Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Baada ya Stephane Aziz Ki, mpira apewe Chama

CHAMA Pict

Muktasari:

Sasa Aziz ameondoka Yanga, nafasi yake kama siyo Chama, anaweza kuichukua Pacome. Na kama wakianzishwa wote, takwimu zinaonyesha wanatisha sana pamoja.

NI wakati wa Clatous Chama sasa kuonyesha rangi zake halisi katika dakika 360 baada ya Stephane Aziz Ki kuondoka Yanga kwa sababu kuna uhusiano mkubwa wa kuuzwa kwa staa huyo wa Burkina Faso, mipango ya kurudishwa Jangwani kwa Feisal Salum na mabalaa ya Pacome Zouzoua anapocheza kama namba 10.

Kivipi? Twende pamoja… Tetesi za Aziz Ki kusajiliwa Yanga zilipoanza, wengi walidai kwamba staa mkubwa wa hadhi yake kamwe hawezi kuja kucheza soka Bongo. Alipokuja, wakasema uwezo wake ni kama homa za vipindi zinapanda na kushuka na alipofunga mabao kwa mashuti yake ya mbali, walisema atawachonganisha sana makipa na klabu zao.

Yote haya hayakuwahi kumrudisha nyuma, Stephane Aziz Ki bali yalimjenga kuwa imara zaidi. Ndio maana haikushangaza aliposhinda tuzo ya MVP ya mwanasoka bora wa msimu, Mfungaji Bora wa Ligi Kuu Bara, hata alipooa Mtanzania na kuuzwa kwa pesa ndefu kwenda kucheza Kombe la Dunia la Klabu huko Marekani. Ndani ya muda mfupi wa miaka mitatu tu, Aziz Ki amefanya mengi makubwa ya kukumbukwa katika soka la Tanzania.

Nyota wa kimataifa wa Burkina Faso, Aziz Ki amejiunga na klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco kwa ada ya uhamisho inayotajwa kuwa ni Sh2 bilioni na ameruhusiwa kuondoka kabla ya msimu kumalizika huku timu yake ya Yanga ikiwa imebakisha mechi tatu, ikiwamo moja dhidi ya wapinzani wao wakubwa wa mbio za ubingwa msimu huu, Simba. Yanga inaongoza Ligi Kuu Bara kwa pointi 73, nne juu ya Simba ambayo ina mechi moja mkononi ukilinganisha na Yanga.

CHAM 01

Kutokana na umuhimu wake,  hasa kwa mambo anayoyafanya katika mechi za dabi, kuruhusiwa kuondoka sasa kunachochea uvumi wa “hatuchezi” ambao umekuwa ukienezwa na upande wa timu yake ya wananchi kuhusu mechi dhidi ya Simba iliyopangwa kufanyika Juni 15. Kuondoka kwa Aziz Ki kunaacha pengo katika kikosi cha Yanga ambacho pia kinakabiliwa na fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya mshindi wa nusu fainali ya pili itakayoikutanisha Simba na Singida Black Stars.

Kwa dau linalotajwa la Sh2 bilioni ingekuwa ngumu kwa klabu yoyote ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, kuacha kumuuza mchezaji wake aliyebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake, huku pia ofa inayotajwa ya mshahara wa Sh72.3 milioni kwa mwezi aliyowekewa Aziz katika mkataba wake wa miaka miwili na wababe hao wa Morocco, ni wazi ingemtoa mchezoni kama Yanga ambayo ilikuwa ikimlipa Dola 13,000 (sawa na Sh34.9 milioni) ingejaribu kumng’ang’ania.

Pesa ni sabuni ya roho, inaweza kununua chochote na yeyote, muhimu ujue bei yake tu. Sasa, kwa kuingiza mkwanja wa Sh2 bilioni, Yanga bila shaka inaweza kumnunua Feisal Salum ‘Fei Toto’ ambaye ilimuuza kwa Azam mwaka 2023, arejee kuziba pengo la Aziz.

Yanga inatajwa kujiandaa kumpa mkononi Fei Sh800 milioni na mshahara wa Sh40 milioni kwa mwezi ili asaini katika klabu yake hiyo ya zamani iliyompa umaarufu mkubwa.

