Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Anton Joshua mwanzo mwisho ajali iliyoua washkaji zake wawili Nigeria

JOSHUA Pict

Muktasari:

  • Vyanzo vinasema pambano lake lenye thamani ya Pauni 100 dhidi ya Tyson Fury liko hatarini kutokana na uwezekano wa majeraha ya ndani anayodaiwa kuyapata katika ajali hiyo na msongo wa kisaikolojia baada ya kushuhudia rafiki zake wa karibu wawaili wakifariki dunia katika gari alilokuwa akisafiri nao.

LAGOS, NIGERIA: HOFU kwamba majeraha aliyoyapata bingwa wa zamani wa ngumi za uzito wa juu duniani, Anthony Joshua, 36, katika ajali ya gari iliyotokea juzi huko Makun, Nigeria, ni makubwa kuliko ilivyodhaniwa awali na huenda yakamgharimu kurudi haraka ulingoni.

Vyanzo vinasema pambano lake lenye thamani ya Pauni 100 dhidi ya Tyson Fury liko hatarini kutokana na uwezekano wa majeraha ya ndani anayodaiwa kuyapata katika ajali hiyo na msongo wa kisaikolojia baada ya kushuhudia rafiki zake wa karibu wawaili wakifariki dunia katika gari alilokuwa akisafiri nao.

Inaelezwa kwamba kuna hofu kwamba majeraha ni makubwa, ingawa hadi jana taarifa za awali zilikuwa zikidai mbabe huyo wa masumbwi aliyeshinda mapambano 29 kati ya 33 aliyocheza, ameumia zaidi ndani ya mwili hususan kifuani. Joshua alikuwa amekaa katika siti ya nyuma ya dereva ndani ya gari hilo lililogonga lori kwa nyuma, huku rafiki zake wawili Sina Ghami na Kevin ‘Lateef’ Ayodele waliokuwa wamekaa viti vya kushoto mbele na nyuma wakipoteza maisha papo hapo.

JOSH 01

Bingwa huyo wa dunia wa uzito wa juu mara mbili alikuwa abiria katika gari aina ya Lexus jeusi lililogonga lori lililokuwa limesimama kwenye barabara kuu ya Lagos–Ibadan, eneo la Makun, Nigeria.

Vifo vya rafiki zake hao wawili wa muda mrefu vilithibitishwa usiku wa kuamkia jana, huku abiria wengine wawili waliokuwa kwenye gari hilo wakitoka bila kuumia.

Polisi wa eneo hilo walidai Joshua alipata majeraha ‘madogo’ na hali yake ilikuwa nzuri. Hata hivyo, vyanzo vilivyo karibu na bondia huyo vinasema kuna hofu kwamba madhara yanaweza kuwa makubwa zaidi kuliko ilivyotangazwa, vikidai kwamba kuna uwezekano ameumia mbavu na goti maeneo ambayo yalitajwa na mtu mmoja kutoka kwenye eneo ilipotokea ajali kutokana na jinsi majeruhi huyo alivyokuwa akilalamika wakati akisaidiwa kutolewa ndani ya gari.

JOSH 02

Video zilizorekodiwa kando ya barabara zilimuonyesha bondia huyo akikunja uso huku akigugumia kwa maumivu makali alipokuwa akisaidiwa kutoka kwenye gari lililoharibika na kupelekwa kwenye gari la polisi ili kuwahishwa hospitali.

Taarifa iliyotolewa na mmoja wa wasaidizi wa bondia huyo ilithibitisha vifo vya rafiki wawili wa Joshua ambao pia walikuwa sehemu ya maofisa wa kambi yake, huku mmoja akiwa amefanya naye kazi kwa zaidi ya miaka 10.

Alisema: “Kwa huzuni kubwa tunathibitisha vifo vya Sina Ghami na Kevin ‘Lateef’ Ayodele kufuatia ajali ya barabarani huko Lagos, Nigeria. Wote wawili walikuwa marafiki wa karibu na maofisa muhimu wa timu ya Anthony. Tunaomba kwa heshima familia zipatiwe nafasi na faragha katika kipindi hiki zinapokabiliana na habari hii ya kushtua na kuhuzunisha.

