yanayohusiana na mchezo huo yanaweza kuwa na athari mbaya kiafya ikiwamo mabadiliko ya hisia kabla ya mchezo, wakati unachezwa na baada ya mchezo.

Kawaida mabadiliko ya kimwili ya hisia huambatana na utiririshaji wa vichochezi vinavyoongeza kasi ya mapigo ya moyo ambayo yanaweza kuleta athari katika moyo.

DOKT 01

Hii ndio sababu kwa wale ambao tayari wana matatizo ya moyo ikiwamo shinikizo la damu kuweza kuwa katika hatari ya kupandwa shinikizo.

Kwa kawaida mwanadamu anapopenda jambo fulani humganda mwilini mwake ikiwamo kumkaa akili mwake.  Hali kama hii inaweza kumletea kuumia kihisia pale anapopata matokeo mabaya.

Mambo haya yanaweza kusababisha mwili kitiririsha vichochezi ambavyo huweza kuusababishia mwili kupata mshtuko ambao unaweza kusababisha kupoteza fahamu.

Leo tutaona baadhi ya athari za kiafya zinazohusiana na kupenda timu kwa hisia kali.

DOKT 02
  1. Kuongezeka kwa Shinikizo la Damu

Hii ni kutokana na Mfadhaiko, mechi za soka mara nyingi huamsha hisia kali, na mfadhaiko na msisimko unaohusishwa na kusaidia timu unayoipenda kushinda. kunaweza kusababisha ongezeko la muda la shinikizo la damu. Watu walio na matatizo ya moyo na mishipa ya damu wanapaswa kuwa waangalifu hasa na kudhibiti viwango vyao vya ushabiki.

Wakati shinikizo la damu la mtu linapoongezeka, uwezekano wa kupata kiharusi au mshtuko wa moyo huongezeka pia kwa wale ambao tayari wana tatizo la shinikizo la damu.


2.Vitafunio visivyofaa

Kuna ulaji holela wa vyakula na huwa ni ngumu kudhibiti wauzaji wa vyakula. Baadhi huwa hawazingatii kanuni za afya. Hapa inamweka shabiki katika hatari ya kupata magonjwa ya matumbo ikiwamo kuhara na kuumwa tumbo.

Kuna aina mbalimbali za vyakula vinavyovutia ikiwamo vyenye sukari na chumvi nyingi. Kuwa mwangalifu na vyakula hivi hasa wale ambao umri umekwenda.


3. Mshutuko wa kimwili

Kupoteza fahamu na kuzimia huwa ni kawaida kutokana na mwili kuwa katika shinikizo kubwa na huku pia kuwa hewa chache uwanjani. Vile vile na mabadiliko ya kihisia yanaweza kuchangia mwili kupata mstuko.

DOKT 03

4. Kelele na Sauti kubwa.

Athari za kelele na Kupoteza sauti ili kusaidia timu yako kwenye mchezo mara nyingi huhusisha kushangilia, kuimba, na kupiga kelele. Ingawa shauku ni muhimu kwa timu, unaweza kukaza sauti yako kwa nguvu na kusababisha mtetemo mkubwa na kudhuru tishu za eneo hilo hatimaye kupoteza sauti baada ya mchezo.

Vile vile kelele kubwa zinaweza kuchangia kuumwa kichwa na kuingilia kupata usingizi hapo baadaye.


5. Hisia kali na Ustawi wa Akili

Mechi za soka zinaweza kuleta hisia kali, na matokeo ya michezo yanaweza kuathiri kiasi kikubwa hisia za mashabiki.

Ni muhimu kukumbuka kuwa mwisho wa yote, mpira wa miguu ni mchezo tu. Ingawa ni kawaida kuhisi umewekeza kibinafsi kupita kiasi hivyo kujihisi ni mwenye deni. Msongo wa mawazo na huzuni kali vinaweza kuwa na athari kubwa kiafya. Ikiwa unapata matatizo yoyote ya afya ya akili ambayo yanasababishwa na soka.

