Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zuchu anapita mlemle kwa Jay-Z na Beyonce

ZUCHU Pict

Muktasari:

  • Penzi hilo limekuwa na nyakati za kuachana na kurudiana, jambo ambalo limewafanya mashabiki kuhisi kama wanatumia ‘kiki’ au ni sehemu ya biashara ya burudani.

PENZI la Zuchu na Diamond Platnumz ni kati ya uhusiano unaozungumziwa sana Afrika Mashariki katika miaka ya karibuni ukizingatia wote ni mastaa wakubwa wa muziki na wanatoka kwenye lebo moja ya muziki (WCB Wasafi).

Wawili hao mara kadhaa wamekuwa wakihusishwa kuachana na mitandao ikiwazungumzia sana wanarudiana tena.

Penzi hilo limekuwa na nyakati za kuachana na kurudiana, jambo ambalo limewafanya mashabiki kuhisi kama wanatumia ‘kiki’ au ni sehemu ya biashara ya burudani.

Mara kadhaa Zuchu ameandika ujumbe wa maumivu na kuonekana kufuta picha za Diamond kwenye Instagram lakini baada ya siku kadhaa unawakuta pamoja.

Penzi hilo kwa kiasi kikubwa linamuongezea soko Diamond, kwa kuonekana na msanii wake wa lebo kama mpenzi, jambo linalovutia mashabiki.

Zuchu ameweza kujijengea jina haraka kwa kuhusishwa na Diamond limemuongezea wafuasi wengi na kumpatia matangazo kadhaa.

Uhusiano wao ulianza kwa uvumi na ukaribu wao kwenye kazi mbili za Cheche na Litawachoma zilizotoka mwaka (2020).

Jambo hilo limekuwa likitokea kwa baadhi ya wasanii duniani ambao wamekuwa wakifanya kazi pamoja na baadaye kuoana na kuongeza wafuasi wengi.

Hivyo ni kama Zuchu na Diamond wanapita njia za mastaa hawa duniani.

ZUCH 01
  1. Jay-Z na Beyonce

Uhusiano wao ulianza mwishoni mwa miaka 1990 ila walipotoa kolabo yao wa kwanza, 03 Bonnie & Clyde (2002) iliyosampo wimbo wa 2Pac, Me and My Girlfriend (1996), ndipo tetesi za kuwa pamoja zilishika kasi ingawa walikanusha wakati huo.

Baada ya tetesi za muda mrefu kuwa wasanii hao wanatoka pamoja kimapenzi Aprili 4, 2008 wakafunga ndoa rasmi ya siri.

Umaarufu wa ndoa yao uliwafanya kuendelea kuwa maarufu duniani na kupata soko kubwa la matangazo kwenye kampuni kubwa.

Wakati huo walikuwa wanafanya kazi lebo moja ya Roc-A-Fella ambayo pia Jay Z ni mmoja wa wamiliki.

Kama ilivyo kwa Diamond ambaye anafanya kazi lebo moja na Zuchu lakini Chibu akiwa ndio Mkurugenzi wa lebo hiyo kama ilivyo kwa Jay -Z.

Imetimia miaka 17 sasa tangu Jay Z, 55, na Beyonce Knowles, 43, kufunga ndoa Aprili 4, 2008, hadi sasa harusi yao ni moja ya mambo yanayojadiliwa sana kutoka katika familia hiyo ya The Carters kutokana na jinsi walivyotekeleza jambo hilo.

ZUCH 02

2. Rihanna na Chris Brown

Mwaka 2007 wawili hao walianza uhusiano ingawa haikuwekwa wazi na wakasema ni marafiki tu wa karibu.

Baadaye wakatangaza kuwa wako kwenye huba na ikumbukwe kipindi hicho walikuwa kwenye lebo moja ya Def Jam Recordings.

Hata hivyo, uhusiano wao ulivunjika kwa mara ya kwanza mwaka 2009, baada ya tukio la ugomvi wa kimwili alilolifanya Chris Brown kumpiga Rihanna usiku wa tuzo za Grammy, jambo ambalo lilipewa uzito mkubwa kimataifa.

Mwishowe Chris Brown alikamatwa na baadaye kufungiwa kuhudhuria baadhi ya matukio ya muziki kwa muda.

Baada ya hapo, walirudiana kwa muda mfupi mwaka 2012–13, lakini hawakudumu wakaachana.

ZUCH 03

3. Cardi B na Offset (Migos)

Wamarekani hao wawili walianzauhusiano muda mrefu na mwaka 2017 wakaoana na mwaka 2019 wakatoa ngoma ‘Clout’ iliyofanya vizuri kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.

Kwa wakati huo walikuwa kwenye lebo moja

‘Quality Control Music’ kabla ya Offset kuhamia Migos na Cardi B kutimkia Atlantic.

Desemba 2023 Cardi B (31), alitangaza kuachana na Offset, 32, kwa madai ya usaliti katika ndoa yao yenye miaka minane sasa, huku wakijaliwa kupata watoto wawili.

Cardi B alivuma kimuziki baada ya kuachia albamu yake ya kwanza, ‘Invasion of Privacy’ (2018) iliyofanya vizuri na kumfanya kuwa msanii wa kwanza wa kike kushinda tuzo ya Grammy katika kipengele cha Albamu Bora ya Rap, huku ikishika nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard 200.

Miongoni mwa mafanikio kwenye kundi la Migos ambalo pia yupo Offset ni ngoma Bad and Boujee ft. Lil Uzi Vert – ilishika namba 1 Billboard Hot 100 (2017) na baadhi ya albamu kama Culture (2017) kushika chati kubwa nchini Marekani.

ZUCH 04

4. Ariana Grande & Big Sean

Ariana Grande na Big Sean wote ni raia wa Marekani na walianza uhusiano wa kimapenzi rasmi Oktoba 2014.

Walikutana mara ya kwanza mwaka 2013, waliposhirikiana kwenye nyimbo kama “Right There” kutoka kwenye albamu ya kwanza ya Ariana.

Mwaka uliofuata (2014), walionekana karibu sana na hatimaye kuthibitisha kuwa wako kwenye uhusiano na Aprili 2015, walithibitisha kuachana wakidumu kwa miezi minane.

Kapo hiyo ilizungumzwa sana wakafanikiwa kufanya kolabo mbili ambazo ziliendelea kuwaweka midomoni mwa mashabiki wa muziki wao kipindi hicho wakiwa pamoja kwenye lebo ya Republic Records.

Ariana ni miongoni mwa wasanii waliopata mafanikio makubwa duniani wakichukua tuzo kama Grammy, American Music Awards, MTV VMAs, Billboard Music Awards na nyinginezo.

Wimbo kama “Thank U, Next” ulishika namba 1 kwenye chati za Billboard na kuandikwa kama wimbo wa wanawake wenye nguvu baada ya kuachiwa rasmi.

Rapa Big Sean miongoni mwa tuzo kubwa alizobeba kwenye muziki wake ni pamoja na Grammy Awards, BET Awards,MTV Video Music Awards naBillboard Music Awards.