JOSH 03

“Anthony alipata majeraha katika ajali hiyo na alipelekwa hospitali kwa uchunguzi na matibabu; hali yake ni nzuri na ataendelea kubaki huko kwa uangalizi. Hakutakuwa na taarifa zaidi zitakazotolewa kwa sasa.”

Hata hivyo, taarifa kutoka Nigeria zinadai Rais Bola Tinubu aliwasiliana na Joshua kwa simu akiwa hospitali kumjulia hali na pia amewasiliana na familia yake iliyopo Uingereza kuipa pole, akiihakikisha kwamba bondia huyo yupo katika mikono salama ya matibabu.

Mapema usiku wa kuamkia jana maofisa wa Nigeria waliivithibitishia vyombo vya habari vya Uingereza kwamba Joshua alikuwa ‘na fahamu na alikuwa amezungumza na familia yake’ baada ya kutolewa kwenye mabaki ya ajali.

JOSH 04

Msemaji wa Jimbo la Ogun alisema: “Anthony Joshua na abiria mwingine walipelekwa haraka katika kituo maalumu cha matibabu jijini Lagos. Baada ya uchunguzi wa kina wa kitabibu madaktari wamethibitisha kuwa wagonjwa wote wawili wako katika hali thabiti na hawahitaji matibabu ya dharura kwa sasa. Timu kamili ya matabibu imeundwa na itaendelea kuwafuatilia kwa karibu.

“Anthony Joshua ana fahamu na amekuwa akiwasiliana na familia yake. Serikali za majimbo ya Ogun na Lagos zinafuatilia kwa karibu hali yake na zitahakikisha wahusika wanapata huduma bora za matibabu. Uchunguzi kuhusu mazingira ya ajali pia umeanza. Tunawashukuru wananchi kwa kuonyesha kujali na tunaomba faragha iheshimiwe kwa Joshua na familia yake wakati huu.”

JOSH 05

Watu watano walihusika katika ajali hiyo, huku picha zikionyesha gari likiwa limeharibiwa na milango kung’oka ilihali paa la juu likiwa limetobolewa na vyuma vya lori.

Picha za gari aina ya SUV lililoharibika vibaya zilitolewa na maofisa wa Nigeria, huku gari aina ya Mitsubishi linaloaminika kuwa sehemu ya msafara wa Joshua likionekana bila kuharibika umbali wa mita chache.

Video zilizo mitandaoni zinamuonyesha bingwa huyo wa zamani wa dunia wa uzito wa juu akiwa hana shati, akionekana  kuchanganyikiwa akiwa amekaa ndani ya gari lililoharibika na vioo vilivyopasuka.

Ajali hiyo iliyotokea saa sita mchana kwa saa za huko, imekuja siku 10 baada ya Joshua kumchapa Jake Paul huko Miami, Marekani katika pambano lisilokuwa la ubingwa, lakini lililovuta hisia za mamilioni ya mashabiki wa ngumi duniani sambamba na malipo manono kutoka kwa wadhamini mbalimbali ukiwamo mtandao wa Netflix.

JOSH 06

Chanzo kinadai kuwa gari alimokuwa Joshua lilikuwa likiendeshwa na dereva wa kukodi kwa ajali ya safari ya kwenda Shagama, Ogun yalipo makazi ya asili yao ambako pia wanaishi ndugu zake. Joshua ana asili ya Nigeria.

Inaeleweka kuwa Joshua amekwenda kutembelea familia nchini Nigeria kama sehemu ya mapumziko ya wiki moja, akiwa na mpango wa kurejea mazoezini kujiandaa na pambano la mwishoni mwa Machi ambalo huenda likapigwa Saudi Arabia dhidi ya mpiganaji wa kickboxing Rico Verhoeven kabla ya pambano lililopendekezwa dhidi ya Fury, Septemba au Oktoba, mwakani.

