Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CHILUNDA: Aliyening'oa Simba huyu hapa

Chilunda Pict

Muktasari:

  • Kiungo huyo mshambuliaji hakuweza kupata namba chini ya Robertinho kutokana na kumtaka apunguze uzito kutokana na kujiunga na timu hiyo akiwa ametoka nje ya uwanja kuuguza majeraha ya goti.

SHAABAN Idd Chilunda lilikuwa miongoni mwa majina yaliyoibuka kwenye usajili wa Simba msimu wa 2023 chini ya kocha Roberto Oliveira 'Robertinho', lakini hakuweza kudumu kikosini humo akiishi kwa miezi sita pekee baada ya kutolewa kwa mkopo.

Kiungo huyo mshambuliaji hakuweza kupata namba chini ya Robertinho kutokana na kumtaka apunguze uzito kutokana na kujiunga na timu hiyo akiwa ametoka nje ya uwanja kuuguza majeraha ya goti.

Lakini unaambiwa uamuzi wa kuondoka kwake Simba haukuwa chini ya Robertinho kwasababu na yeye kwa wakati huo alikuwa ameondolewa Simba na nafasi yake kuchukuliwa na Abdelhak Benchikha.

Mwanaspoti limefanya mahojiano na kiungo huyo mshambuliaji wa KMC aliyejiunga na timu hiyo kupitia dirisha dogo la usajili amefunguka mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sababu iliyomfaya ang'olewe katika kikosi cha Simba akimtaja Benchikha kuwa alihusika.

Licha ya usajili wake kushtua, hata hivyo, kwenye kikosi cha Simba hakuwa na nafasi na hadi anapewa mkono wa kwa heri, alikuwa amecheza dakika 17 tu. Ni chache. Hata hivyo, licha ya kuwepo mastaa wengine waliocheza dakika chache zaidi wakiwamo Husseni Abeli, Hussein Kazi, lakini uwezo wake ni dakika chache.

Alicheza dhidi ya Tanzania Prisons akipewa dakika moja tu, baada ya kuingia akitokea benchi Simba ikishinda mabao matatu na alicheza tena kwenye mechi dhidi ya Ihefu FC kwa dakika 16 timu yao ikishinda mabao 2-1.

"Sikuwa na maelewano mazuri na kocha kwa sababu alikuwa ananilazimisha nicheze kiungo mkabaji eneo ambalo nilikuwa siliwezi naumia lakini sikupewa nafasi ya kusikilizwa zaidi nililazimishwa nipambane," anasema na kuongeza;

"Nakumbuka nilicheza mechi moja Mapinduzi nilikuwa timamu lakini baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza nilitoka natetemeka kutokana na kutumia nguvu nyingi tofauti na nafasi niliyoizoea kucheza."

Chilunda anasema baada ya kuona hivyo aliamua kumuambia kocha kuwa nafasi hiyo haiwezi majibu aliyopewa ni kwamba kama hawezi kucheza nafasi hiyo basi hana nafasi kikosioni kwake.

CHILU 01

"Nilisaini mkataba wa mwaka mmoja na Simba wenye kipengere cha kuongeza lakini sikuwa na msimu mzuri kwasababu nilikuta timu ipo kwenye changamoto ya kutengeneza timu," anasema;

"Kutokana na presha iliyokuwepo pale haikuwa raisi mimi kupewa nafasi ya kucheza kwasababu wageni ndio walikuwa wanaaminiwa zaidi na timu ilikuwa inataka matokeo zaidi ya kumpa nafasi mchezaji."

Anasema hakuaminiwa kabisa hivyo alikosa nafasi ya kucheza lakini anaamini angepata nafasi ya kuonyesha hadi muda huu angekuwa bado ndani ya kikosi cha Simba.


ISHU YA FEI TOTO

Chilunda akilia kuhamishwa namba kuwa ndio sababu ya kutoka ndani ya kikosi cha Yanga ameibuka na kutolea ufafanuzi utofauti wa kuhamishwa nafasi aliyokuwa anacheza na kupelekwa nyingine na Feisal Salum 'Fei Toto' kumudu kuhamishwa nafasi.

"Fei Toto alitoka kukaba na kuletwa kushambulia hauwezi kuwa na changamoto sana ametoka kukaba kasogezwa mbele ana mpango wa kukaba kidogo na kushambulia tofauti na kutoka kushambulia hadi kukaba," anasema Chilunda na kuongeza;

CHILU 02

"Kwa upande wa Fei Toto ni sawa na kutoka kwenye umaskini na kupelekwa kwenye utajili kwasababu amepunguziwa majukumu aliyokuwa nayo awali yalikuwa ni magumu sana lakini pia nafasi aliyopelekwa haina utofauti mkubwa na aliyokuwa anafanya utofauti ni kukaba sana na kushambulia sana."