Afya ya akili ndio huathirika zaidi ikiwamo kupata msongo wa mawazo shinikizo la akili, sonona, hofu kali, kukosa utulivu na mpasuko wa kihisia na kisaikolojia.

Vile vile kupata hisia mbaya za kujizuru na kujitenga.

DOKT 04

6. Matatizo ya kitabia

Mabadiliko ya kitabia, kutokana na kuchanganyikiwa na kugandwa na huzuni kali inaweza kukufanya kuwa tabia za hasira, unywaji wa pombe kupita kiasi au matumizi ya tumbaku.


7. Ukosefu wa usingizi

Hali hizo zinaweza kusababisha matatizo ya kihisia na kiakili, huweza kuambatana na kichwa kuuma, uchovu mkali na kuchoka. Hali hii inaweza kumfanya mtu kukosa umakini katika kufanya uamuzi sahihi katika maisha yake ya kila siku.


8. Kukosa hamu ya kula

Ni kawaida mwili wa mwanadamu unapopata huzuni kali huweza kumfanya mtu kukosa hamu ya kula.

DOKT 05

9. Kuumwa kusiko na sababu

Kupata hisia mbaya na mvurugiko wa akili vinaweza kumfanya mtu kuumwa lakini sababu isijulikane. Na hata anapopimwa hukutwa hana yale magonjwa ambayo yanaambatana na dalili alizonazo. Hali hii inakuwa ni kuathirika kiakili zaidi.


10. Msongamano na magonjwa ya mfumo wa hewa

Endapo kutakuwa na mashabiki wenye magonjwa ya mfumo wa hewa ikiwamo mafua ya msimu huwa ni rahisi kuyapata katika mazingira ya michezo ya derby kutokana na kuwa na msongamano mkubwa wa watu.


Chakua hatua hizi


1.Ushauri nasaha

Ni muhimu kuwasiliana na rafiki, mwanafamilia au mtaalamu saikolojia au daktari wa magonjwa ya akili kwa ushauri nasaha.


2. Pumzika, lala na burudika

Pumzika maeneo tulivu yasiyo na kelele, lala angalau kwa saa 8 na pata burudani kama vile ya muziki au kuangalia filamu. Epuka na kujitenga na kukaa peke yako. Kufanya hivyo kunazidisha hisia hasi ikiwamo huzuni hasira. Jichanganye katika mazingira mazuri ili kupeperusha shinikizo la akili na msongo wa mawazo.

DOKT 06

3. Kula lishe bora na kunywa maji

Kipindi unapopatwa na hisia hasi ni muhimu kuhakikisha unapata lishe iliyosheheni makundi yote ya vyakula ikiwamo mboga mboga na matunda na hakikisha unakunywa maji mengi. Lishe inasawazisha athari za kiafya zilizojitokeza na huku ikikupa kinga imara.

Ili kuepuka hili. Kunywa maji na kuepuka kupiga kelele kwa muda wa dakika 90 husaidia kulinda sauti yako wakati bado unafurahia hali ya mechi.


4. Fanya mazoezi mepesi na shughulisha mwili

Wakati wa huzuni kali au msongo wa mawazo ni vizuri kufanya mazoezi mepesi ikiwamo kutembea, kukimbia, kuendesha baiskeli na fanya shughuli ikiwa kazi za bustani na usafi wa nyumba


5. Fanya na saidia shughuli za kijamii

Pamoja ya kuwa mpira umebeba hisia zako lakini kumbuka huo mpira ni burudani na ni raha zaidi timu yako inapokupa matokeo chanya. Kubaliana na hali, badala yake jichanganye na mambo ya jamii ikiwamo kushiriki usafi wa mazingira ya jamii na kusaidia vituo vya malezi kama vile yatima. Hii inakupa mbadala wa furaha na kupoteza hasira za timu yako kufanya vibaya.