Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

"Amini mchakato” umezaa matunda! Umpende au umchukie Arteta anastahili

ARTETA Pict

Muktasari:

  • Kwa mtazamo huo, sehemu kubwa ya pongezi kwa mafanikio ya Arsenal kushinda Ligi Kuu England inapaswa kwenda kwa klabu yenyewe. Licha ya kuona mara kwa mara timu ya Arteta ikishindwa pale ilipohitajika zaidi, bodi iliendelea kumuunga mkono kocha huyo hasa kwenye usajili wa wachezaji.

LONDON, ENGLAND: Muda kama huu mwaka jana, Gary Neville alidai mafanikio makubwa zaidi ya Mikel Arteta akiwa Arsenal hayakuwa kutwaa Kombe la FA 2020, bali ni kuendelea kubaki kazini licha ya kupita misimu mitano bila kushinda taji kubwa.

“Tulidhani siku hizo zimekwisha, ambapo kocha angepewa uvumilivu wa aina hii,” amesema beki huyo wa zamani wa Manchester United kupitia Sky Sports.

Kwa mtazamo huo, sehemu kubwa ya pongezi kwa mafanikio ya Arsenal kushinda Ligi Kuu England inapaswa kwenda kwa klabu yenyewe. Licha ya kuona mara kwa mara timu ya Arteta ikishindwa pale ilipohitajika zaidi, bodi iliendelea kumuunga mkono kocha huyo hasa kwenye usajili wa wachezaji.

Muda na fedha ambazo wamewekeza kwa Arteta hatimaye zimezaa matunda, jambo lililothibitishwa baada ya kipigo cha Manchester City dhidi ya AFC Bournemouth Jumanne.

ART 04

Kwa jinsi mambo yalivyokwenda, walikuwa sahihi kabisa “kuamini mchakato”. Arteta aliwahi kusema kwamba mwishowe “atafanikiwa” na alichohitaji ni “muda kidogo”.

Ni wazi ilichukua muda mrefu zaidi kuliko alivyotarajia kocha huyo Mhispania, lakini amethibitisha kuwa ni mtu wa kauli yake. Hivyo basi, Arsenal wamemaliza ukame wao wa miaka 22 bila ubingwa si ushindi wa uvumilivu wa waajiri wake pekee, bali pia ni ushahidi wa ustahimilivu wake binafsi na uwezo wake wa kubadilika kwa busara.


“Jenga upya kila kitu”

Kama ambavyo Arteta amekuwa akisisitiza mara nyingi, Arsenal walikuwa kwenye hali mbaya kabla hajachukua usukani.

Msongo na kutoridhika uliokuwa umejengeka katika muongo wa pili wa utawala wa miaka 22 wa Arsène Wenger hatimaye uligeuka kuwa hali ya kukata tamaa mwishoni mwa kipindi kibaya cha Unai Emery kama kocha mkuu.

ART 03

Bila shaka, inaweza kusemwa kwa urahisi kwamba kama Emery angepewa kiwango kilekile cha sapoti alichopewa Arteta, kuna uwezekano mkubwa angepata mafanikio yanayofanana na mrithi wake. Kama alivyoonyesha baadaye akiwa na Villarreal CF na Aston Villa, Emery ni mmoja wa makocha bora kabisa wa soka la kisasa.

Hata hivyo, alikuwa tayari amepoteza imani ya mashabiki muda mrefu kabla ya kufukuzwa kazi tarehe 29 Novemba 2019. Hata kuteuliwa kwa mchezaji wa zamani kipenzi cha mashabiki, Freddie Ljungberg, kama kocha wa muda hakukuweza kuondoa hali ya huzuni na kukata tamaa iliyokuwa imeitanda klabu hiyo.

Arteta bado anakumbuka vizuri hali hiyo alipoitembelea mara ya mwisho Emirates akiwa kocha wa Manchester City, siku tano tu kabla ya kutangazwa rasmi kuwa kocha mpya wa kudumu wa Arsenal.

"Taswira ile, hisia za uwanjani, kuona karibu asilimia 50 ya viti vikiwa tupu, ilinikaa sana moyoni," alikumbuka.

"Nilisema, ‘Kwa hali hii, hakuna mradi wowote hapa. Hii haiwezi kufanya kazi.’

