Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Aziz KI v Ahoua… Hapa kuna vita nzito

Kazi Pict

Muktasari:

  • Wawili hao wanacheza nafasi moja utofauti ukiwa ni timu na Ahoua amemtupa Aziz Ki kwa mbali akihusika kwenye mabao 15 akifunga 10 na kuasisti tano, huku Aziz Ki akifunga matano na kuasisti saba.

NAMBA haziongopi. Ndivyo unavyoweza kusema kutokana na namba za kiungo wao mshambuliaji wa Simba, Jean Charles Ahoua akimfunika MVP na mfungaji bora msimu uliopita, Stephane Aziz Ki.

Wawili hao wanacheza nafasi moja utofauti ukiwa ni timu na Ahoua amemtupa Aziz Ki kwa mbali akihusika kwenye mabao 15 akifunga 10 na kuasisti tano, huku Aziz Ki akifunga matano na kuasisti saba.

Ahoua aliyesajiliwa na Simba akitokea Stella Club d’Adjame ya kwao Ivory Coast amekuwa na msimu mzuri hadi sasa akiwa na mabao 10 ana jambo lake huku timu yake ikiwa imesaliwa na michezo 11 kabla ya Ligi Kuu kumalizika.

Ujio wa Ahoua Simba ulimfanya awe mmoja wa nyota wa tatu waliotoka Ivory Coast wakiwa MVP baada ya Aziz KI msimu wa 2022-2023 na Pacome Zouzoua msimu wa 2023-2024 ambao wote wapo Yanga wakitokea ASEC Mimosas. Hata hivyo, vitani yuko na MVP wa ligi kuu msimu uliopita ambaye amemuacha mbali.

KZ 01

Ipo hivi. Nyota huyo amekuwa na mchango mkubwa Simba, ikiwamo kuhusika na mabao 15 kati ya hayo ameipa Simba pointi 12 kati ya 47 zilizokusanywa na timu hiyo katika mechi 19 ilizocheza.

Kiungo huyo ameipa Simba pointi 12 katika ligi kupitia mechi dhidi ya JKT Tanzania waliyoilaza bao 1-0 lililofunga kwa penalti kabla ya kuinyoa KMC alipofunga mawili katika ushindi 4-0, pia alifunga penalti dhidi ya Dodoma Jiji na juzi tena dhidi ya Namungo alifunga mawili yote ya penalti wakati Mnyama akishinda mabao 3-0.

Wakati kwa upande wa Aziz Ki aliyehusika na mabao 12 msimu huu akifunga matano na asisti saba, mabao yake yote hayakuwa ya kuamua ushindi wa timu yake hivyo ameongeza idadi ya kutumia mabao mengi kwa timu yake ambayo imefunga mabao 50 kwenye mechi 20.

Wakati Ahoua akiwa kinara kwa kukusanya pointi, ni wazi bila yeye Simba ingekuwa na pointi 36 na kushika nafasi ya tano kwenye msimamo baada ya kutoa pointi alizoipa timu yake.

KZ 02

Kwa upande wa Yanga hakuna kinachobadilika kwani hakuna mchango wa mabao yake kwenye pointi zaidi idadi ya mabao ingepungua kutoka 50 wangekuwa na 45.


AZIZ KI KIMATAIFA

Wakati Ahoua akimfunika Aziz Ki Ligi Kuu Bara kwa kuikusanyia Simba pointi tisa, kiungo wa Yanga amefanya vizuri kimataifa na timu yake ilianzia hatua ya awali Ligi ya Mabingwa Afrika na kuishia hatua ya makundi amefunga mabao 4.

Aziz Ki alianza kufunga dhidi ya Vital'O ya Burundi wakati Yanga ikishinda jumla ya mabao 10-0, katika mechi ya kwanza Vijana wa Jangwani wakishinda 4-0, alifunga bao moja na ziliporudiana na Warundi kupigwa 6-0, Mwamba wa Burkina Faso alifunga tena bao moja.

Katika mechi za raundi ya pili, Yanga ilikutana na CBE ya Ethiopia na Aziz KI alifunga tena mabao mawili katika ushindi wa mchezo wa marudiano ambao Yanga ilishinda 6-0 baada ya ule wa kwanza ugenini kushinda 1-0 lililowekwa na Prince Dube.

Matokeo hayo yakaivusha Yanga hadi makundi ikipangwa Kundi A pamoja na Al Hilal ya Sudan, MC Alger ya Algeria na TP Mazembe ya DR Congo na hata hatua hiyo, Aziz KI aliendelea kufunga, japo timu hiyo ilishindwa kuvuka kwenda robo fainali.

KZ 04

Aziz Ki alifunga mabao mawili, likiwemo la pekee lililoizamisha Al Hilal ikiwa kwao mechi iliyopigwa Mauritania, lakini mapema alifunga dhidi ya TP Mazembe iliyokufa 3-1 Kwa Mkapa, wakati mengine mawili yaliwekwa kimiani na Clement Mzize. Hata hivyo suluhu katika mechi ya mwisho dhidi ya MC Alger iliizuia Yanga kutinga robo fainali kwa msimu wa pili mfululizo na kumfanya Aziz KI kufikisha jumla ya mabao sita.


AHOUA NAYE WAMO

Kwa upande wa Simba iliyopo hatua ya robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika, Ahoua amefunga mabao mawili, likiwamo la mchezo wa kwanza dhidi ya Bravos do Maquis ya Angola na kurudia tena dhidi ya CS Sfaxien ilipoifuata ugenini. Pia alisisti mara mbili na kuchangia timu hiyo kutinga robo fainali na jana droo ya hatua hiyo ilifanyika mjini Doha, Qatar.

Kwa upande wa ligi kuu, Ahoua anaisaka rekodi yake aliyoiweka akiwa na Stella Club d’Adjame msimu uliopita ya kufunga mabao 12 na amebakiza mabao manne tu kuifikia kabla ligi haijaisha.

KZ 05
KZ 05

Ahoua aliyejiunga na Simba Julai 3 mwaka jana akitokea Stella, msimu uliopita aliifungia timu hiyo mabao hayo na kuasisti tisa na kumfanya aibuke Mchezaji Bora wa msimu huo yaani MVP kabla ya kuja nchini na kwa sasa akiwa na Simba ameshafunga mabao 10 na asisti tano.

Wakati Aziz Ki akipambana kufikia rekodi yake msimu ulipita fundi huyo wa mguu wa kushoto aliibuka na tuzo mbili kubwa kwanza akichukua tuzo ya mfungaji bora wa ligi akimaliza msimu na mabao 21 akimuacha Feisal Salum 'Fei toto' aliyemaliza nyuma yake kwa mabao 19.

Mbali na kufunga mabao, pia Aziz Ki alikuwa mchezaji aliyeshika namba mbili kwa kuasisti akiwa na nane, ikiwa ni sawa na alivyofanya msimu uliopita na kushika nafasi ya pili nyuma ya kinara Kipre Junior aliyekuwa Azam aliyeasisti tisa kabla ya kusajiliwa MC Alger ya Algeria.

Tuzo hiyo ikazaa tuzo nyingine ndani yake akiibuka na tuzo ya Mchezaji Bora wa msimu (MVP) akiwabwaga wenzake akiwemo Fei Toto na tuzo hiyo inakuwa ya pili kwake nyingine akiichukua pale Asec Mimosas akiwa nako aliwahi kuisomba tuzo kama hiyo.