Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zuchu na Harmonize waongoza kusikilizwa 2023

Muktasari:

  • Harmonize ameongoza upande wa wanamuziki wa kiume, akifuatiwa na Mbosso na Diamond Platnumz. Upande wa wasanii wa kike, Zuchu ndiye kinara, akifuatiwa na Nandy na Yammi.

Waimbaji wa Bongofleva, Harmonize na Zuchu wameongoza waliosikilizwa zaidi kwa mwaka 2023 katika jukwaa la kutiririsha muziki la Boomplay Music.

Boomplay Music Tanzania wametoa taarifa ya wasanii waliofanya vizuri katika jukwaa lao upande wa Tanzania pekee kwa kipindi cha kuanzia Novemba 1, 2022 hadi Oktoba 31, 2023.

Harmonize ameongoza upande wa wanamuziki wa kiume, akifuatiwa na Mbosso na Diamond Platnumz.

Upande wa wasanii wa kike, Zuchu ndiye kinara, akifuatiwa na Nandy na Yammi.

Akizungumzia hilo, Yammi ambaye amesainiwa The African Princess Label yake Nandy, amewashukuru mashabiki wake pamoja na lebo yake kwa hatua hiyo.

"Asanteni mashabiki zangu kwa kuendelea kunisapoti na naomba muendelee kunisapoti mdogo wenu, dada yenu, kijana mwenzenu, mtoto wenu.

"Nafurahi sana kuwa miongoni mwa dada zangu Nandy na Zuchu. Nawapenda sana na nashukuru kwa sapoti yenu kubwa kwangu mashabiki zangu, asante uongozi wote wa The African Princess Label na Mziiki," amesema Yammi.

Utakumbuka Januari mwaka huu ndipo The African Princess ilimtambulisha Yammi akiwa ni msanii wa kwanza kusainiwa, huku akiachia EP moja ‘Three Hearts’ (2023) yenye nyimbo tatu.

Vilevile katika ripoti hiyo ya Boomplay Music 2023, albamu zilizosikilizwa zaidi ni ‘Khan’ ya Mbosso, ‘Made For Us’ ya Harmonize na ‘The Kid You Know’ ya Marioo.

Upande wa nyimbo za Bongofleva ni 'Puuh' wake Billnass akimshirikisha Jay Melody, 'Utaniua' wa Zuchu, na 'Mahaba' wa Alikiba. Huku nyimbo zilizongooza kwenye chati zikiwa ni Sawa (Jay Melody) kwa wiki nane, Wewe Hapo (Lony Bway) ft. Marioo, 'Puuh' (Billnass) ft. Jay Melody, hizi mbili zilikaa namba moja kwa wiki sita.