JOSH 07

Ingawa aina halisi ya majeraha ya Joshua bado haijulikani, inaaminika kuwa kuna shaka kubwa kama ataweza kurejea ulingoni haraka. Pia kuna suala la kisaikolojia baada ya tukio hilo lililosababisha vifo vya rafii zake hao aliokuwa akisafiri nao kila mahali alipokuwa akienda kwa shughuli rasmi na zisizo rasmi.

Picha zinaonyesha kuwa upande wa gari ambao haukuwa wa dereva ndio ulijibamiza kwenye lori katika barabara iliyo karibu na eneo ambako Joshua alisoma shule ya bweni alipokuwa mtoto.

Matokeo ya awali ya uchunguzi yanaonyesha kuwa gari la Joshua lilikuwa linaendeshwa kwa kasi zaidi ya iliyoruhusiwa kisheria na kisha likapoteza mwelekeo wakati wa kulipita gari jingine kulingana na mamlaka za eneo hilo.

Kamishna wa Polisi wa Jimbo la Ogun, Lanre Ogunlowo alisema: “Gari (la Joshua) liligonga gari lililokuwa limesimama.  Bahati mbaya kuna vifo viwili. Joshua alihudumiwa na wahudumu eneo la tukio kisha akapelekwa hospitali.”

JOSH 08

Polisi wa usalama barabarani wa Shirikisho la Nigeria walitoa picha za eneo la ajali ikiwemo moja iliyoonyesha kile kinachoonekana kuwa dimbwi kubwa la damu karibu na Lexus iliyoharibika, na katika taarifa walisema: “Matokeo ya awali yanaonyesha kuwa gari aina ya Lexus Jeep linaloshukiwa kuwa lililokuwa linaendeshwa kwa kasi zaidi ya kikomo cha kisheria katika eneo hilo lilipoteza mwelekeo wakati wa kulipita gari jingine na kugonga lori lililokuwa limesimama vizuri pembeni ya barabara.

“Sababu kuu za ajali ni mwendokasi na kupita magari kinyume cha sheria, ambayo ni makosa makubwa ya barabarani na yanaendelea kuwa miongoni mwa chanzo kikuu cha ajali mbaya za barabarani nchini Nigeria.”

Kikomo cha mwendo katika eneo la ajali kinatajwa kuwa ni kilomita 70 kwa saa.


SHUHUDA, NDUGU

Akizungumzia ajali hiyo, shuhuda mmoja aliliambia gazeti la Punch kuwa, “ulikuwa msafara wa magari mawili; Lexus SUV na Pajero SUV. Joshua alikuwa amekaa nyuma ya dereva akiwa na mtu mwingine pembeni yake. Kulikuwa pia na abiria aliyekaa pembeni ya dereva, hivyo kulikuwa na watu wanne ndani ya Lexus. Walinzi wake walikuwa kwenye gari lililokuwa nyuma yao kabla ya ajali.

Mmoja wa Joshua aliyeomba asitajwe jina, aliiambia BBC kuwa familia ilikuwa katika mshtuko.

“Tunaomba apone haraka na pia kwa waliopoteza maisha tunawaombea wapumzike kwa amani. Kwa kawaida (Joshua) huwa anakuja kipindi cha mwaka mpya. Hatukumuona, hivyo tulikuwa tukimtarajia,” alisema ndugu huyo.

Joshua alikuwa ameweka ‘stori’ kwenye akaunti yake ya Instagram saa chache tu kabla ya ajali akionekana hana shati kwenye video akicheza mchezo wa tenisi mezani na rafiki yake wa muda mrefu, Ayodele na aliambatanisha video hiyo na ujumbe: “@afya_huondoa mvuke wa tenisi.”

Joshua ambaye ana tattoo ya ramani ya mipaka ya Nigeria kwenye bega lake la kulia kwa muda mrefu amekuwa akisherehekea asili yake ya Nigeria. Bondia huyo ana asili ya Sagamu kusini-magharibi mwa Nigeria na alisoma shule ya bweni huko Ikenne zaidi ya kilomita 70 kutoka mahali ajali ilipotokea.