Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Carlos Alcaraz avunja rekodi ya Djokovic

ALCAREZ Pict

Muktasari:

  • Mhispania huyo amekusanya pointi 12,050 mwaka huu ikiwa ni 20 zaidi ya zile alizokusanya Djokovic 2020 alipoibuka mbabe kwa ubora msimu huo upande wa wanaume.

MIAMI, MAREKANI: SUPASTAA wa tenisi duniani, Carlos Alcaraz amevuka rekodi ya pointi za Novak Djokovic kwa msimu mmoja, baada ya kufanya kazi kubwa uwanjani katika mashindano.

Hii inamfanya kuwa mchezaji namba moja duniani kwa sasa akiongoza kwa viwango vya alama kwa mara ya pili katika kazi yake.

Mhispania huyo amekusanya pointi 12,050 mwaka huu ikiwa ni 20 zaidi ya zile alizokusanya Djokovic 2020 alipoibuka mbabe kwa ubora msimu huo upande wa wanaume.

Licha ya kuwa na msimu wa mafanikio makubwa, Alcaraz ameshindwa kufikia alama 12,410 zilizofikiwa na Andy Murray 2016 aliyekuwa kinara kwa ubora.

ALCA 01

Alcaraz amemaliza mbele ya staa namba mbili duniani kwa ubora, Jannik Sinner ambaye amevuna alama 11,500, licha ya kwamba mpinzani wake huyo mwaka huu alikuwa bora zaidi.

Hata hivyo kuna pengo kubwa kati ya nyota aliyeshika namba mbili na yule aliyekamata tatu, ambapo Alexander Zverev amemaliza na pointi 5,160 ikiwa ni alama 6,300 pungufu ya zile alizokusanya Muitaliano Sinner.


WAWILI WALIOTAWALA

Viwango vinaonyesha viwango ambavyo Alcaraz na Sinner wamekionyesha msimu huu kilikuwa kikubwa wakishinda kwa pamoja mashindano manane kati ya tisa ya Shirikisho la Tenisi Duniani (ATP) yenye alama nyingi zaidi.

Alcaraz ndiye mchezaji wa kwanza wa kiume kumaliza msimu akiwa na zaidi ya alama 12,000 tangu Djokovic miaka mitano iliyopita. Na cha kuvutia zaidi ni kwamba amevuna asilimia 88 ya alama zake (10,640) kati ya Aprili na Novemba.

ALCA 02

Alcaraz, Sinner, na Zverev ndio mastaa watatu wa pili katika karne hii kumaliza msimu wakiwa nafasi tatu za juu mfululizo kwa miaka miwili. Mara ya mwisho ilikuwa ni kwa utatu wa Rafael Nadal, Roger Federer na Djokovic.


APIGWA KITU KIZITO

Maajabu hayo yamekuja kama habari njema baada ya Alcaraz kuadhibiwa kwa kutoshiriki mashindano ya ATP Masters 1000.

Mhispania huyo alipoteza zaidi ya Pauni 1.8 milioni katika zawadi kutokana na kutokuwepo na hivyo kujikuta akiadhibiwa na ATP kutokana na sheria kali kwa nyota wanaoamua kutoshiriki michuano mikubwa.

Alcaraz alitarajiwa kuvuna Pauni 3.6 milioni, lakini ukiukaji wa sheria hiyo hupunguza zawadi za mchezaji kwa asilimia 25 kwa kila mashindano ya Masters 1000 anayoyakosa kutokana na kujiondoa au kuumia hadi kiwango cha juu cha michuano mitatu.

ALCA 03

Kisha, kuanzia mashindano ya nne anayokosekana zawadi za fedha hupunguzwa kwa asilimia 100. Alcaraz alikosa Canada Open majira ya kiangazi kabla ya kugoma kushiriki Shanghai Open mwishoni mwa Septemba jambo linalomaanisha ataambulia Pauni  1.8 milioni yaani nusu ya zawadi ya jumla.

Mhispania huyo alitwaa mataji saba 2025 ikiwa ni pamoja na Grand Slam mbili. Alishinda French Open kabla ya US Open mwezi Septemba. Kulikuwa pia na mafanikio zaidi kwa Alcaraz baada ya kubeba mataji ya Paris, Rome, Monte-Carlo na Cincinnati.