ART 02

“Kwa bahati mbaya, hali ilizidi kuwa mbaya haraka sana kwa sababu baadaye janga la COVID-19 likatokea. Badala ya asilimia 50 ya mashabiki, tukawa na sifuri. Hilo lilifanya kazi kuwa ngumu zaidi. Baada ya hapo tulilazimika kujenga upya kila kitu.”


“Inapendeza kuitazama”

Hakuna anayeweza kupinga kwamba Arteta alifanya kazi kubwa kuweka msingi wa timu yenye uwezo wa kushinda ubingwa.

Hata hivyo, siku zote kulikuwa na shaka ile ya ndani kuhusu kama kweli alikuwa mtu sahihi wa kuibadilisha Arsenal kutoka timu ya ushindani hadi mabingwa halisi.

Kama gwiji wa klabu hiyo, Thierry Henry, alivyokiri hivi karibuni kupitia Sky Sports:

"Nitakuwa mkweli, kuna kipindi nilikuwa nikihoji haya yote ya‘Amini mchakato'. Nilikuwa nataka kujua, ‘Tunaelekea wapi?’”

Hata msimu huu, kulikuwa na hofu kwamba Arsenal wangemaliza nafasi ya pili kwa msimu wa nne mfululizo  hasa baada ya kufungwa nyumbani na AFC Bournemouth Aprili 11, wakati wachezaji walionekana kuathiriwa na presha kutoka kwa mashabiki waliokuwa na wasiwasi mkubwa.

Lakini mashabiki walijitokeza kwa nguvu kwa ajili ya Arteta na Arsenal walipowahitaji zaidi.

ART 01

Mazingira ndani ya Uwanja Emirates katika mchezo wa ligi dhidi ya Fulham, pamoja na mechi ya marudiano ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa UEFA dhidi ya Atlético Madrid, yalikuwa ya kusisimua mno yakionyesha wazi jinsi hali ya klabu ilivyobadilika tangu kipigo cha 3-0 nyumbani dhidi ya Manchester City mwezi Desemba 2019.


Ni Mourinho zaidi kuliko Pep

Bila shaka, ukweli kwamba Arsenal hawajawa “wa kuvutia kutazama” kwa mtazamo wa soka safi umekuwa mjadala mkubwa msimu huu.

ART 05

Kwa kuwa ni mwanafunzi wa falsafa ya ukocha ya Pep Guardiola, wengi walitarajia Arteta angeitumia Arsenal kwa mtindo unaofanana na kocha huyo wa Katalunya.

Ni kweli, mwanzoni 'The Gunners' walionekana kama “nakala nyepesi ya Manchester City,” kama alivyoeleza Jamie Carragher, hasa baada ya kuwasajili wachezaji wa zamani wa City kama Gabriel Jesus na Oleksandr Zinchenko katika dirisha la usajili la kiangazi la mwaka 2022.

Hata hivyo, kumekuwa na mabadiliko makubwa ya kimkakati katika misimu mitatu iliyopita, na mabadiliko hayo yameonekana zaidi tangu kuanza kwa msimu huu.

Kwa mshangao wa wengi, Arteta ameikumbatia falsafa ya kushinda kwa gharama yoyote jambo lililosababisha kulinganishwa zaidi na Jose Mourinho kuliko Guardiola.

Arsenal kimsingi wamekuwa hodari katika kuchelewesha muda kupitia mipira ya adhabu kama walivyo hodari kufunga kupitia hali hizo.

Kipa David Raya mara kwa mara hujirusha chini kana kwamba ameumia ili kumpa Arteta nafasi ya kutoa maelekezo ya haraka pembeni mwa uwanja.

Pia, Arsenal walionekana kutumia kwa ujanja kanuni za tahadhari ya mtikisiko wa ubongo  msimu huu kufanya mabadiliko ya kujihami katika mchezo dhidi ya Wolverhampton Wanderers mwezi Januari.

Kwa namna fulani, hilo linaelezea vizuri kabisa sura mpya ya Arteta kocha ambaye sasa ameonyesha ukatili wa kimkakati na ujanja wa ushindi ambao hapo awali wengi hawakutarajia kuuona kwake.