Akitolea ufafanuzi zaidi Chilunda anasema mshambuliaji anaeneo dogo sana la kucheza tofauti na kiungo mkabaji ambaye anatakiwa kufanya majukumu makubwa uwanjani kwa kuhakikisha anaulinda ukuta wake uliruhusu mabao.

"Mshambuliaji kutoka kushambulia kushushwa chini ni sawa na kutoka kwenye utajiri kwenda kwenye umasikini hauwezi kuwa na kazi nzuri na bora kama mwanzo."

CHILU 03

DUBE, ATEBA HABARI NYINGINE

Licha ya eneo la ushambuliaji kukosa nyota wengi lakini Chilunda amewataja nyota wa ndani na wa kigeni wanaocheza Ligi Kuu Bara kuwa ni wachezaji wanaofanya vizuri eneo hilo kwa sasa licha ya wengi kukosa imani nao.

"Kwenye ligi kuna washambuliaji wengi wanaofanya vizuri navutiwa na Prince Dube, Leonel Ateba kwa upande wa wageni wamekuja kuongeza changamoto kwetu na wanatufanya tupambane ili tuweze kuwa bora," anasema na kuongeza;

"Kwa upande wa wazawa kuna Clement Mzize na Seleman Mwalimu 'Gomez' wanavipaji na wanatubeba sana kutokana na kile wanachokifanya wamekuwa bora na wanaonyesha ushindani kwa nyota wa kigeni."

Chilunda anasema Gomez ameonyesha uwezo mkubwa kwa miezio sita pekee aliyocheza Ligi Kuu Bara na kupata nafasi ya kutoka Tanzania hii ndio maana halisi ya kipaji na vipo vingi tu shida ni kukosa nafasi kama ilivyotokea kwa nyota huyo.

CHILU 03 (1)

AZAM ILIMRUDISHA BONGO

Wakadi wadau wengi wakiamini kuwa Chilunda alirudi Tanzania akitokea soka la Hispania alishindwa kuendekea kucheza huko mwenyewe amefunguka sababu.

“Kuna kitu watu wengi hawafahamu mimi sikurudi Tanzania kwa kupenda Azam walinirudisha kwasababu walinipeleka kwa mkopo Tenerife ya Hispania baada ya mkataba wangu wa mkopo kuisha nilitakiwa kurudi,” anasema na kuongeza;

“Lakini naweza kusema kurudi kwangu Tanzania ni mipango ya Mungu alipenda iwe ivyo na sikuwa na mamlaka ya kurudi au nisirudi lakini hayakuwa matakwa yangu sababu kubwa mimi nilikuwa mchezaji wa Azam FC,” anasema.

Chilunda anasema baada ya kurudi Azam FC hakumaliza msimu alipata bahati ya kuuzwa tena Botola ambapo hakupata nafasi ya kucheza kutokana na kulipwa fedha zake.

“Botola nilicheza msimu mmoja nikawa nadai fedha zangu nilikaa nao chini wakagoma kulipa nikaenda FIFA ambapo ndio kimbilio letu mimi nacheza mpira ili nilipwe nisingeweza kukubali kuacha,” anasema na kuongeza;

“Baada ya kukimbilia FIFA nilikaa nje zaidi ya miezi saba kutokana na kesi huwezi kusaini timu nyingine ukiwa na mashtaka kwenye chombo hicho cha haki za wachezaji nilihisi nimefanya makosa lakini ilikuwa sahihi kwasababu nilikuwa napigania haki yangu.”

CHILU 05

MECHI MOJA MSIMU MZIMA

Baada ya kukaa nje kwa miezi nane Chilunda anasema alipata nafasi tena ya kujiunga na Azam FC lakini maisha yake hayakuwa mazuri kutokana na kuumia mwanzoni mwa mkataba wake.

"Nakumbuka baada ya kusaini mkataba na Azam FC nilicheza mechi moja tu ya Mapinduzi Cup Zanzibar sikumaliza dakika 90 baada ya bao tu niligusa mpira mara mbili nikaumia nikakaa nje miezi mitano,” anasema na kuongeza;

“Niliumia goti la kushoto ambalo liliniweka nje ya uwanja kwa miezi mitano nilipopona nikarudi sijakaa sawa nikaumia tena goti la kulia nilikaa miezi mitatu baada ya kupona nikarudi uwanjani mkataba ukaisha hivyo mkataba mzima nilicheza mechi moja.” Anasema Chilunda ambaye amethibitisha kupunguza kilo kutoka 76 hadi 72.