CHAM 02

Lakini kabla ya juhudi zozote za kumsajili Zanzibar Finest, Yanga kwa kumuuza Aziz inaacha mwanya kwa mastaa wawili Clatous Chama na Pacome Zouzoua wakubwa waliopo kikosini humo kuonyesha makali yao.


CLATOUS CHAMA

Mara nyingi kikosini, alianzishwa Aziz Ki na kuzua maneno kwamba Clatous Chama ambaye alitua mwanzoni mwa msimu huu akitokea kwa watani Simba, hana furaha Jangwani.

Na pia mara nyingi alipofanyiwa mabadiliko Aziz, aliingia Chama na kuwasha moto ule ule. Pengine mashabiki wanakumbuka Mwamba wa Lusaka alivyohusika katika mabao sita kati ya mabao 10-0, ambayo Yanga ilishinda katika mechi mbili dhidi ya Vital’O za hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu akifunga mawili na kutoa asisti nne. Alikuwa wa moto sana akianzishwa pamoja na Pacome. Bara hadi sasa msimu, Chama amehusika katika mabao 6, akifunga manne na asisti mbili.

Katika mechi ya kumuaga Aziz, ambayo ilikuwa ni nusu fainali ya Kombe la Shirikisho, Yanga ilishinda 2-0 dhidi ya JKT  Mei 18, 2025, Tanga. Aziz alitoka, Chama akaingia. Ni ‘sub’ iliyojirudia iliyokuwa maarufu ya mara kwa mara msimu huu.

Wakati presha za mashabiki wa Yanga zikianza kupanda kutokana na kuongoza kwa bao 1-0 huku JKT wakiongeza mashambulizi ya kushtukiza na dakika zikienda ukingoni, Pacome, ambaye pia aliingia sub, aliuwahi mpira ulionasa kwenye maji, ambao ulionekana kama umetoka.

Akapiga “vii-pasi” kwa Chama. Mwamba wa Lusaka katika ule utulivu wake uliozoeleka na kumpa heshima kubwa awapo jirani na lango, alimpitishia mpira njiani Mudathir Yahya ambaye alikuwa anakuja mbio kutokea nyuma yake upande wa kulia na kiungo huyo wa Zanzibar akaweka chuma ya pili iliyowahakikishia Yanga kwenda fainali ya nne mfululizo ya michuano hiyo iliyotwaa taji lake mara zote tatu zilizopita. 

CHAM 03

Kama ‘sub’ yake inavyoonyesha, “Aziz anatoka Chama anaingia,” hiki ndicho kitu kinachotarajiwa kutokea Yanga baada ya staa huyo wa Burkina Faso kuondoka nchini. Chama anatarajiwa kuimiliki ile Namba 10 kikosini, angalau kwa mechi chache zilizobaki kumalizia msimu. 

Lakini tatizo ni kwamba Chama alisaini mwaka mmoja tu katika mkataba wake Jangwani akitokea Msimbazi, ambako alifanya mambo makubwa ya kukumbukwa.

Hii ina maana gani? Kama ni kweli Chama hakuwa na furaha msimu mzima, halafu akija kuwasha moto katika mechi hizi chache za kumalizia msimu, na huku Yanga ikiwa bado haina uhakika wa kumpata Fei Toto, ni wazi Mwamba wa Lusaka atakuwa na nguvu kubwa katika mapatano ya kuongezwa mkataba mpya.  Yanga italazimika kuvunja benki kumbakisha licha ya msimu mzima kuonekana nafasi yake kikosini ni ndogo.  Dakika za ‘jiooni’ Chama anaweza kubadilisha upepo.


PACOME ZOUZOUA

Wakati anakuja kutokea kwenye Ligi Kuu ya Ivory Coast, Pacome, alitokea kushinda tuzo ya MVP wa ligi hiyo.

Pacome alikuwa akicheza Namba 10 katika klabu yake ya zamani ya Asec Mimosas akirithi nafasi iliyoachwa na Aziz Ki alipotimka kutua Yanga.

Aziz alikuwa MVP mwaka uliotangulia, Pacome aliporithi nafasi hiyo msimu uliofuata akawa MVP kisha naye akamfuata Aziz Ki Yanga.

Sasa Aziz ameondoka Yanga, nafasi yake kama siyo Chama, anaweza kuichukua Pacome. Na kama wakianzishwa wote, takwimu zinaonyesha wanatisha sana pamoja.