Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Balaa la Bruno Fernandes Manchester United!

BRUNO Pict

Muktasari:

  • Akiwa na asisti 12 kwenye Ligi Kuu England msimu huu na bado kuna mechi 14 za kucheza, supastaa huyo na nahodha wa Manchester United yupo katika nafasi kubwa ya kuvunja rekodi iliyodumu kwa miaka mingi kwenye ligi hiyo ya asisti 20 ndani ya msimu mmoja.

MANCHESTER, ENGLAND: BRUNO Fernandes hachezi mpira. Bali anafikiria mpira. Kwa kile anachokifanya ndani ya uwanja, basi tu hapewi sifa anazostahiki. Mreno huyo ni fundi wa boli na mara zote amekuwa akifanya mambo magumu kuonekana kuwa mepesi uwanjani.

Akiwa na asisti 12 kwenye Ligi Kuu England msimu huu na bado kuna mechi 14 za kucheza, supastaa huyo na nahodha wa Manchester United yupo katika nafasi kubwa ya kuvunja rekodi iliyodumu kwa miaka mingi kwenye ligi hiyo ya asisti 20 ndani ya msimu mmoja.

Rekodi hiyo ya mastaa walioasisti mara nyingi msimu mmoja wa Ligi Kuu England inashikiliwa na Thierry Henry na Kevin De Bruyne, walioingia kwenye vitabu vya kihistoria baada ya kuasisti mara 20 kila mmoja.

Na Fernandes, ambaye aliisaidia timu yake ya Man United kuichapa Fulham mabao 3-2 katika mchezo wa Ligi Kuu England uliofanyika Old Trafford, Jumapili, ameweka rekodi ya kuasisti mfululizo katika mechi tano za mwisho.

Staa huyo ameasisti mara sita katika mechi tano za mwisho, hiyo ni rekodi nyingine kabisa ya kibabe kutoka kwa mkali huyo.

BRU 01

Kwa Fernandes haya si makali tu ya msimu huu, staa huyo imekuwa kawaida yake tangu alipojiunga na Man United na amekuwa akichangia walau mabao 23 katika kila msimu alitumikia miamba hiyo ya Old Trafford tangu alipotoka Sporting Lisbon.

Lakini, msimu huu, Fernandes anaonekana kuwa kwenye kiwango chake bora zaidi katika maisha yake ya soka akiwa Man United, ambayo kwa sasa ipo kwenye mchakamchaka wa kufukuzia tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, ikishika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Kwenye msimamo huo, Man United imeachwa nyuma pointi tano na timu inayoshika nafasi ya tatu, Aston Villa na pointi sita dhidi ya timu inayoshika nafasi ya pili, Manchester City, huku ikiwa nyuma ya vinara Arsenal kwa pointi 12.

Bado kuna pointi 42 za kupambania kabla ya ligi kufika tamati, huku Man United ikionyesha matumaini makubwa kwa kushinda mechi tatu mfululizo chini ya Michael Carrick.

Lakini, kitu kikubwa anachotambia kocha wa muda wa Man United, Carrick kwa sasa ni ubora wa kiungo wake, Fernandes, ambaye asisti zake 12 alizopiga hadi sasa, zinamfanya ashike namba moja kwenye Ligi Kuu England.

Fernandes kwenye asisti hizo, saba zilitokana na mipira iliyokufa, kipengele ambacho anashika namba moja pia.

BRU 02

Fernandes ametengeneza nafasi 68 za mashambulizi ikiwamo asisti, kipengele ambacho pia anashika namba moja. Katika nafasi alizotengeneza ambazo hazikuhusisha mpira iliyokufa, Fernandes alifanya hivyo mara 45 na kushika namba moja pia kwenye Ligi Kuu England msimu huu.

Fundi huyo wa boli, Fernandes ametengeneza nafasi kubwa za mashambulizi 16 katika mechi ambapo kwenye kipengele hicho anashika namba moja pia, sawa na anavyoshika namba moja kwenye wachezaji waliopiga pasi nyingi za kupenyeza kwenye Ligi Kuu England msimu huu, akifanya hivyo mara 21.

Fernandes amekuwa mtamu balaa kwa msimu huu, huku asisti zake sita alizotoa katika mechi tano mfululizo za mwisho, amefanya hivyo dhidi ya Burnley, Brighton, Man City, Arsenal na Fulham, alipoasisti mara mbili, bao la Casemiro la kwanza na la Benjamin Sesko la ushindi kwenye dakika za majeruhi.