KIDOGO TU AKIPIGE NA HIMID

Wakati mastaa wengi ndoto zao zikiwa ni kupata nafasi ya kucheza soka la kulipwa nje ya Tanzania kwa upande wa Chilunda mwenyewe anasema kwake ni uwezo tu akiwa fiti tu anaondoka.

“Majeraha ndio adui yangu mkubwa kabla ya kujiunga na Simba nikitokea Azam FC nilipata ofa ya kwenda Misri, timu ya Ghazl El Mehalla timu ambayo anacheza kiungo wa kitanzania Himid Mao lakini mambo hayakwenda vizuri,” anasema na kuongeza;

“Baada ya kumaliza mkataba na Azam FC nilikuwa nafanya mazoezi binafsi kujiweka fiti maana nilimaliza mkataba na Azam kipindi cha dirisha dogo nisingeweza kukaa tu katika harakati za kufanya mazoezi binafsi niliumia tena na tayari nilikuwa nimeshasaini mkataba wa awali na Ghazl El Mehalla.

Chilunda anasema baada ya kuumia akiwa tayari amebakiza siku tano kwenda kuungana na timu hiyo ndio ukawa mwisho wake kwenda kucheza kwenye timu hiyo, alifanikiwa kujitibia na kurudi katika hali yake ya kawaida na ndipo alipopata ofa ya kujiunga na Simba ambayo hata hivyo hakuwa na msimu mzuri.


CHAMA, AJIBU WANAJUA BOLI

Mpira ni burudani, mpira ni furaha na raha ya soka upate mchezaji au timu inayocheza mpira wa kupasiana pasi nyingi hadi kufika golini kama anavyothibitisha Chilunda kuwa yeye ni muhumini wa mpira mzuri na amekuwa akiucheza.

"Mpira una raha yake hasa ukipata wachezaji wanaoucheza vizuri na kuufanya kuwa rahisi mimi nafurahishwa na nyota wote wanaoucheza vizuri mpira nikisema niwataje wote sitamaliza leo kwasababu ni wengi," anasema na kuongeza;

"Mfano navutiwa na Clatous Chama, Ibrahim Ajibu na mastaa wengine wengi wanaoufanya mpira kuwa mchezo rahisi ukiwaangalia unaburudika na unaupenda mpira."

Chilunda anasema Tanzania imebarikiwa vipaji hivyo amekuwa akishuhudia sio kwenye ligi tu bali ata kwenye mechi za mchangani ameshuhudia nyota wengi bora ambao anabaki anajiuliza imekuwaje wanacheza huko.


KUFUNGA SIO MCHEZO

"Kuweka mpira kwenye nyavu sio kitu rahisi na ndio maana kwa asilimia kubwa washambuliaji wanalipwa fedha nyingi, naamini kukosekana kwa wachezaji wengi eneo hilo inaweza ikawa inachangiwa na wachezaji wengi kukimbia eneo hilo," anasema na kuongeza;

"Mchezaji anaweza akapewa nafasi ya kucheza eneo la mwisho akafanya vizuri na baadae akapotea kwenye ramani ndio mpira sio rahisi kwa mchezaji kuwa bora misimu minne au zaidi japo wapo wachezaji wa aina hiyo lakini inategemea na timu aliyopo na nafasi anayoipata hii pia inaweza ikawa sababu ya kupotea kwa washambuliaji."

Anasema lakini pia wachezaji wamekuwa wakikimbia kutokana na ugumu wanaokutana nao akifafanua kuwa mchezaji anapata nafasi ya kucheza eneo hilo kutokana na kukosa nafasi mara kwa mara na maneno makali ya mashabiki bila kujua mchezaji anapitia nyakati gani anaamua kuhama nafasi.

"Kuna muda mchezaji anaambiwa na kocha anakupa majukumu ya kufanya ambayo sio kila mdau wa soka atatambua ni kazi kani umepewa anaibuka na kuzungumza maneno makali mchezaji gani amekaa tu uwanjani hakuna anachofanya kumbe kocha kakwambia wewe kazi yako ni kufunga tu au unamkaba mtu fulani lakini maneno yanakuwa mengi nje ya uwanja."